2. Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Julai, 1990.

Maono:

Naona Mwanga mweupe ukishuka chini kutoka angani; ukipitia katikati ya mawingu. Nikawa nahisi uwepo wa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mwanga mweupe unashuka chini

Maono:

Kisha kutoka ndani ya huo Mwanga; Nyota nyeupe ilijichomoza.

Maono:

Niliona hiyo Nyota nyeupe iliyojichomoza ikiruka yenyewe angani. Kisha baada ya hapo niliona hiyo Nyota nyeupe, ikiwa inaelea na kuvinjari juu ya Wingu Kubwa Jeupe.

Nilijua kuwa wingu hilo ni sehemu ya juu ya wingu la mlipuko wa kinuklia; kwani nilikuwa nafahamu sura ya wingu la mlipuko wake. Hata hivyo nilijifanya kama sielewi ni kitu gani hicho. Wakati wa maono haya nilijua wazi kuwa ni Yesu anaongea nami; ingawa sielewi jinsi nilivyo fahamu. Ila nilijua wazi wazi kuwa ni Yeye. Alikuwa anaongea nami kwa kuweka mawazo ndani ya akili yangu. Hapakuwa na sauti yeyote tuliyobadilishana. Tuliwasiliana kwa mawazo. Jambo hili lilinistua sana; kwa sababu sijawahi kuwa na maono ya aina hiyo kabla. Nakumbuka nilitishika sana; kwani nilijua ni nani anayeongea nami sikupenda nilicho kuwa nakiona. Nilifanya kila njia ya kukwepa swala la wingu hilo lenye umbo la uyoga, lakini Yeye, hakuniacha nisiitazame maono haya ya wingu la uyoga. Haya maono ya wingu la uyoga nadhani yalichukua muda wa kiasi cha dakika kumi na tano au ishirini hivi; kwa sababu mimi nilikuwa na jaribu kulikwepa swala hilo. Sikumbuki ni kwa sababu gani nilikuwa nakwepa jambo hilo, lakini Yeye hakuniachia mpaka nilipo salimu amri; na Yeye kisha alinionyeshea kila kitu.

Maono:

Nilikuwa naweza kuona ile Nyota juu ya mlipuko wa kinuklia nami nikaanza kulia. Kisha nikamkasirikia sana nakumwabia anionyeshee kila kitu na wala asinifiche chochote. Kilichofuata ni kuwa niliona pande la kioo safi kubwa kama futi moja hivi kwa upana na matone juu yake.

Maono haya ya pande kubwa la glasi angavu yalinifanya nizidi kukasirika zaidi; kwani baada ya kuona mlipuko wa kinuklia sasa naonyeshewa kitu ambacho hakieleweki. Kilichofuata baada ya hapo kilikuwa ardhi. Nilipokuwa bado natazama, ardhi hiyo; ilifumuka na kisha kitu kikajitokeza mfano wa jiwe angavu kama kioo kama kilivyo hapa chini. Kilikuwa kama futi moja kwa mpenyo na yenye urefu wa inchi kumi na nane hivi, juu yake kilikuwa na kofia angavu ya mviringo na kilicho chongoka kwa juu kwa mfano wa koni ya aisikrimu kama kilivyo hapo chini.

Maono hayo nayo sikuyaelewa pia. Jiwe hilo mara likageuka na kuwa mfano wa jengo la kijeshi la Marekani "Pentagon".

Kutoka jengo la Pentagon

 ikageuka kuwa sura ya koni ya aisikrimu

Nayo kile kikofia cha mviringo na kilicho chongoka kwa juu; kikageuka kuwa mfano wa bara la Amerika ya Kusini kama kilivyo hapo kwenye mchoro.

Ilibadilika kutoka sura hii

Nakuwa na sura hii

Kutoka Amerika ya Kusini na kuwa na sura hii

 

Kutoka Afrika ikwa na sura hii

Kisha kutoka sura hii

 

Nakuwa na sura hii

Maono:

Bwana alinionyeshea nchi ya Uholanzi kwa mfano wa mshine ya kipepeo kinacho peperushwa na upepo.

Uholanzi

 

Maono:

Kisha Alinionyeshea nchi ya Misri; kwa kunionyeshea picha ya Simba Mtu; yule maarufu anayejulikana kama "The Egyptian Sphinx" kama alivyo hapa chini.

Sanamu ya Simbamtu wa Misri

 

Maono:

Ghafla nikaona Piramidi tatu zikiwa zimerushwa angani. Nilikuwa naziona kutoka kwenye upande wa chini kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini.

Maono:

Maono yaliyofuata yalikuwa ya wingu kubwa sana jeusi; lililokuwa likitokea kushoto na kuelekea kulia; Kisha wingu lingine kubwa sana njeupe lilotokea kutoka kushoto likielekea kulia. Mawingu haya mawili; kisha yalikutana katikati, na wingu lile njeupe liliimeza wingu jeusi.

 

Maono:

Kisha anga likageuka kuwa ya rangi ya bluu nyembamba; ikiwa na upinde mzuri wa mvua angani. Ingawa siwezi kujieleza hali hiyo halisi, lakini nilijisikia na amani sana na kila nilicho kiona kilikuwa na amani kubwa.

Maono:

Maono yaliyofuata yalinitatiza kidogo, kwani nilijisikia niko kwenye anga za juu na nilikuwa naona Sayari yetu ya Dunia. Ghafla nikaona mwamba mkubwa uliokuwa uking’aa kwa moto unatokea. Nilikuwa naona uweusi wa gamba la juu; lililokuwa limepoa na gamba la ndani lililokuwa linawaka bado kwa mwanga mwekundu unaong’aa. Mwamba huo mweusi ulipogonga Dunia ulidunda kama mpira juu ya Nchi na Mabara na Jimbo lile la Texas; ambazo niliziona hapo kabla kwenye maono niliyoyaeleza hapo juu.

MWAMBA MWEUSI UKAIDUNDA DUNIA

Maono:

Kila kitu kilitulia kwa sekunde moja, kisha ghafla mwanga mkali kama wa tochi ulipenya kutoka uweusi wa anga za juu. Baada ya hayo; kukawa na mwanga mwingine kama wa tochi ukielekea kwenye Sayari yetu ya Dunia. Hiyo ilifuatiwa na mwanga au mwali wa pili, wa tatu na kabla sijaelewa miali hiyo ni nini nikastukia anga yote ikawa imejaa miali hiyo ya moto. Yaliangukia kwenye dunia kama mvua na kunyunyizia umbo lote la dunia.

Dunia

Maono:

Katika maono yaliyofuata, niliona dunia kama unavyoona ukiwa katika anga za juu. Ilionekana kuwa nzuri sana; ikiwa na mawingu meupe na maji ya bahari yake yenye rangi ya bluu na kijani kibichi, nilikuwa hata naona umbo la hali na hewa yake. Sikuweza kuelewa wapi Yesu alipotokea; ila ghafla nikaona amesimama karibu nami wakati naangalia dunia. Kisha ghafla dunia ikatokomea na nilichoweza kukiona ni uweusi wa anga za juu. Nakumbuka nilianza kubishana na Kristo; kwa sababu dunia ilipotea tu na kugeuka kuwa utupu. Yeye alinionyeshea dunia tena mara ya pili na kila wakati ilipotea nakuwa utupu kama hapo mwanzo. Hii iliniudhi sana na ndiyo maana niliendelea kubishana Naye.

Kabla Baadaye

Dunia nzuri yenye rangi

Anga za juu nyeusi Anga za juu nyeusi

Maono:

Kisha ghafla dunia mpya ilijitokeza, lakini dunia hii mpya ilikuwa kubwa mara tatu au nne ya dunia yetu hii. Ilikuwa na mwanga mweupe ulioizunguka kwa juu na katikati yake ilikuwa nyeusi.

Mwanga mweupe

Dunia mpya Anga za juu nyeusi

Maono:

Mpaka wakati huo; sikujua la kuamini, hivyo nikamwambia Kristo, "Siamini. Nataka kwenda kule chini ilinijionee mwenyewe kilichopo pale." Kilichofuata ni kwamba wote wawili; tulianza kushuka kuelekea kwenye Sayari ile. Tulipoanza kuingia kwenye anga lake, nilichokiona ni mawingu haya meupe yakizunguka angani, ila yalikuwa siyo mawingu ya kawaida niliyo ya zoea kuyaona. Sayari yenyewe ilikuwa haionekani kwa sababu mawingu haya yalikuwa yameifunika Sayari hii. Mawingu haya yalikuwa tofauti; kwani yaelekea kila wingu moja lilikuwa likijiendea pekee, na kila moja lilikuwa limejitenga na mwenziwe. Wazo lililonijia ni kuwa nilihisi haya hayakuwa mawingu; ila roho mbalimbali, ila kwa kweli sikujua hasa ni nini. Haya yote yalitokea wakati mimi na Kristo tulipokuwa tukishuka kwenye Sayari, sasa kwa kuwa nilikuwa sioni kitu nikamwambia siamini na nikamwambia anipeleke chini zaidi kwenye sayari.

Dunia mpya imefunikwa na mawingu

Mawingu yaliyokuwa yanajiendea kila mmoja kikwake

Maono:

Nilichokiona pale kilikuwa ule mwanga mkubwa sana juu angani na juu ya bahari hii kubwa sana ya maji. Haya maji hayakuwa na mawimbi wala mtikisiko wowote. Ilikuwa inaonekana kama kipande kikubwa sana cha kioo.

Mwanga mkubwa mweupe

Maji mengi sana yaliyotulia kama ziwa, lakini ilikuwa bahari

Maono:

Wakati wa maongezi yangu na Kristo; nilikuwa naendelea kumwambia kuwa siamini; kwakuwa hapakuwa na ardhi au udongo. Kila kitu kilikuwa cha ajabu kwa kuwa tulikuwa tumesimama juu ya maji. Ghafla na bila onyo lolote pale tuliposima, lile umbo la mviringo uliochongoka juu kama aisikirimu au mlima niliyokwisha ielezea hapo juu, kilijitokeza kutoka kwenye maji hayo, ukianzia na kulikochongoka bila kuleta mawimbi na karibu na sisi. Ilianza kukua mpaka ikawa kama mlima wenye urefu labda wa maili moja kwenda juu angani. Kisha bila onyo Kristu alipotea na maono yakaishia pale.

Koni ya Aisikirimu

Maji mengi sana


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.