3. Matukio na Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 23 Julai 1990.
(Nilipokea Matukio/Maono haya; siku tano baada ya yale maono ya tarehe 18 Julai 1990. Haya maono/mtukio yanaelezwa kutoka kumbukumbu ya kichwani kwa sababu kumbukumbu pekee niliyonayo ni ile ya michoro niliyo kuwa nimeyachora wakati wa maono hayo.)
Wakati wa maombi nikiwa nimelala kitandani
mwangu, niliona maono ya ile koni ya aisikirimu ambayo ilikuwa na urefu wa kama
maili moja iliyonyanyuka kutoka majini ambayo niliiona katika yale maono ya
kwanza (No. 2).

Nilianza kuomba na kitu kilichofuata kilikuwa kiti cha Enzi au cha Kifalme ambacho hakikuwa cha kawaida, lakini niliweza kukiona kutoka sehemu mmoja tu. Haikujalisha jinsi nilivyo jaribu kukiangalia lakini sikuweza kufanikiwa kuangalia upande zaidi ya ule nilioruhusiwa kuangalia.

Mwanga mweupe sana ulijitokeza mara juu ya kile kiti cha Enzi kikiwa na Nyota Nyeupe yenye kung’aa sana ndani na katikati ya Mwanga huo Mweupe.

Nilipokuwa nakiangalia Kiti hicho cha ajabu cha Enzi; ile koni ya aisikrimu ilikuja chini ya hicho Kiti cha Enzi na kikawa kama stuli cha hicho kiti cha Enzi. Mara kikageuka kuwa kama kiweko/stuli mfano wa Piramidi kikiwa na maelfu ya ngazi nyingi iliyokuwa ikipanda kwenda juu kuelekea kwenye kiti cha Enzi.

Wakati nikiwa najaribu kutafakari maono hayo, mara sura ya Taji ikatokea ikiwa na Nyota Tatu katikati yake na naami vitufe vidogo kumi na viwili juu ya miinuko iliyokuwa kwenye taji na ikiizunguka nyuma yake.

Maono mengine yaliyofuata niliyoyaona yalikuwa kutoka hewani. Nilikuwa mmoja kwa mmoja juu ya Kiti cha Enzi. Niliweza kukiona Kiti cha Enzi kutoka juu ya bahari ya maji maangavu sana yakiwa na wingu la roho ya kiizunguka kiti hicho cha Enzi kwa kwenda kinyume na mkono wa saa.

Kukutana na Baba Yehova kwa mara ya kwanza
Mwanga fulani Mweupe sana ulitokea. Mwanga huo ulikuwa mkubwa sana kuliko ule uliokuwa na nyota ndani yake. Mwanzoni mwanga huo ulikuwa mkubwa sana nikadhania kuwa labda ilikuwa Dunia mpya ikimeremeta. Mara kwa namna fulani nikajikuta nauangalia nikiwa juu angani nikiangalia chini. Nikadhania labda naangalia ndani ya moyo wa Sayari. Ilikuwa inaonekana kuwa na nguvu nyingi, lakini ilipoanza kuhema kama moyo wa binadamu ndipo nikatambua kuwa siyo moyo wa Sayari.

wakati mawasiliano ya akili kwa akili ulipoanza kutokea, ulivuta umakini wangu na usikivu wangu. Ndipo Sauti ikasema "Je unajua Mimi ni Nani?"
Nikasema, "Wewe ni Baba?"
Nayo Sauti ikasema, "Ndiyo, Mimi Ndimi. Unataka tuzungumze? "
"Nadhani ndio, hakika," Nilisema.
Ndipo Baba alisema, "Je, unataka kuniuliza kitu fulani?"
Wakati huo nilikuwa nimezidiwa na shauku, lakini sikuweza kujua la kusema au kuuliza.
Hivyo nilisema, "Nieleze Utatu Mtakatifu kwani nashindwa kuuelewa kinaganaga."
Kitu kilichofuata nilichokiona kilikuwa Mwanga mweupe ukijipenyeza kutoka katika ule Mwanga Mkubwa na Nyota Nyeupe ikatokea katikati yake.
Kisha Baba akasema "Je, unamjua huyo ni nani?"
"Huyo ni Mwana, Yesu Kristo." Nilisema kwa kujiamini, kwa kuwa nilisha wahi kuiona kabla.
Baba akaniambia, "Hiyo ni sawa. Kisha Mimi ni Nani?"
"Wewe ni Baba," Nikasema. "Kisha Roho Mtakatifu ni nani?" Nikauliza.
Kisha nikaonyeshewa mistari mitatu au mine zikiunganisha Mianga hiyo Miwili inayong’aa sana.
"Sisi ni Watatu na tuko mbali mbali, Sisi tu Mmoja." Baba akasema.
Siku kukubali kujionyesha kuwa sijaelewa, lakini bado nilikuwa sijaelewa na wala sikutaka nionekane kuwa mjinga.
Hivyo nikasema, "Sawa."

Baba akasema, "Je, unataka kuona Nguvu Zangu ? "
Nikasema, "Sawa."
Kilijofuata nikuwa ule Mwanga Mkubwa Mweupe ukaanza kukua kuwa Mkubwa na kuendelea kuwa Mkubwa zaidi. Ghafla na mimi nikawa ninakua na Mwanga huo kwa kasi ile ile ya ule Mwanga Mweupe. Nikawa naona Dunia mpya ikigeuka kuwa ndogo jinsi Mwanga ule unavyokuwa mkubwa. Na nyota za angani zikaanza kuwa ndogo jinsi Mwanga ule Mweupe ulivyo kuwa unazidi kuwa mkubwa na kuendelea kukua. Nilikuwa naona jinsi Ulimwengu ulivyozidi kuwa mdogo wakati Mwanga ule ulivyokuwa unaendelea kuwa mkubwa na kuzidi kukua, Ulimwengu ukawa sawa na kichwa cha pini na mwanga ukaendelea kukua na kukua. Malimwengu baada ya Malimwengu vikanywea na kuwa utupu lakini Baba aliendelea kukua kwa kasisi kubwa sana. Kwangu mimi ilionekana kila kitu kilinywea nakuwa utupu na Baba Yeye aliendelea kuzidi kukua na kukua, Mwili wangu na roho yangu ilishindwa kuchukua ukweli huo ya yale yanayotokea. Ilibidi nisema, "SIMAMA! Nimeshindwa kupokea zaidi. Unaweza kunionyeshea zaidi wakati mwingine, siwezi kustahimili zaidi kwa wakati huu sasa. Nimeelemewa."
Kisha Baba alisema, "Mimi ni kila kitu, lakini Kila kitu."
Hivyo kila kitu ghafla kikaacha kukua na tukazungumza kuhusu shetani
Nikauliza, "Kwanini una mwachia shetani kufanya mambo haya mabaya Duniani, nakuwaumiza wengi sana, na hali nionavyo mimi kwa nguvu ulizonazo siyo kazi kubwa kumkomesha yeye?"
"Vitu Fulani inabidi vitokee kabla vitu vingine kutokea na kila kitu kina mipangilio yake. Tutaongea nawe tena baadaye kidogo." Alisema.
Kisha Maono/Tukio ikasemama.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )