34. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Januari 1991 katika lugha ya Kiingereza na Kihispania na Lugha isiyoeleweka.

Ilani muhimu:

Tafadahili soma Unabii huu kwa umakini mkubwa na kuamua kwa macho ya Yesu Kristu wa Nazareti na kwa Biblia. Unabii huu nilipewa muda mchache baada ya Mchungaji alipojaribu kunikamata na kuniwekwa chini ya ulinzi kwenye nyumba ya mzee wa kanisa, baada ya kuomba maombi kutoka kwa mzee wa kanisa. Wakati wa vita vya kiroho, ambavyo vilizuka wakati wa maombi hayo, Mzee huyo aliomba msaada kwa Mchungaji Mkuu iliasaidie kuongoza maombi hayo, baada ya kufika yule mchungaji alichukua mamlaka ya nyumba hiyo, ninacho kifahamau baada ya hapo ni kuwa mimi nilizungukwa na polisi watano.

Unabii huu una maneno Fulani ya kutiliwa mashaka, ambayo nina hisi hayaendani na Biblia. Kwahiyo, ninakwenda kuwaonyesheeni kwa kuyaweka kwenye mibano kama ifuatavyo { }. Maelezo yangu yatakuwa kwenye mibano kama hivi ( ); Maneno ya kishetani katika mibano hii [ ]. Sababu pekee ya kuweka Unabii huu hapa ni kwa sababu inahusu kujaribu roho zote, na inaonyesha jinsi nilivyofanya wakati wa Unabii huu.

Kihispania:

Mtazame Mwanangu. Mwanangu Yesu. Mwanangu Yesu. Ndiyo, Wanangu wa Kiume na wa Kike. Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Huyu ni Baba yenu. Baba yenu, Mungu wenu, Mungu, Mungu wenu, tazameni. Tazame ninayo waambia ninyi. Dunia hii, Dunia hii lazima ibadilike, inabidi ibadilike Wanangu wa Kiume na Kike, kwani isipobadilika shetani atakwenda kushinda, lakini hawezi kuwashinda wote. Kwani wale watakaoenda na Yesu, na Yesu, Mwanangu watakwenda kujiokoa, lakini leo kuna watu wengi wenye vichwa vigumu. Wanataka kusikia tu yale wanayo ya penda. Ni aibu gani! Ni aibu gani! Ni aibu gani Wanangu wa kike na wa kiume. Huyu ni Baba ni Baba yenu! Huyu ni Baba yenu! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize

Kiingereza:

Unisikilize Ray, huyu ni Baba yako. Huyu ni Baba yako, Ray! Zijaribu roho. Zijaribu roho. Endelea kuzijaribu kwa sababu utashambuliwa tena. Usijali niko pamoja na wewe…

Hii ni sauti ya kishetani:

[uko mikononi mwangu Bwana, uko mikononi mwangu]......

Ray: Je, Yesu alikuja katika mwili....? Je, Yesu wa Nazareti alikuja katika Mwili....? Je, Yesu wa Nazareti alikuja katika Mwili....? (Hapakuwa na jibu. Kwa hiyo nikasema,) "Nakufunga, na ninakulaani katika Jina la Yesu Kristu wa Nazareti." "Sasa, nenda popote pale ambako Yesu atakapo kupeleka." Je, Yesu wa Nazareti alikuja katika Mwili....?

Bwana: "Ndiyo, Ray." Yesu wa Nazareti alikuja katika mwili.

Ray: Je, Yesu Kristo wa Nazareti alikufa kwa ajili ya dhambi zetu juu ya msalaba?.....

Bwana: "Ndiyo, Ray!"

Ray: Je, Yesu Kristu alifufuka siku ya tatu?.....

Bwana: "Ndiyo, Ray!"

Ray: Je, Yesu Kristu wa Nazareti amekaa mkono wa kulia wa Baba?....

Bwana: "Ndiyo, Ray!"

Ray: Je, Yesu Kristu wa Nazareti anastahili heshima zote, utukufu, na mamlaka na ukuu sasa na hata milele?....

Bwana: "Ndiyo, Ray,na kisha zaidi na zaidi. Yesu Kristo ni Mwanangu. Yeye ni Mwanagu, Ray.

Endelea kuzijaribu roho, Ray. Endelea kujaribu roho kwa sababu utaendelea kushambuliwa. Zitajaribu kukupotosha iliuende kwenye njia ya upotofu, lakini Unisikilize Mimi, Ray. Unisikilize, fungua masikio yako na macho. Kwani huyu ni Yehova anaongea nawe, Ray.

Unajua kilichotokea leo na Mchungaji. Siyo kosa la Mchungai X. Yeye anashinikizwa na nguvu za nje, lakini inakubidi ukumbuke, Ray, yeye ni kiongozi wa kundi Langu pale. Yeye ni kiongozi wa kundi Langu pale, lakini msikilize yeye ila usifanye kama yeye anavyo fanya. Anatatizo la majivuno! Ana kifua kikubwa na anapenda kujikweza sana. Hajiamini. Anabusara nzuri, lakini usiku wa leo amenipiga. Ameiachia kupenda sifa na majivuno yamshinde. Ameachia kiburi na kichwa ngumu chake kimtawale.

Kwa hiyo ni sikilize, Ray. Hivi ndivyo nitakavyo mfanyia. Sintakwambia lini, ila nakwambia uwezo wake wa kiakili utazidi kuwa mgumu. Atazidi kujisikia kutokujiaamini. Wasi wasi wake utazidi kuongezeka. Ufahamu wake utazidi kuwa kwenye mstari. Kuna wakati atajisikia amerukwa na akili. Nakueleza hayo Ray, iliumwangalie. Wewe umwangalie na kisha ujifunze.

Ikiwa Mchungaji anakupinga, wakati wewe unatoa Unabii au kama Mimi naongea kupitia kwako kwa lugha ngeni, anakwenda kinyume Nami, Mungu Yehova. Kwa hiyo wewe umwangalie. Usijaribu kumwombea, Ray, mwachilie! Mwachilie! Ulikuwa unafanya tu Niliyo kuagiza.

Wewe uliomba maombi, yeye akaita Polisi. Huyo siyo aina ya viongozi Ninaotaka waongoze kundi Langu. Hivyo wewe mwangalie Ray. Wewe umwangalie nauone kitakachotokea. Haitasaidia kumwombea au kufunga kwa ajili yake. Alikuwa na uhuru wa kufungua akili yake, macho yake, na masikio yake, lakini alikuandama wewe kwa kisasi, kisasi ilikuwa iwe juu Yangu, kwa sababu haikuwa wewe hapo Ray, ilikuwa Baba yako, Roho Mtakatifu, na Kristu. Nataka wewe ujifunze, nataka wewe ujifunze kutokana na uzoefu huu, Ray.

Unakua sana. Najua, na nina soma moyo wako. Ulikuwa uende jela kwa ajili Yangu, ulikuwa uende jela kwa ajili Yangu. Unajua , Ray, hiyo inaipasha joto Moyo Wangu, Lakini sinta ruhusu hilo litokee. Sinta ruhusu hilo liende mbali. Wewe ni Nabii Wangu, wewe ni Mtume Wangu. Nakufundisha, Ray. Unisikilize Mimi, mpaka hapa, umefanya kila kitu nilicho kuambia ufanye, mpaka vitisho vya kwenda jela.

Hivyo, kuanzia leo, mambo yataanza kuonekana mazuri kwako, Ray, kifedha, kiroho, na yule mwanamke niliye kuahidi, ataanza kukaribia, lakini Nataka unisikilize, Ray. Sitaki mambo haya yakuvimbishe kichwa, lakini mwangalie Mchungaji X, Kwa sababu kutakuwa na Wachungaji wa aina hiyo kama Mchungaji X baada ya hapo wengine watakuwa wazuri, wengine hawata ona tofauti wengine watakuwa wachungu.Wewe msikilize Roho Mtakatifu, na Roho Mtakatifu atakuambia lakufanya.

Una nguvu zile nilizokuambia hapo mwanzo katika unabii, lakini Ray wewe fanya tu ukiongozwa na Roho Mtakatifu. Kwa sababu huta endakufanya kitu kibaya, au ovu kwa mtu yeyote. Roho Mtakatifu atakuongoza, na kukutangulia katika njia ya haki. Kwa hiyo Ray, kama utakuja kujisikia vibaya kuhusu Mchungaji yeyote au Padri, au Mzee wa Kanisa rudia kusikiliza mkanda huu wa kunasa sauti upaya, uusikilize, na ukumbuke.

Kumbuka nilicho kisema, Mwangalie mchungaji X. Mchungaji X...., Nasikitika kusema, siwezi kuruhusu Kiongozi wa kundi langu akienda kinyume na Mungu, ambaye ni Mimi. Inabidi kukusanya Mwili wa Kristu pamoja. Nisikilize, Ray. Kila kilicho tokea leo siyo kwa ajili yako. Ilikuwa kwenye mipango Yangu, Nilitaka kuona utakwenda kiasi gani, kwa ajili ya Yehova. Najua sasa kuwa nilimchangua mtu wa uhakika, lakini Nilijua tokea zamani ungefanya nini, lakini sasa tazama ulichokijifunza. Nisikilize Ray, kazi, fedha, furaha, mke, kila kitu kitakuja kutokea ila USIWEKE mtu yeyote kabla Yangu".

shetani: [bwana.......] (hakumaanisha Yesu Kristu)

Bwana: "Ray, jaribu roho sasa, Sasa! Jaribu roho, Sasa!"

Ray: "Je, Yesu Kristu wa Nazareti alikuja katika mwili?..... Je, Yesu Kristu wa Nazareti alikuja katika Mwili?.... Je, Yesu Kristu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu juu ya msalaba?..... (Hapa kuwa na jibu. Kwa hiyo mimi nikasema,) Nakufunga, na ninakukemea kwa Jina la Bwana Yesu Kristu wa Nazareti. Nakupeleka popote pale ambako Yesu Kristu wa Nazareti anataka kukupeleka. Nakufunga sasa na ninakukemea katika Jina la Bwana Yesu Kristu ..... Nenda!"

Bwana: "Nimerudi, Ray." Ray: "Nani amerudi?.....

Bwana: "Huyu ni Baba yako Yehova."

Ray: "Je, Yesu Kristo wa Nazareti alikuja katika Mwili?...."

Bwana: "Ndiyo, Ray."

Ray: "Jes, Yesu Kristo wa Nazareti alikufa juu ya Msalaba kwa ajili ya dhambi zetu??.....

Bwana: "Ndiyo,"

Ray: "Je, Yesu Kristu wa Nazareti alifufuka siku ya tatu?...."

Bwana: "Ndiyo."

Ray: "Je, Yesu Kristu wa Nazareti amekaa mkono wa kuume wa Baba?.... Je, Yesu Kristu wa Nazareti anastahili Heshima zote, Sifa, Utukufu, na Mamlaka sasa na milele?...."

Bwana: "Ndiyo, Ray."

Ray: "Je, Yesu Kristu wa Nazareti alikuja katika Mwili?...."

Bwana: "Ndiyo, Ray."

Ray: "Je, Yesu Kristu ni wewe?"

Yesu: "Ndiyo."

Ray: "Je, Yesu Kristu wa Nazareti alikuja katika mwili?..."

Yesu: "Ndiyo."

{Ona Ray, ona ilivyo rahisi kwa adui kuingilia hata wakati tunaongea.} "Zijaribu roho siku zote, zijaribu roho ziku zote, usisahau kamwe Ray, zijaribu roho, mara nyingi kwa jinsi unavyotaka, mara kwa mara kama unavyotaka, katikati ya maongezi simama, na uzijaribu roho. Kuna vita vikali vinavyo endelea sasa Ray. Kuna uchawi unahusika, kuna watu wako wanaokuombea, na adui ana watu wake wanaokuombea, lakini hawakuombei mema yako, lakini Unisikilize Mimi Ray. Wewe uko kwenye Mikono ya Bwana Yesu Kristo, Roho Mtakatifu, na Baba. Hakuna kitakacho kutokea, Ray.

Ray: "Nani anaongea nami sasa?"

Baba: "Huyu ni Baba, Huyu ni Baba. Ray, nilikuchagua kabla huja zaliwa. Nilikuchagua kabla hujazaliwa, ebu endelea tu kufanya hicho unacho kifanya. Bado una kichwa kigumu, lakini nakiona, na ninakuona ukibadilika kidogo kidogo, ebu endelea zaidi, ujipe muda zaidi.

Bwana Yesu Kristu, Roho Mtakatifu, na Yehova Watakubadilisha. Tutakufinyanga upya, tutakuongoza. Kwa hiyo Ray, Ninapokuambia kuwa nakupenda ninamaanisha. Ninapokuambia nakupenda Ninamaanisha. Ninapokuambia nakupenda ninamaanisha.

Kwa hiyo Ray, Najua hujisikii una wasiwasi, au kuweweseka baada ya usiku huu wa leo, baada ya mapambano haya hiyo ni kwa sababu nilikujaza Roho Mtakatifu. Unajisikia mwenye amani, unajisikia mwenye raha, lakini Mchungaji X hajisikii hivyo kabisa.

Kwanini? Kwa sababu alikuwa amekosea. Amekosea, na hali yake itazidi kuwa mbaya, itazidi kuwa mbaya lakini wewe utazidi kujisikia afadhali, lakini zijaribu roho, zijaribu roho. Unaposikia neno ambalo siyo sawa, au silabi isiyo sawa zijaribu, lakini Mimi Nitamfanya Roho Mtakatifu akukumbushe. Anakwenda kukukumbusha, wakati gani wa kuzijaribu roho. Atakupa utambuzi huo, kule kujisikia. Hivyo zijaribu roho wakati unapohisi kuwa siyo siyo sawa, Ray.

Kwani Mimi ni Baba yako, Mimi ni Baba wa wote, na nilikuchagua, Ray, kuchukua Neno Langu, kuwaambia Watoto Wangu ujumbe Wangu. Sintakuambia chochote kisichokuwa kwenye Biblia. Utawafumbulia vitu fulani vipya ambavyo havipo kwenye Biblia, lakini vitatokea, sehemu nyingine iko kwenye Biblia lakini siku sema vyote. Kuna vitu vichache vinatakiwa vikamilishwe. Kwa hiyo kila kitu, kila kitu kiko kwenye Biblia, lakini kuna vitu fulani fulani havikufafanuliwa wazi, lakini vichache sana..

Mimi ni Mungu wako, Mimi ni Yehova. Mimi ninayo mamlaka pamoja na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo Ray, utapata majaribu ya kila aina. Wewe vumilia tu, utakuwa pamoja Nami Mbinguni, lakini kama nilivyosema, utaipata kirahisi.

Wewe utaipata kirahisi ukulinganisha na Mitume wengine. Utaipata kirahisi, utaweza kuponya watu. Utaweza kuponya watu. Utakuwa na maono na unabii, na Ray utaweza kupambanua mabaya na mazuri. Utaweza kutambua wakati Mchungaji akiwa anasema uwongo au kama siyo mwaminifu, na anajaribu kukupotosha, lakini usijali kuhusu mambo kama hayo. Roho Mtakatifu atakuongoza, na kukuambia.

Sintakuacha peke yako. Hata mara mmoja, Ray. Sintakuacha peke yako kamwe, kwani tuna kazi. Vita vimeanza, na Ninakuhutaji uwe mkakamavu katika dunia. Unafanya kazi nzuri. Unafanya kazi nzuri, lakini itakuwa mapambano ya muda mrefu, hii ndiyo maana nitakupa mke, watoto wawili, siku yeyote tangia sasa, Ray. Siku yeyote mambo yatakuendea vizuri. Kwa uhakika kifedha, kiroho na maisha yako ya kimapenzi, wewe na mweziwako mtaanza kuongea hivi karibuni, kidogo kidogo kwa wakati, lakini wewe utaanza, na nilichokuambia hapo mwanzo kitatokea maana Mimi ni Mungu wako, Mungu wako hadanganyi.

Mungu wako ni Haki, na Kweli, na ninawapenda wote. Sintataka kitu kibaya kiwatokee yeyote wenu, lakini Ray ebu kaa kwa kutulia, Ombe/Sali, hubiri, na uniachie nishughulikee ule upande mwingine. Nitaanza kumbadilisha yeye. Nitakubadilisha, lakini itakuwa hivyo kwa sababu Mimi ni Baba yako, na nina agano na wewe, siwaachi Mitume Wangu. Siwaachi Mitume Wangu au Manabii Wangu. Kumbuka hilo, Ray.

Utakapo kumbana na tatizo, fikiri: Je, Kristu angelitatuaje? Je, Yesu Kristu angelitatuaje tatizo hilo?" Na kisha fanya jitahada yote, na uitatue jinsi ambavyo Kristu angeliitatua. Kwa hiyo Ray, hiyo nikama yote ambayo nilitaka kukueleza kwa sasa. Uwe imara. Uwe Mnyenyekevu. Uwe mnyofu. Maskini mchungaji X, lakini mwangalie X, mwangalie yeye, Ray. Kama nilivyo kuambia, usibishane naye. Usimkwepe, ila mwangalie, na utafahamu, kuwa Mimi ni Baba yako wa Mbinguni, Baba wa mababu, Baba wa mababu wa mababu." (Lugha isiyoelewaka?)

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.