36. Unabii aliopewa Raymond Aguilera wiki ya kwanza ya Februari 1991 katika Kiingereza na katika Lugha isiyo eleweka.

Wee Mtu, Wee mtu, Nakupenda. Nakupenda, unafanya nini? Wajua Mtu, Nilikuwa nakufikiria wewe hivi leo. Nilikuwa nakufikiria wewe. Wajua kwa kweli sielewi jinsi ya kukueleza, jinsi ya kukueleza vitu fulani fulani kwako. Kwa sababu nikisema kitu ambacho hakipo kwenye Biblia kinakuchanganya.

Umeifundisha akili yako ifikirie kwa njia mmoja tu. Kila kitu lazima kiende Kibiblia au iwe na kiini kwenye Biblia. Hivyo ndivyo nilivyoiweka, lakini kuna wakati kuna vitu ambavyo havipo kwenye Biblia, lakini vitatokea. Hakuna kwa kweli…. Sielewi jinsi ya kuweka kwenye maneno bila kukuchanganya.

Ebu jaribu kwa sekunde mmoja kufikiri. Mfikiri Baba yako. Huyu ni Baba yako wa Mbinguni Yehova, Yehova, Yahwe, Yahwe pamoja na Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Nilikuwa na kuambia. Nilikuwa na sema nawe. Nimekuwa nikiongea nawe na Nikijaribu kueleza mambo, kinachokuja kutokea, kilichotokea, na nakitakavyotokea. Vitu vingine vitawachanganya, kwa sababu mmekuwa kama mmeachwa peke yenu.

Kwa sababu nilimtuma Roho Mtakatifu. Yuko pale pamoja nanyi sasa hivi kuwaongoza ninyi, kuwa zuia ili msidanganywe, lakini mfuate Biblia. Ile Biblia ina majibu yote. Nadhani kwa wengine wenu inamaswali mengi pia, lakini inabidi muingie ndani mwake Watoto Wangu. Inabidi muingie ndani mwake. Inabidi muingie ndani mwake mtakuja kusikia Manabii wa Uwongo wengi. Watu Wengi watakuja kusema maneno mengi ambayo akili yenu itakuja kuzidiwa, akili ambayo imekwisha zidiwa.

Mtakuja kuchanganyikiwa, lakini ombeni. Mwombeni Yesu. Mwombeni Yehova. Mwombeni Roho Mtakatifu. Mtapata njia yenu, inabidi mvumilie. Jifunzeni Neno. Jifunzeni kwa Moyo ulio wazi. Roho yako itajiunga na Roho Mtakatifu na matokeo yake itakuwa zawadi Mbinguni, zaidi ya uwezo wako wa kudhania, zaidi zaidi ya ubongo wako unavyoweza kuwaza.

Kwani Mbingu ni mahali pa kustaajabia. Kwani mwili wako haukuumbwa kuweza kutafakari ukuu wa Mbinguni. Kwani Watoto Wangu, Mbingu ina kila kitu cha kustaajabia, kizuri, na kinadumu kinadumu milele, kinadumu milele na milele na milele na kuzidi milele. Hata Mbingu pekee haiwaziki. Kwa hiyo iwapo unapata taabu kuelewa Biblia, hutaweza kuelewa au kutafakari Mbingu. Kwani sikingine, ila uzuri mtupu, uzuri, na furaha, na utamkuta Muumba wako pale, Yesu, Roho Mtakatifu, na Yehova na tutaishi pamoja pale kwa milele, na milele, na milele na milele. Je, hicho sicho cha maana.

Kwa hiyo, Watoto Wangu, njia pekee ya kufika huko ni kupitia kwa Yesu Kristu wa Nazareti. Hicho ni cha maana sana! Njia pekee ya kwenda Mbinguni ni kupitia kwa Yesu Kristu wa Nazareti. Nawapenda, kumbuka hicho. Nawapenda ninyi. Mtakwenda kuwekwa kwenye majaribu. Mtakwenda kujaribiwa hadi mwisho wa uwezo wenu. Wengine wenu mtasambaratika. Wengine wenu mtavumilia, lakini kama nilivyo kwisha kusema, nendeni kwenye vyumba vile, fungeni milango, washeni mshumaa na msali. Ule mshumaa utawakumbusha kuwa Niko njiani, lakini lazima mtambue, niko pale pamoja nanyi pia.

Nimesimama karibu kabisa nawe, nikisikiliza sala zeko. Ukinyoosha Mkinyoosha mkono wako unaweza kunigusa. Unaweza kusikia miali ya uwepo Wangu, kupitia kwa Roho Mtakatifu, kupitia kwa Yesu, lakini kumbukeni jaribu lolote litakalowapata Mimi niako hapo. Niko hapo na siku zote nitakuwepo. Kwa hiyo fungueni akili zenu, mioyo yenu, ongeeni Nami. Nawapendeni. Sintawaacha kamwe.

Nyakati zitakuja kuwa ngumu Watoto wangu, kuanzia hali ya hewa, hadi maisha yenu ya kifamilia, majaribu yenu ninyi wenyewe na mateso, lakini nitakuwa pale. Nitakuwa pale, Huyu ni Yehova, Huyu ni Yehova, Huyu ni Yehova lakini Watoto Wangu unganisheni Mwili wa Kristu. Unganisheni Makanisa yote, haijalishi mnajiita nini unganeni. Mjiimarishe, Msali pamoja, imbeni pamoja, mjiunge pamoja kama kitu kimoja.

Hiyo ni muhimu. Jinsi mnavyo kuwa karibu ndivyo mtakavyokuwa na nguvu. KUMBUKENI MANENO YANGU, jinsi mtakavyo karibiana, jinzi hiyo hiyo mtakuwa imara. Inabidi muache kugombana ninyi kwa ninyi. Inabidi mfungue mikono yenu kwa watu wasiojiita Wakristu, lakini wanaimani. Inabidi muwabadilishe. Inabidi muwabadilishe kwa Yesu Kristu.

Kwani wanaweza kuwa na imani, lakini kama hawamwamini Yesu Kristu hawataweza kufika, na kwa wale wanao mwamini Yesu kristu, inabidi muwe wanyenyekevu. Inabidi muwe wapole. Lazima mfanane na Yesu, la sivyo hamtaweza kufika. Inasikika kuwa ngumu kueleweka, lakini kimsingi ni rahisi, fanya kwa wengine kama unavyo taka kufanyiwa wewe. Mpende Baba yako Mwenyezi kwanza ya yote. Mpende jirani yako, vumilia, ungama dhambi zako, na mengine yote yatajirekebisha yenyewe.

Soma Biblia, abuduni pamoja, pendaneni. Siyo ngumu kiasi hicho mnachodhania. Siyo ngumu kiasi mnachodhania. Wakati mwingine akili zenu zina kwama… sijui niwekeje katika maneno, ambayo mtayaelewa kwa sababu ni rahisi sana. Mnakawaida ya kukuza mambo kupita kiwango chake, lakini someni Biblia. Muwe na imani juu ya uweza wa Roho Mtakatifu Kuwa fundisheni ninyi, na kuwaongoza. Yeye hatawapotosha.

Mtawapata Manabii kadha wa uwongo, kumbukeni maneno Yangu haya na muyaweke kwenye kumbukumbu zenu, mtapata pia baadhi ya Wachungaji wabaya sana wanaopenda kujikweza, wenye kupenda sifa na majivuno, lakini kumbukeni pia kuna wengi wao amabao ni wazuri, wengi wengi wa walio wazuri ni Wachungaji wema. Kwa kweli Wanajitahidi sana, ni ngumu, gumu sana.

Kuna manung’uniko mengi Makanisani, ambayo inafanyakazi yao kuwa ngumu sana. Kuna wengi Walio wazuri . Watawaongozeni pia kwa sababu Roho yuko pamoja nao, lakini kinacho ni sumbua niwale wabaya. Mmoja mbaya anaweza kuwaongoza wengi kwenye njia ya upotovu, anaweza kuwachanganya, lakini muda unazidi kuyoyoma unazidi kwisha, kama nilivyo kwisha sema kabla. Shetani kweli ataweka shinikizo juu yenu, lakini kumbukeni nawapenda ninyi. Msisahau hilo. Nawapenda. Mimi ndiyo Mimi Ndimi Yehova, Yahwe, Yahwe (Lugah isiyo eleweka?)

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.