45. Unabii na Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 5 Mai 1992 saa 1:12 asubuhi. Jumane katika lugha katika Kiingereza na Lugha isiyoeleweka.

Maono:

Naona Piramidi. Kisha Bwana akasema:

Kiingereza:

Njoni, njoni, wakati wa dunia umeisha. Kwani mbingu ndiko mahali pa Watoto Wangu, Baba yenu, Mfalme wenu wa Wafalme, Bwana wenu wa Mabwana, Yesu Kristu na Roho Mtakatifu wanawakaribisheni, kwa sababu hakutakuwa na amani duniani. Nami nitawachukua Kondoo Wangu wa Kiume na wa Kike Mbinguni kabla ya ile taabu kuu, kabla ya machinjio, kabla sijamwaga hasira ya Duniani.

Lakini ni wale wema tu, wenye haki wasio na lawama, wasio na doa, wale tu waliotubu. Wale tu wanaonipenda kwa Mioyo yao yote, na siyo kwa midomo yao. Kutoka moyoni ndio tu ninacho kiona, mengine yote hayana maana.

Nimekuwa nikukuambia Ray, mipango itakayokuwa hapo kwa wakati wake hapo baadaye. Nitakuambia nini la kufanya na taarifa niliyokuwa nikikupa , lakini nisikilize Ray, nilichokisema kitakuja kutokea. Utakuja kuteswa kwa ulichosema, lakini usinisahau Mimi. Nitakulinda kutoka kwa Wanatheologia, kutoka kwa Wachungaji, kutoka kwa adui. Niamini Mimi na Mimi pekee, naitakuwa rahisi, lakini inabidi uniamini Mimi.

(Lugha isiyoeleweka?)

Ray, Nakupenda. Amani, utulivu itakuangunkia, uwe tu na uvumilivu. Naangalia kila hatua ya njia yako. Asante Ray. Asante Ray.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.