Sehemu hii ya sauti 46
imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 2:57 au (355 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia sauti ya dakika 8:24. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hili. Unabii huu uko katika lugha ya Kihispania na Lugha ngeni. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti,
na Modemu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player"
ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe
hiki.
46. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 5 Mei 1992 siku ya Jumanne katika lugha ya Kihispaniola, na katika Lugha isiyoeleweka
Kihispania:
Kitu kimoja ni nini...?
Dunia, Dunia ni kama ilivyo.
Masista, Mapadre,
Mapadre ni kama wale wengine wote walivyo,
Wanaoangalia Biblia,
Kwa ajili ya sababu za kidunia.
Inaendeleaje?
Inakujaje?
Itakuwaje?
Hawajui tena zaidi ya wengine.
Kila mmoja anaamini,
Kila mmoja anadhania kuwa wanajua,
Lakini ni vigumu sana kujifunza
Kilicho sahihi,
Na kufanya kilicho cha sahihi.
Watu wa dunia walipoteza mengi,
Wakati walipopoteza dunia kwa maji.
Na watu Wangu walipoteza (lugha isiyoeleweka)
Safina, Safina,
(lugha isiyoeleweka)
Safina, Safina,
(Lugha isiyoeleweka)
Kihispaniola:
Ndiyo, mpira, mpira unakuja. Unakuja kwa kasi sana. Tazama unakuja mpira ambao utakuja kuifunga dunia. Kwanini? Kwanini? Ni siri ambayo sitawaambia kwa njia yoyote ile. Kwa sababu wakati ni mfupi, wakati ni mfupi kwa lolote litakalo tokea. Wakati utakaposikia mlango unagongwa hutaweza kujua ni nani yuko pale. Utatishika sana, kwa sababu, kutakuwa na shetani ambaye atakuwa anawatafuteni ninyi kama vile mbwa anavyotafuta mfupa. Mbwa anakuja sasa, mbwa akiwa amekenyua meno yake na mdomo wake unaonuka kwa ajili ya nyama ya miili yenu.
Hivyo ndivyo itakavyo kuwa, kama hamtaamka. Uso wa mioyo yenu umelala kwa sababu kila unachokifikiria ni mamabo ya dunia, lakini dunia haitakuokoa. Unamhitaji Mungu, Roho Mtakatifu na Yesu. Baba ni kila kitu, na anajua kila kitu.
Mtakuja kukumbuka ninacho wa ambia ninyi. Tazama mpira unakuja mmoja kwa mmoja. Utakuja kuwa dunda vichwani kwa muhuri wa nyota ya shetani. Na hamtaweza kuuondoa muhuri huo wa nyota ya shetani. Shetani atakuja kuwatafuneni ninyi. Ni aibu gani, ni aibu gani, Wanangu wa kiume na wa kike, pamoja na Upendo, pamoja na Upendo, nawaambieni Ukweli. Ni aibu gani, tazama mpira unakuja, pamoja na nyota (lugha isiyoeleweka)? Ya Yesu (lugha isiyoeleweka).
Maono:
Naona taji la dhahabu. Naona na sululu na beleshi ikiwa na kitambaa kilicho na maneno yanayosema: "Umeifanyiakazi, unastahili kuipokea."


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )