Sehemu hii ya sauti 48
imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 3:00 au (362 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia sauti ya dakika 7.35 Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti,
na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player"
ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye kompyuta yako, bonyeza kwenye kitufe
hiki.
48. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 7 Mei 1992, saa 7:22 usiku katika lugha isiyoeleweka, katika Kiingereza na Kihispaniola.
Kihispaniola:
Unanisomaje?
Unanisomaje, Mwanangu?
Unanisomaje?
unanisomaje?
Oo ni aibu gani,
kwa kila kitu kile kilichopo,
kwa kila tu kile kitakachokuwepo,
kwa kila kile ambacho ni lazima kiwepo,
Ni aibu gani.
(lugha isiyo eleweka?)
Kihispania:
Mambo yanaendeleaje?
Kila kitu kitakuja kuwa shwari sana. Kila kitu kitakuja kuwa shwari sana.
kikombe, kikombe, na sahani
ni kitu kimoja. Kahawa na kikombe, mojawapo hakiwezi kuishi peke yake bila
mwenziwe.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Wote ni Wamoja.
Na kila Mmoja wao ni tofauti au amejitenga kutoka wengine wawili.
Siku inakuja ambapo wote Watatu tutakwenda kuunda Dunia
Mpya,
Lakini mawazo Yangu yameungana na wengine Wawili, Mwana na Roho Mtakatifu,
Sisi ni Wamoja,
Lakini sisi sote siyo sawa sawa au hatufanani.
(Lugha isiyoeleweka?)
Kiingereza:
Mimi Sielewi.
Mimi sielewi la kufanya.
Mimi sielewi cha kusema.
Unasema, na unasema,
lakini hakuna hata mmoja anayesikiliza,
ila sehemu ndogo sana ya Mwili wa Kristu.
Kwani wanaonekana kwenda njia zao binafsi,
lakini itakuja kuwa sawa na mipango Yangu mwishoni.
Kwani nilichosema hakiwezi kurudi tupu, bila kutimiza lengo, Hakijawahi kurudi
tupu na wala hakitatokea kurudi tupu.
Kambi imekwisha kuwa tayari.
Wachezaji wote wamezunguka kambi ya kuotea moto, wakingojea zamu zao.
Wakingojea kibendera,
Wakingojea filimbi au parapanda,
Wakingojea tarumbeta ya maisha ipigwe kuashiria mwito wao. Mara mchezo
utakapoanza hautasimama,
hautasimama mpaka mambo yote yaishe.
Kwani ninachosema, kwani nilichokianzisha au kukiweka kwenye mwendo, hakuna atakayeweza kukisimamisha. Kwahiyo ni kweli kuwa Nguvu na Utukufu na Heshima ni mali ya Baba.
Kwani anawapenda, na Anawahitaji, na Ninawataka ninyi, lakini njia ya Baba ni ya haki, na safi, isiyo na doa.
Msikilizeni Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu.
Wamekwisha tayarisha na kuichora njia hiyo kwa ajili yenu. Tubuni, tiini, na
Wapendeni jirani zenu.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )