Sehemu hii ya sauti 49
imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 7:11 au (865 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia sauti ya dakika 17:21. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa chini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.Ili kusikiliza mkanda huu unatakiwa uwe na Kadi ya sauti,
na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player"
ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe
hiki.
49. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 12 Mai 1992, Jumanne saa 3:13 asubuhi katika lugha isiyoeleweka na katika Kiingereza.
Njoni! Njoni! Ninyi watu waaminifu, Mikono Yangu iko wazi kuwapokea. Njoni! Njoni Mbinguni, Tunawangojeeni ninyi, Malaika, Yesu Kristo, Roho Mtakatifu, na Mimi Yehova. Njoni! Mnakaribishwa, Tumekuwa tukiwangojea. Tubuni mjitakase. Mnakaribishwa! Kila mtu anakaribishwa.
Saa iko karibu kuwadia, ni kama imewadia. Siku na saa zimekwisha chaguliwa. Siku ya Mekka, siku ya ukombozi, siku ya Utukufu, siku ambayo Ulimwengu umekuwa ukiisubiri, inakaribia kwa kasi. Waambie marafiki zako, waambie ndugu zako, waambie dada zako, waambie majirani zako. Simama juu ya milima na upige kelele kwa pumzi yako yote uliyonayo, kwa sauti kubwa iwezekanavyo. Kwani itafika kama ilivyowadia katika siku zile za Nuhu. Kama Mwizi usiku, lakini itakuwa ya ajabu sana. Itakuwa ya Utukufu kwa Watakatifu, kwa Watakatifu wa Kristo, kama nilivyo waambia hapo mwanzo. Wachezaji wana nafasi yao, jukwaa liko tayari, saa imekwisha chaguliwa.
Nyota iko njiani. Inakuja kwa kasi ambayo hamwezi kuitafakari, lakini iko njiani. Tazameni mawinguni, tazameni angani, mtafuteni Yesu, mtafuteni Yesu. Siku za shetani zimekwisha kwa sababu siku na saa zimekwisha chaguliwa.
Malaika wa Mbinguni wamekuwa wakiingojea siku hiyo kwa shauku kuu kwa miaka mamia na mamia na maelefu, sare za vita ziko tayari. Wengine tayari wako vitani. Wengine wanapigana sekunde hii ya sasa, ingawa hamuuwaoni. Vita vimekuwa vikiendelea kwa nguvu sana kuanzia DESEMBA 2, DESEMBA 2, 1990. Vita vilianza, lakini mtaelewaje vitu vya namna hiyo.
Mmezoea mambo ya dunia yenu hiyo ndogo, kucheza na vidoli vyenu, michezo yenu midogo, matatizo yenu madogo; mtawezeje kuelewa mambo ya ulimwengu wa roho? Nipana zaidi, ni magumu zaidi; kuweza kuyaelewa kwa akili zenu hizo ndogo kuweza kuyatafakari. Huyu ni Baba yenu. Baba wa Mbingu na Dunia, wa yote yale yaliyoko, na yatakayo kuwako na yaliyokuwako.
Mnisikilize Mimi, Nimekuwa nikiongea nanyi kwa maelfu ya miaka na angalieni saa zenu. Unakuja wakati ambako hakuta kuwa na wakati tena. Wakati wa saa umeisha, na muda huo unakuja kwa kasi. Nikama unatembea haraka gizani, na kuna bonde la ufa kali kwenye jabali mbele yako. Kisha ghafla unaamua kukimbia haraka iwezekanavyo kuelekea kwenye mtelemko huo mkali, bila kufahamu kuwa mtelemko huo uko hapo mbele yako. Nawe unaenda kama kipofu kulikaribia bonde hilo kwa kasi sana, bila kujua kuna nini mbele yako. Hivi ndivyo itakavyo kuwa hapo mwishoni. Ghafla, ambapo hamtaweza kufunga breki ili kusimama msianguke kwenye mtelemko huo mkali wa jabali.
Siku za malumbano kati ya Makanisa na Makanisa, siku za mapambano kati ya kaka na dada zinakaribia ukingoni. Inawezekana kuwa wengi wenu mnadhani kuwa haya ni maneno ya mwenda wazimu. Nabii Wangu huyu atakuja kuteswa, kwa kuleta maneno haya au ujumbe huu, lakini fahamuni yuko kwenye Mikono Yangu. Fahamuni wale watakaoenda kinyume naye kuwa wanaenda kinyume Nami, na hasira Yangu hutaweza kuikwepa. Kwani na walinda Manabii Wangu, Nawalinda Mitume Wangu, na msifanye mzaha na watu niliowachagua. Msidhubutu kutumia Biblia ili kujithibitishia haja zenu. Kwani Mimi ndiye Neno la Kwanza na ni Neno la Mwisho, na hicho pekee ndicho kilichoko. Fikiri! Kabla hujampinga Mtume Wangu, omba na aheri yako uwe sawa na kile unachomfikiria, kwani Hasira Yangu itakuwa juu yako bila Huruma kama kile unacho mdhania siyo sawa.
Kwa sababu muda unakuja ambako hakutakuwa na wakati tena. Navua maglovu yangu ya mikononi na nitakuonyeshea, dunia, Ulimwengu, na nani hasa ni Mungu wa kweli, kwani hakuna, na nina maanisha hakuna kilicho umbwa bila ya Mimi. Kwa hiyo ninyi watu wenye akili duni, na mliofunga mioyo yenu, na wenye mioyo ya mawe mmeonywa. Nimejaribu kuwaambieni, kwa upole, kwa sauti ndogo, kwa kelele, nyakati za amani, nyakati za vita, kwa njia yote unayoweza kuifikiria. Nimejaribu kuwaonyesheni Ukweli; kuwa Waadilifu; Kutubu; kunigusa; kuwa wema ninyi kwa ninyi. Mnafanya nini? Mnawapiga mawe Manabii Wangu, mnawadhihaki, Mnawatesa, mnawaua, na mnanikufuru Mimi. Na mnacheka na kucheza dansi juu ya makaburi yao. Wakati mnapowaumiza mnaniumiza Mimi, na imeendelea muda mrefu vya kutosha.
Kwa hiyo angalieni angani. Mnitafute Mimi, kwani kile nilichoki sema kitatimia. Mimi ni Mwumbaji, Mjenzi, Kinga, Mlinzi wa Ulimwengu. Kupitia kwa Mwanagu, Yesu Kristu ni njia pekee, njia pekee ya Wokovu. Ni Rahisi, imenyooka, ni ya moja kwa moja, na ni ya uhakika. Na hakuna na, wala lakini, au iwapo, au ikiwa, kuhusu njia hiyo. Huyu ni Yehova, Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova. Nataka mkumbuke, Mimi ni Yule Yule leo kama nilivyokuwa jana, Niliwapendeni wakati huo, Nawapendeni, Nawapendeni hata sasa, lakini siku ya Nuhu inakaribia haraka. Amkeni! Sikilizeni! Oneni!
Oneni ishara zote zilizoko kwenye Biblia. Msiwe Wajinga! Msiwe wajinga Watoto Wangu, kwani mwaka na siku ile itawajieni ninyi kwa wakati ambako hamuutarajii kabisa hata kidogo! Kwaherini Watoto Wangu. Tutaonana na ninyi mlio na bahati Mbinguni. Lakini Nitalia na Nitalia kwa ajili ya wale nitakao wapoteza, kwa sababu niliwapenda wao pia. Nikiwa na machozi Machoni Mwangu na Upendo Moyoni Mwangu, niseme nini zaidi. Nifanye nini zaidi. Ila kuwaonyeni ninyi watoto Wangu. Nawapendeni. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova. Baba yenu Mpendwa. Amani na iwe nanyi.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )