Sauti 50

Sehemu hii ya sauti 50 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 5:23 au (650 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia sauti ya dakika 14:49. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa chini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.

Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

50. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 15 Mei 1992 Ijumaa saa 7:20 mchana katika lugha isiyo eleweka, na katika Kiingereza.

Mimi ninasogea. Mimi ninasogea karibu zidi na zaidi. Mimi ninasogea karibu zaidi na zaidi kuelekea nyakati za mwisho Watoto Wangu. Wakati na saa zimekwisha chaguliwa na hakuna katika Ulimwengu kinachoweza kuibadilisha tarehe hiyo. Nyota, Nyota ya Daudi itaonekana wakati wake uliopangwa utakapofika.

Milki ya Mbinguni iko tayari, imeshajivika silaha, inangojea Neno Langu. Kuna msisimko, kuna shangwe, kuna shangwe zaidi ya ufahamu. Kwa sababu Malaika wa Mbinguni wamekuwa wakiingojea wakati huu toka wakati ule wa Uasi Mkuu. Kila kitu lazima kitokee katika utaratibu unaotakiwa, utaratibu uliowekwa,na haitakuja mpaka Maagizo Yangu yamekamilika. Kisha Majeshi ya Mbinguni yatakomesha maasi hayo kwa mara ya mwisho mara mmoja.

Wakati ni huu, wakati ni huu wa Watakatifu Wangu kueleweshwa; Mjihadhari, Muwe imara; Muwe na hekima. Kwa sababu vita Mbinguni vimekwisha anza na vinaendelea kuwa vikali. Desemba 2, 1990 imeweka alama ya mwanzo. Kuanzia siku hiyo na kuendelea imeanza mwanzo wa mwisho. Hakuna ajuaye mwisho ila Mimi, Yehova. Na waambieni hayo kabla kwa sababu nataka mjue kabla hayajaanza.

Unaweza kuzika kichwa chako kwenye mchanga. Unaweza kuyapima na kuyapanga upendavyo, lakini hakuna kitu katika ulimwengu kitakachoweza kuzuia ambacho nimeamua kukifanya. Miaka maelfu na maelfu na maelfu na maelfu ya miaka kabla hujazaliwa, muda ulichaguliwa. Wasikilize Manabii, Wasikilize Watakatifu, kwa kuwa Jina Langu ni Yehova, kwa kuwa Jina Langu ni Yehova, kwa kuwa Jina Langu ni Jehova, na ya kuwa Jina la Mwanagu ni Yesu Kristu wa Nazareti, na ya kuwa Jina la Mwanangu ni Yesu Kristo wa Nazareti, kupitia nguvu na utukufu, ya Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana ambaye atatekeleza nilicho kisema tokea mwanzo.

Ni wale tu wenye busara ndio watakaoweza kuja, bali kwa wengine kwa wengine imekwisha amuliwa, kwani walifanya uamuzi wao wenyewe. Jeshi la mbinguni liko tayari, Jeshi la Duniani linajikusanya. Roho Mtakatifu anautayarisha, anaukusanya mwili wa Kristo, na hakuna lolote katika ulimwengu kitakacho zuia hicho, kwani kama ni kutosha imetosha.

Kwani ama uko pamoja Nami au unapingana Nami. Sitakubali katikati ambako huna upande, au kusema labda. Ama umo au haumo. Ama utaishi Milele mbinguni, au utaishi na Mashetani na Mapepo milele mahala nilipowagawia Wakuu wa Maasi.

Kumbukeni Watoto Wangu, kuwa huu siyo mchezo ambako unachukua na kuchagua kwa wakati wako unaofaa, kwa sababu wakati unaofaa ni juu Yangu. Siku imekwisha pangwa, saa imekwisha chaguliwa. Kumbukeni, ama uko pamoja nami, au unapingana Nami.

Mwanangu, Mwanangu, Yesu wa Kristu wa Nazareti atakuja kuwachukua mabaki, Wachache ambao watakuwa wamebaki, wakati huo wa mwisho. Kwa wakati uliopangwa. Mnaweza kujidanganya kwa yote mnayotaka. Hamwezi kumdanganya Muumbaji, kwani najua mwisho. Najua nani atakuja na nani haji. Huwezi kunidanganya Mimi, Huwezi kamwe, sielewi kwanini unajaribu. Mengi yamesemwa, kwani imefika, kwa lolote litakalokutokea wewe mwenyewe unahusika. Huna wa kumlaumu ila wewe mwenyewe. Huna wakumnyoshea kidole ila wewe mwenyewe. Kwani ishara zilikuwa pale, Biblia ilikuwa pale, Malaika wako walikuwa pale, lakini wewe uligeuza mgongo wako naukajiondokea mwenyewe.

Ila kumbuka, Nilikupenda kutokea mwanzo, na nitakupenda hadi mwisho. Ila Nasikia kilio cha Watakatifu Wangu kutoka kwenye Sayari. Nasikia machozi yao nasikia maumivu yao, huzuni yao, mateso yao, na Masikio Yangu hayatasikia zaidi ya hayo. Kwani nakwenda kukomesha hayo yote. Watakatifu Wangu wameteseka vya kutosha! Huyu ni Yehova, Huyu ni Mungu Wenu, Mungu wa Ulimwengu, wa vyote vilivyokuwemo, vilivyoko na vitakavyo kuwepo. Siku na saa vimefika.

Unabii: 7:51 Mchana kwa Kiingereza.

Saa ya Safina (Lugha isiyoeleweka ?), saa ya Safina Yangu, saa ya Safina Yangu itakamilika wakati mpinga Kristu atakapo kuwa anakaribia Mekka. Saa ya Safina Yangu itatimia wakati Mpinga Kristu atakapo kuwa ana karibia Mekka. Kisha Parapanda, Parapanda ya Mbingu na Dunia Italia.

Sifa zimwendee Bwana Yesu Kristu, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana. Sifa ziwe kwa Yesu Kristu. Kwani Mfalme na Mwokozi atakuja kwa shangwe na ushindi kama Nilivyosema. Tawanya habari; waambie marafiki zako, waambie ndugu zako wa kiume na wa kike, waambie familia yako kuwa saa ya Safina itaonekana, wakati Mpinga Kristu atakapokuwa anakaribia Mekka.
Sifa na utukufu, na Heshima zimwendee Baba. Sifa na Utukufu na Heshima ziwe za Baba. Sifa na utukufu, na Heshima zimwendee Baba. Sifa na Utukufu na Heshima ziwe za Baba. Sifa na utukufu, na Heshima zimwendee Baba. Asante Baba. Asante Baba. Asante Baba. Huyu ni Yesu. Nakushukuru, Baba Yangu wa Mbinguni. Sifa na utukufu, na Heshima zimwendee Baba.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.