52. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 16 Mei 1992 katika Kiingereza.

Nawapenda. Nawapenda. Nakupenda. Amani, Amani iwe nanyi. Amani, Amani iwe nanyi. Kwa maana kila kilichoko Mbinguni kiko chini ya miguu yenu. Kwa maana kila kilichoko Mbinguni kipo chini ya miguu yenu Watoto Wangu. Mnachotakiwa kufanya ni kuomba. Ombeni na mtapewa. Tubuni. Tubuni dhambi zenu. Nawapenda. Nawapenda. Ombeni na mtapewa. Oo watoto Wangu, Watoto Wangu, Wapendwa Wangu, Kondoo Wangu, kwa Damu ya Yesu Kristu wa Nazareti, Mkombozi wenu.

Kwa Damu ya Yesu Kristo. Ninyi ni Mali ya Yesu Kristo. Ni mali ya Yesu Kristo, Mfalme wa Dunia. Yesu Kristo wa Nazareti Mwokozi wenu.

Mwezi, Mwezi utageuka kuwa mwekundu. Mwezi utageuka na kuwa mwekundu, na nyota zitaanguka, kwani ndivyo ilivyo andikwa.

Mawingu, Mawingu iko vitani. Malaika, Malaika wa Yesu Kristu wanapigana, na wanashinda. Oo Nawapenda sana Wanangu. Kwa Damu ya Yesu, mliokolewa.

Mjihadhari. Muwe imara. Mjihadhari na muwe imara. Kwa maana ninyi siyo wa dunia hii. Ninyi siyo wa dunia hii. Saidianeni ninyi kwa ninyi. Roho Mtakatifu atawaongoza, Atawafundisha katika njia ya unyofu, na katika mikono ya Yesu.

Saidianeni ninyi kwa ninyi. Saidianeni ninyi kwa ninyi. Acheni kuwa na vichwa vigumu. Sameheni, sameheni maadui zenu. Wapendeni adui zenu. Wapendeni adui zenu. Pendeni kama watoto wadogo, Nami nitawasikiliza ninyi, na Nitawasikiliza ninyi.

Naona wasiwasi mwingi kwenu. Naona wasiwasi mwingi kati yenu. Lakini vumilieni. Vumilieni kwani mtakuja kupata amani mbinguni, Mbingu ni mahali pazuri, lakini mtakuja kuelewa. Mtakuja kuelewa hivi karibuni, kwa sababu Mbingu iliumbwa kwa ajili ya Watakatifu wa Yesu Kristu.

Kaeni katika hali ya usafi na muwe mmetakata, na muwashirikishe Neno la Yesu Kristu kwa Wasioamini kwani inabidi nao waisikie pia. Nawapendeni ninyi. Nawapendeni ninyi. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ni Yesu Kristo. Huyu ni Yesu Kristo. Saidianeni ninyi kwa ninyi, Saidianeni ninyi kwa ninyi. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.