53. Unabii aliopewa na Raymond Aguilera tarehe 17 Mai 1992, Jumapili saa 7:19 usiku katika lugha, Kiingereza.
Urusi itamla nguruwe. Utawala wa ndani utakula nguruwe. Kwani Nguvu na Utukufu ni Yesu Kristu; Kwani Nguvu na Utukufu ni Yehova; Kwani Nguvu na Utukufu ni Roho Mtakatifu, Utatu Mtakatifu Uliobarikiwa, ni Mungu wa Wote. Nguruwe ataliwa na Warusi. Siku kati ya Nguruwe, Mwanakondoo, na kuja kwa Tambiko itawasha anga.
Kwani Tambiko litakuwa chukizo kwa Baba yenu Mtakatifu, kwa Mfalme wenu wa Wafalme, Bwana wa Mabwana. Kwani Tambiko litakuwa chukizo kuu kwa vitu vyote visafi, vizuri na vya uadilifu vya Mbinguni vya Mbinguni, lakini lazima itokee. Lazima niiruhusu, ili kufunga, kumaliza kile ambacho lazima kiwe, lazima kiwe, kwani mpangilio wa onyesho la vita utakamilika. Na Mwana wa Mfalme wa Amani (Kristo) Malaika wa Mbinguni mwishoni watakuwa mahali nilipopachagua katika saa ile, na mahali nilipopachagua miaka maelfu iliyopita. Kwani kuja kwa mwisho utakuwa sawa sawa na nilivyosema utakuwa. Kila kitu kitafanyika katika njia na mpangilio ambao niliukusudia.
Kasuku na upanga zitakuja kukoma siku ile. Kwani kasuku ni kitu cha chukizo kuu ambalo sitaliruhusu. Jihadharini na kasuku, yule anayerudia na kurudia makufuru. Kasuku atakuwa mwisho wa miisho. Mwangalieni kasuku. Kwa kuwa Nimesema, hakuna budi ila itabidi ifanyike, Kwani Urusi ni nguruwe, kwani Urusi ni nguruwe. Njoni Mbinguni Watakatifu Wangu. Njoni Mbinguni ambako kuna Amani, utulivu Milele. Hivyo ndivyo asemavyo Yehova. Kwani yatakamilika pale Mwanangu atakapokuwa amemchinja joka (zimwi, dragoni), mara moja na mwisho.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )