55. Unabii na Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Mei 1992 katika ndimi, Kiingereza, Kihispani, na lugha isiyoeleweka.

Maono:

Niliona kanda mbili za chumba cha kulala.

 

Kanda mbili, kanda mbili za Mbinguni zinawangojea Watakatifu, kanda mbili. Kwani majumba yao ya anasa yako tayari, yale niliyokuambia hapo awali. Vyumba katika ufalme wa Baba Yangu viko tayari. (Ndimi zisizoeleweka?) kwani (Ndimi zisizoeleweka?) ni (Ndimi -zisizoeleweka?) ni tabia ya dunia. Kula viatu vyako, kula viatu. Ndiyo, kula viatu vyako. Ndiyo, kula viatu vyenu Wanangu.

Kiingereza:

Siku ya nguruwe imewadia, siku ya meno makali yaliyochongoka ya nduli imefika, kwani kucha za nduli zimechongoka sana ili kurarua vipande vipande. Njoni ninyi wanafunzi waaminifu wa Biblia, kwani hekima na maarifa ya nduli/taiga na meno yake zitajidhihirisha zenyewe katika nchi na mali ya watu walio na mikuki na mishale. Lakini ulinzi wa watu, walio na mikuki na mishale watamteka nduli mwenye magego na kucha. Kwani nguruwe atamhadaa nduli. Naye nduli ataanguka bila kupata fursa ya kulipiza kisasi. Hakujua kuwa muda usingefika. Kwa sababu ya kitendo chake cha makusudi ya nduli ya kwenda kwenye eneo ambalo nguruwe na joka hawakukubaliana nayo.

Nawapenda, wenye uso wa chokoleti. Nawapenda.

Maono:

Naona chombo chenye maua.

Unabii:

Chombo chenye maua kitaanguka kwanza, chombo chenye chachu kitashinda juu ya chombo kitakachoingia katikati ya vita. Kilichoko juu kitakuwa chini na kitakachokuwa chini kitakuwa juu. Na mbwa mwitu na mbweha watakimbia kuokoa maisha yao. Kwani wakati wa toba utakuja haraka kwa bundi.

Mkasi ule utakaokata utepe utakata mkono uliofunga utepe. Na utepe ni mwekundu lakini damu ya mkono pamoja na mikasi hautadhuriwa na ukataji huo. Kwani nguvu ya mkono ni kubwa kuliko damu za watu.

Kwani maandamano ya amani ya vita itafika kwenye mlango wa Sheol wakati wa asubuhi ile iliyoelezwa na Nabii Yeremia. Kwani Nabii aliaye ataona matokeo ya maamuzi ya adui. Na uchinjaji wa damu isiyo na hatia bila ya huruma ya upanga, kwani kilicho onekana kitatendeka saa ile, mwezi utakapokuwa juu na kuonekana na vikundi hivyo husika; katika bonde iliyo na mti ule uliotumika kutundika Mwili Bwana Yesu Kristu wa Nazareti.

Kwani Kondoo atawateka Mbuzi, na masaa ya mchana na usiku ule utafunikwa yote kwa damu. Kwani damu ya Abeli itamwagwa hadi mwisho wa nyakati, kwa upanga katika bonde.

Ni kwanini, ni kwanini, ni kwanini kuja kwake nguruwe inavuruga halaiki ya Wakristu. Kwani nyota itatua kwenye bonde, ambako Swala na mbuzi walifanya makubaliano. (Ndimi zisizoeleweka?)

Kihispania:

kwanini?, upendo. (Ndimi zisizoeleweka?)

Kihispania: Upendo. Ah nini zaidi! Nini zaidi!

Kiingereza:

Tazama angani kwani kobe mwekundu anaruka kwa kasi iwezekanavyo kumshinda chui "Jaguar". Kwani Simba mtu "Sphinxes" wa Misri wamejaa damu nyekundu kwa sababu miungu yao ni chukizo kwa Mungu.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.