Sauti 57

Sauti 57 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya kama dakika 13:47 au (1.67 KB) kutoka kwenye habari yenyewe ya dakika 23 ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispania na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa chini wakati unaposikiliza mkanda huu wote ili uweze kupata matokeo mazuri.

Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the Real Audio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
 

 

 

57. Unabii aliopewa Raymond Aguilera wa tarehe 19 Mei 1992 saa 12:30 asubuhi Jumanne, katika lugha ya kihispania, Kiingereza na Lugha isiyoeleweka.

Kiingereza:

Upepo wa Dunia. (Lugha isiyoeleweka)

kihispania:

Hiki ni kitu. Hiki ni Kitu. Lazima mpande Mbegu. Mbegu iliyoadilifu. Lazima mapande Mbegu.

Kiingereza:

Kwa maana hakuna, hakuna kitakachomea mpaka upande mbegu. Kisha inabidi uimwagilie mbegu hiyo kabla haijaweza kusimika mizizi. Tumieni akili zenu Watoto Wangu, akili safi, akili ya Yesu Kristu wa Nazareti na kuotesha mbegu Dunia nzima. Dunia ni bustani yenu. Inabidi kupanda Mbegu kama mnataka kaka zeni, dada zenu, Mama zenu Baba zenu kuja Mbinguni. Wakati Fulani ni ngumu. Wakati Fulani ni rahisi. Wakati Fulani inaumiza, lakini bila mbegu hakuna kitakachoota. Wakati na saa ya Kupanda mbegu katika rika hili lazima uanze leo, na kwa kasi iwezekanavyo.

Kwa maana bado mnakimbia kuelekea mtelemko ule mkali kwa kasi kubwa iwezekanavyo. Iko pale! iko pale! Kila hatua mnayochukua ni siku mmoja karibu zaidi na shimo la Jehanamu. Kama unampenda Kaka yako, na unampenda Dada yako, na kama unampenda Mtoto wako, panda mbegu. Roho Mtakatifu atakusaidia kuimwagilia maji, lakini mtu mmoja lazima apande mbegu. Sayari ya Dunia ni bustani kubwa. Mavuno ni mengi tu kama mtapanda mbegu. Uwe mkulima wa Bustani, uwe mpanda mbegu, na tuzo lako Mbinguni litakuwa kubwa sana, Kwani utavuna ulichopanda.

Wakati wa maneno matupu/domo kaya umepita, wakati wa matendo ni huu. Fanya hivyo! Fanya hivyo kwa ajili ya Kristu. Fanya hivyo kwa ajili ya Roho Mtakatifu. Fanya hivi kwa ajili Yangu Mimi Yehova. Kwa sababu nitaweka kidole changu juu yako, na mtaongezeka zaidi ya mtakavyoweza kuwazia katika ndoto zenu za kufikirika, kwa maana kila anigusaye ataongezeka zaidi ya mtakavyo weza kufikiria. Nitawabadilisha, lakini inabidi mfanye kwa hiari yenu. Sitawalazimisha. Sitafanya lolote ila kwa kuwaongoza. Nataka Mnipende kwa hiari yenu kwa uwezo wenu wote, kwa uwezo wenu wote. Sitarajii mfanye zaidi ya mtakayoweza kufanya, kwa hatua mliyofikia.

Naangalia vitu vidogo. Naona hata vile vitu ambavyo hamvitilii maanani. Mnapo mkumbatia mtoto mdogo, mnapomsaidia mzee, mnapomtunza mgonjwa, au hata wakati mnapomtazama mtu nakutabasamu. Natabasamu yenu inasema kaka, dada ninakupenda, lakini tabasamu yakumaanisha, na wala siyo tabasamu ya kujifanya. Kwa maana naona ndani ya uchafu na kuona kilicho ndani sana, hadi kwenye mizizi ya mioyo yenu, na Nina jua uhakika, uhakika wa tabasamu. Kwa maana kuna mazuri mengi pale, ambayo imejificha chini ya uchafu na mizigo, ambayo adui ameweka juu yenu. Kama mkinigusa hata kwa kidogo tuu nitakuwa pale kuuondoa uchafu huo, Nitakuweka huru.

Hata huna haja ya kusema kuwa unajaribu, kwa sababu tayari najua kilichoko ndani ya Mioyo yenu. Kwa maana moyo wako ndio ninachokiangalia, na nia ya moyo wako. Na uwezo wa Moyo naujua kwa sababu ndiye niliyeuumba. Hakuna chochote kuhusu wewe nisichokijua. Nimekuwa nikijaribu kuwaokoeni ninyi kwa miaka maelfu. Nilimtuma Mwanagu, Nafanya kila kinachowezekana kufanywa. Kwa maana saa na siku ni karibu kama pua yako ilivyo. Nami nitaendelea kuwaelezeni, na kuwaelezeni na kuwaelezeni ninyi, mpaka muugue kwa ajili ya kusikiliza haya.

Kwa maana Upendo Wangu ni Mkuu na mwisho utatokea, kama nilivyo upanga karne nyingi zilizopita. Kwani ninyi hamkukusudiwa kuishi kama mnavyoishi sasa. Mipango Yangu kwa ajili yenu ilikuwa muishi kwa amani, utulivu, upendo, furaha, shangwe katika dunia inayokua katika mambo hayo. Kwa hiyo, sikilizeni, Pandeni Mbegu. Nitawasaidia kuimwagilia maji na tutakuwa na bustani ya ajabu iliyojaa matunda. Tunahitaji matunda.

Nawatumieni Mitume, Manabii, Watu wa Busara, lakini siyo wa busara ya makanisa yenu mliyounda ambayo mnazipongeza theologia zinazowaambia kuwa kila kitu ni shwari. Kila mmoja anaenda kwa njia yake. Hakuna umoja. Kuna Mungu Mmoja tuu, Yehova, Yesu Kristu wa Nazareti, na Roho Mtakatifu. Hiyo labda inawazidi ninyi msio Wakristu na hata wengine wenu ambao ni Wakristu. Tamko hilo pekee, lakini nitawaelezeni hayo Mbinguni. Kwa hiyo mnitafute Mimi, na mtajifunza maana ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hiyo pekee na iwe kivutio, kwani bila Sisi ninyi hamnacho kitu.

Mtafikia wakati ambapo tairi lazima ikutane na barabara. Je mtaendesha kwenye barabara au mtaacha barabara. Nataka ninyi mjaribu kitu fulani kwa ajili Yangu. Nataka mjaribu na mtu unayemfahamu, na kisha mjaribu na mtu usiyemfahamu. Mwangalie machoni, tabasamu kwa uso ule kuanzia sikio hadi sikio na kwa upendo kutoka moyoni mwako, mwambie huyu rafiki, "Nakupenda wewe na Yesu Kristu anakupenda. Amani na iwe pamoja nawe Kaka yangu, Dada yangu." Sema kwa kumaanisha na kutoka ndani yako.

Na baadaye jaribu kwa mtu usiye mfahamu, kisha angalia mambo mazuri yatakayo tokea. Kwanza watakuona kuwa umerukwa na akili lakini wewe endelea kufanya hivyo. Nao wataona kuwa moyo wako unamaanisha, lakini wakati unafanya hivyo usifanye hivyo kwa kujionyesha.

Usiifanye kwa ajili ya sifa. Usifanye hivyo kwa ubinafsi wa kujionyesha kuwa wewe ni mtu fulani wa maana. Kwa sababu inawakatisha tamaa, kwa sababu wao siyo wajinga. Wanaona undani wa mchezo wako japo wewe unadhania kuwa hawaoni, kwa sababu hakuna aliye kipofu ila wewe, lakini maanisha kabisa. Na utaona kuwa umepanda mbegu na mbegu hiyo itaanza kuota na kukua. Ni lazima mjifunze kujinyenyekesha wenyewe. Na simaanisha kwa kujionyesha kwa nje. Ila na maanisha moja kwa moja ndani ya moyo wako.

Nasikitika kusema kuwa wengi wa Viongozi wa Kundi la Kondoo Wangu wameenda kinyume kiasi ambacho kumekuwa na dini/madhehebu mengi tofauti. Kuna machukiano, mashindano, na mapigano. Kijana, ninyi Viongozi wa Kundi, mtaangaliwa kwa ukali zaidi kuliko wengine. Kwa maana wengi wenu mlianza kwa nia njema, na adui akaja na kuwashambulia. Na kisha sifa na kujikweza vikawapoteza; Fedha, Utukufu, ni milki Yangu. Sifa ni mali Yangu. Hamjawahi kufanya kitu! Hamwezi hata kutunza au kutawala mlicho nacho. Na mnakwenda na mnaongea na kondoo Wangu, na mnajiweka kwenye kiti changu cha Enzi. Na hata mnajidanganya wenyewe, mnawawekea mzigo huu juu ya Kondoo Wangu. Ni aibu gani, ni aibu gani.

Najua. Najua unafikiri nini sekunde hii, wakati unasoma habari hii. Na jua wengine wenu mnafikiri nini na mioyo yenu hiyo ya mawe. "Nitakwenda kumkamata yule Mtume. Na kwenda kuwamba ngozi yake kwenye ukuta kwa misumari. Hana haki ya kuniongelea mimi namna hii. Yeye anadhania kuwa nani? Kwa sababu mimi ni mwadilifu. Najua neno, Nina mamia ya wafuasi. Ana haki gani kuniambia jinsi ya kuwahudumia wafuasi wangu?"

Oneni, ninyi Wachungaji. Najua kilichomo kwenye mawazo yenu. Najua kilichopo kwenye mioyo yenu hata kabla hamjasema, kwa midomo yenu. Najua mnaenda kujaribu kumsulubisha Nabii Wangu Najua mtajaribu kumwamba ukutani kwa misumari, lakini itabidi mjaribu kuniwamba Mimi kwanza.

Kama mlivyo mfanyia Mwanangu, Mbingu ipishilie mbali kama mtadhubuti, kwa maana Nabii huyu ni Wimp??, amejificha nyuma yangu sasa hivi. Anaogopa kufungua mdomo wake, lakini anafanya hivi kwa upendo wake Kwangu. Na unafikiri unavita mikononi mwako. Wewe jaribu kucheza naye Nami nitakuangukia kwa nguvu kiasi kuwa utaomba usingelikuwa unaishi. Kwa maana nimemweka chini ya ulinzi wa Mbinguni na Malaika Zangu. Sitawaachia Manabii Wangu, Mitume Wangu wanyanyaswe!

Kwa maana wakati na saa imekaribia kutimia, ya ukomo wa Siku za Sifa na Ubinafsi ya wengi wenu ninyi Viongozi wa Wakristu. Najua sasa hivi inauma kusikia mambo kama hayo, kwa sababu wengi wenu mmejikweza juu sana na kujilimbikizia madaraka makuu. Mnadhani kuwa ninyi ni miungu, lakini wakati wa ubinafsi umeisha. Na Siku ya Kristu, Siku ya Roho Mtakatifu, siku ya Yesu Kristo imefika. Siku ya Nuhu, Siku ya Safina, ni wale tuu watakaopanda kwenye Safina, ndio watakao okoka. Kumbukeni hayo! Mnajidai kufahamu kila kitu kuhusu Biblia. Kumbukeni Safina! Kumbukeni Safina!

Nasema mambo haya kwa upendo. Lakini najua hamtapokea maneno haya kwa upendo kwa sababu hampendi kukaripiwa, lakini huyu ni Baba yenu Yehova. Nami ninaweza kumkaripia kila mmoja ninayempenda, kwa wakati wowote ninao penda, kwa maana nilikuumba wewe. Kwa hiyo kumbuka hivyo, na aheri uombe.

Niombe Mimi kwa sababu Mimi ni Mungu wa Upendo na Msamaha. Lakini usishindane Nami kwa Utukufu, Heshima na Sifa. Kwa maana ulikuja kama vumbi na mavumbini utarudi. Kwa hiyo nakupenda bila kujali unacho kifanya. Nitakupenda mpaka sekunde ya mwisho lakini sheria ya Mwanangu lazima itekelezwe.

Haya yalikwisha pangwa kwa maelfu ya miaka iliyopita. Kama Jogoo awikavyo asubuhi kuanza siku mpya, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwishoni. Kwa ajili ya dunia mpya, Mbingu Mpya, lakini usisahau, Mimi nawapendeni, hata kama nawakaripia. Kwa sababu ninyi watu mnageuka kuwa wanyama pori, na yeyote anayegeuka kuwa mnyama pori bila nidhamu ataangukia kwenye shimo la Jehanamu.

Kwa hiyo nitawaoneni, Siku ile ya Hukumu, pamoja na Mwanangu, na Roho Mtakatifu na kisha tutaongea Mimi na wewe moja kwa moja. Kisha mtaelewa ni nini ninachoongea. Kisha nitayashughulikia mambo yale ambayo hayajashughulikiwa na yamekuwa hivyo kwa muda mrefu. Pamoja na Upendo kutoka Moyoni Mwangu, Amani na iwe nanyi Watoto Wangu. Kwa maana Nawapenda kila Mmoja wenu. Huyu ni Yehova, pamoja na Mwangu, na Roho mtakatifu akiwapeni ujumbe wa Upendo. Kwa maana siku na saa imekwisha wadia. Kumbukeni Safina! Kumbukeni Safina!

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.