58. Unabii na Maono aliyopewa tarehe 24 Mei 1992 sa 6:23 usiku. Jumapili, katika lugha na Kihispania.

Una hali gani? Inaonekana unafanyakazi kwa bidii sana, Nimekuchunguza. Nimekuona. Ninayo macho. Na kwa macho Yangu, naona kila kitu. Ndiyo, hakuna kinachotokea bila Mimi kukiona. Huwezi kuficha chochote kutoka kwangu. Mimi ni Baba wa Dunia, wa Mbingu, wa kila kilichoko na kitakacho kuwapo.

Vitu ninavyo kuambia ni vitu vya Moyoni, kwa sababu Mimi naona Moyo siyo kama ninyi mfanyavyo, kama mfanyavyo, na kama msivyo fanya. Moyo tu, hicho pekee ndicho cha maana. Siku inakuja ambayo Mwanangu Yesu ataangalia Moyo wako, na kama siyo safi, mambo yatakuendea vibaya sana.

Nataka wewe ukumbuke kuwa nilikuambia, Baba yako wa mbinguni, Mungu, Mungu, Mungu. Itakuwa siku ya kuzaliwa kwa Watoto Wangu. Siku ya kuzaliwa kwa watu wa duniani, imekaribia sana, siku ya kuzaliwa. Nakwenda kuwatakia furaha, furaha nyingi. Kwa sababu Watu wote wa dunia, wamefika mahali ambapo kila mmoja Mbinguni amekuwa akiingojea. Inabidi usafishe moyo wako, kama unataka kuishi Nami.

Inakuja siku, ambako anga yote itajazwa mioto. Siku ya mioto, hakuna mtu atakaye ishi bila kuona mioto angani. Kwa sababu Mimi nakwenda kusimamisha kila kitu kilichokuwa kibaya duniani kote. Sitaki mseme kuwa siku waambia, kuwa hakuna aliye sema hayo au yale. Kwa sababu sasa hivi, Baba anawaambia kwa midomo misafi, kuwa siku ya mioto, ya angani, inakuja.

Kuna wengi wasiopenda kusikia haya. Sasa hivi, wana weka mikono yao masikioni mwao. Hawataki kusikia zaidi Hawataki kusoma zaidi. Hawataki kuona zaidi. Wale wenye mikono yao masikioni, hakuna atakaye wasaidia, kwa sababu nimesha watayarishia mahala pao.

Lakini watu walio na akili ya kusikia Neno la Mungu, Baba wa yote. Mnisikilize! Safisheni Mioyo yenu na mtafute Mwanangu Yesu Kristo, Mfalme wenu wa kila kitu, ndiyo, hamtasema weza kusema kuwa sikuwaambia, kwa sababu dakika hii ya sasa Maneno Yangu yatagonga Mioyo yenu. Mtakuja kujua kuwa niliwaambia na hamwezi kujificha kutoka Kwangu. Mtaenda wapi, wapi mtaweka miili yenu mahali ambapo Mimi sijui? Hiyo inaenda pia sawa sawa na akili zenu.

Hayo ni yote niliyotaka kuwa eleza, kwa maana Mimi sitakwenda kuwakimbilia ninyi. Bali nataka ninyi mje wenyewe mnikimbilie Mimi, Hicho ndicho kilicho cha sawa, huo ndio utaratibu ulio sawa. Je, Mmenisikia, au bado mikono yenu iko masikioni? Mnisikie, Watu wa Dunia, kwa sababu, anga itakuwa na mioto ambayo mtataka kuchificha kutokanayo. Lakini hamtaweza, kwa sababu najua mlipo. Sikukuu njema ya kuzaliwa. Sikukuu njema ya kuzaliwa kwa dunia nzima. Sikukuu njema ya kuzaliwa. Huyu ni Baba yenu. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.