Sehemu hii ya sauti 64 ni ya dakika kama 7 (1.7 MB) imehaririwa (kufupishwa) kutoka kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.
Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4
au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia
mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
64. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 26 Mei 1992 saa 2:46 asubuhi siku ya Jumanne, katika lugha ya Kiiingereza, na Lugha isiyoeleweka.
Mbweha anaanza kutoka kwenye shimo lake, anaanza kupata ushupavu wa kuweka mipango yake katika utekelezaji. Mbweha mwanzoni atazunguka zunguka jagwani na porini kwa uangalifu mkubwa. Lakini baadaye atapata ujasiri anaohitaji wa kuweka taasisi au utaratibu wake madarakani. Kwa maana Mbweha ni mmoja wa wachezaji katika mambo ya nyakati za mwisho.
Mbweha atamsaidia Mnyama mwanzoni, kisha Mnyama atamwangamiza Mbweha. Mbweha atajilimbikizia utajiri na maarifa ambayo yatatumika kuwavuta kwa hila Watawala wa nchi fulani fulani. Na Mnyama atatumia taarifa hiyo kwa hila na kugawa, kuangamiza Watawala wa Nchi hizo.
Taarifa hizo zitakuwa zana za muhimu kwa Mnyama. Lakini utakapofika wakati na saa ambayo Mbweha atakapokuwa hahitajiki ataangamizwa. Atachinjwa. Atashutumiwa hadharani. Atakuwa moja ya jiwe la kukanyagia Mnyama huyo. Kwa hiyo jihadharini na Mnyama na jihadharini pia na mawe ya kukanyagia. (lugha isiyoeleweka?)
Nawapenda Watu wangu. Natumaini, kwa kweli natumaini mtalainisha mioyo yenu hiyo migumu. Fungueni masikio yenu hayo, macho yenu, mtendee mwenzako kama wewe unavyotaka kutendewa naye. Kwa maana Mnyama atajaribu kuwachinja Kondoo Wangu, atafanya kila kilicho kwenye uwezo wake kujaribu kutekeleza lengo lake hilo. Na atawadharau na kuwadhalilisha hadi kwenye mzizi wa moyo wake, Kondoo Wangu wa kike na wa kiume, Kundi Langu.
Kwa hiyo fungueni mioyo yenu, masikio yenu, Mnisikilize Mimi. Huyu ni Baba yako wa Mbinguni,. Nawapenda na Ninawaonya kabla hayajatokea. Kwa hiyo leteni Kondoo Wangu pamoja na Mwili wa Kristu. Acheni kubishana ninyi kwa ninyi, acheni kupigana ninyi kwa ninyi. Mnajishughulisha mno kupigana ninyi kwa ninyi kiasi ambacho mtaishia kuumizana wenyewe kwa wenyewe kuliko mngeanzisha umoja imara chini ya Yesu Kristu wa Nazareti, Mwanangu. Kwa maana mtalindwa, mtapendwa, na mtahifadhiwa na kutunzwa chini ya mwavuli wa Baba Mbinguni. Tafadhalini Watoto Wangu Mnisikilize. Yasikilizeni Maneno ya kweli, maneno ya haki, maneno ya upendo. Kwa maana inaniumiza kuona Mwili (wa Mwanangu) ukiwa katika hali ya machafuko/vurumai.
Acheni kujifikiria ninyi wenyewe ninyi Wachungaji. Acheni kufikiria itikadi zenu, theologia zenu. Wafikirieni Kondoo Wangu kwa ajili Yangu Mimi Yehova, Mungu wenu. Kwa maana adhabu ya uchungaji mbaya ni kali mno. Tafadhalini, Mimi sipendi kutekeleza hukumu hiyo ya sheria Yangu juu yenu, lakini kama hamtafikiria kondoo wenu kwanza, hasira Yangu itawaangukia ninyi bila ya huruma, kwa maana kondoo Wangu wa kiume na wa kike wananililia.
Kilio cha Maombi yao kinachacharisha masikio Yangu masaa 24 kila siku. Na nimechoka kutazama Viongozi wa Kanisa Langu wakiwa wamewapuuzia kabisa Kondoo Wangu; wale ambao hawana mtu; wapweke; waliovunjika moyo; wenye njaa; wagonjwa. Walioko mitaani na ambao hawana mahali pa kupatia msaada; wale ambao nimewaongelea lakini hakuna mtu wa Kunisikiliza. Macho Yangu yanatokwa na machozi kwa maana inanibidi nikafunge yale ambayo niliyoanzisha hapo mwanzo.
Shetani atawekwa kwenye bonde la kifo cha milele, nasikitika kusema kuwa na pamoja na Viongozi wengine wa Mwili Wangu. Nawaonya kwa upendo mdomoni Mwangu, tubuni, watafuteni kondoo Wangu wa kike, watunzeni kondoo Wangu kiume, kwa maana Maneno haya siyo ya mungu kinyango, haya ni maneno ya Hukumu, kwa maana hukumu itawaangukia bila huruma.
Nawapenda kondoo Wangu. Nawapenda kondoo Wangu. Huyu ni Baba yenu wa Mbinguni, Yehova. Muumba wa Mbingu na Dunia, wa kila kitu kilichopo, na kitakacho kuwepo. Mimi leo ni yule yule wa leo na jana na Mwanangu Yesu Kristu wa Nazareti na Roho Mtakatifu; Tuko tayari kufunga kurasa kubwa sana za Sayari yenu hii ndogo. Amani na huruma na upendo natoa kwa Kondoo Wangu, wale ambao wako peke yao hawana msaada. Sijawasahau.Tafadhalini kamwe msisahau kuwa Mimi sisahau kitu, kwa maana Mimi ni Mungu na Ninawapenda.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )