Sauti 65

Sehemu hii ya sauti 65 imehaririwa (kufupishwa) na kuwa ya dakika 6:39(800 KB) kutoka dakika 20 ya kwenye habari yenyewe ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.

Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.
  

 

65. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 27 Mei siku ya Jumatano 1992 saa 7:19 usiku katika lugha, Kiingereza.

Nataka kukuambia kuwa unatekeleza na unafanya mapenzi ya Yehova. Shukrani zangu nyingi sana kwa maana utashi wa Binadamu wakati fulani ni mgumu kuuelewa. Kwa maana Binadamu ana asili ya uovu tokea wakati ule Adamu alipoanguka. Najua jinsi ilivyokuwa ngumu kuandika Unabii, Maono haya. Najua matokeo utakayoleta kwa watu ambao watausoma na utaona kitakachowekwa kwenye mioyo ya watu kwa kupitia kwenye Unabii huu. Kwa maana Mapenzi ya Mungu yatatendeka, kwani hakuna kitu katika Ulimwengu kitakachomzuia Yehova, Yesu Kristu na Roho Mtakatifu.

Najua wengine wenu nyie watu mmelitafakari wazo la Mungu mawazoni mwenu wengine wenu kila siku, wengine kila mwezi, wengine wakati mambo yanapoenda vibaya, wengine wakati inapowapendeza, wakati inapokuwa mzuri kwao kuzungumzia kuhusu mambo ya Mungu na ya maisha kama gumzo tu la kijifurahisha. Kwa maana sasa nasema na ninyi watu ambao mna mtazamo wa kutokujali kuhusu Mungu. Na nina maanisha Yehova, Muumba Mbingu na Dunia.

Kwa maana naongea nanyi kupitia kwa Nabii Wangu. Huenda hivi sasa mnawaza na kuwasema kuwa huyu mpumbavu ni nani, ambaye ajidai kuongea badala ya Mungu. Sawa anayecheka mwisho hucheka vizuri zaidi. Kuna mahali nilipopatayarisha kwa ajili ya watu walio na mtazamo wa aina hiyo. Siyo mahali pakucheka, siyo mahali pa kutafakari kuhusu nini kitakuwa na nini hakitakuwa kwa maana uamuzi huo hautakuwa wako mara utakapo ingia mahali hapa.

Hivyo fikiri kwa makini sana kabla hujafunga Moyo wako na akili yako na nafsi yako. Fikiria hayo kabla hujaokota jiwe lile, kwa maana unaweza kulitupa. Ebu kumbuka unamtupia nani kwa maana ninyi mnafikiria, mnawaza, mnatenda Kidunia tu. Sisi tuko hapa katika ulimwengu wa Kiroho tukiwaangalieni ninyi hapo chini.

Tunawapendeni ninyi, Tunataka ninyi mje kuishi Nasi, lakini kuna kiumbe kingine karibu nanyi ambacho hakioni. Jina lake ni Shetani, na anataka aishi nanyi. Mnauchaguzi. Siku zote mmekuwa na uchaguzi. Hata hivyo inakuja siku ambayo hamtakuwa na uchaguzi. Na siku hiyo ni siku ya Hukumu, na siku ya Hukumu itatimizwa kwa namna ile iliyoelezwa kwenye Biblia.

Kile ndicho kile kitabu ambacho hamkisomi hata mara moja, ambacho kinakaa katika shelfu, ambacho kinaonekana kizuri watu wakione wakati wanapokuja kukutembelea. Ni kile kitabu unachokiona wakati wa mazishi, wakati mwingine wakati wa harusi, na wakati mwingine wakati maalum ambao hutokea mara kadhaa kwa mwaka, ambao mnauita Sikukuu. Na na kisha kitabu hicho kinarudishwa kwenye shelfu mpaka wakati mwingine. Laiti mngelijua thamani ya kitabu hicho.

Kitabu hicho kinachokaa kwenye shelfu ile, kinachoitwa Biblia kina majibu ya maisha ya Milele, lakini Lakini Najua kuwa ninyi ni wajanja sana kiasi ambacho mnaona hakuna haja ya kukifungua na kukisoma kitabu hicho. Mna kazi za kufanya, mna mahala pa kwenda. Kesho, kesho mnasema nitakisoma, lakini fahamuni kesho Mimi nitakuwa hapo na hutakisoma. Mtakuwa pale mahala pa hukumu hata hivyo. Na kisha Mwanangu, Mwanangu Yesu Kristo wa Nazareti atajua kwa hakika ni nini akufanyie wewe na marafiki zako, ambao mnazo shughuli nyingi sana kiasi kuwa hamna muda wa kufungua Kitabu kile, na kusoma kuhusu Baba yenu wa Mbinguni.

Najua ujumbe huu unasikika kuwa na ukali, wengine wenu wanadhani kuwa ni ujumbe ovyo. Wakati fulani inabidi niwe mkali, kwa sababu nawapenda. Ningelipenda mambo yangelikuwa kinyume chake, ambapo ningelikuwa nawapenda na kuwapenda.

Siku hiyo inakuja hivi karibuni, lakini kumbukeni haijalishi mmefanya nini, haijalishi unakwenda mahali gani siku za karibuni unaweza kunigeukia wakati wowote. Yehova ni Mungu wa Upendo na Mungu wa Msamaha. Hakuna lolote katika Ulimwengu ambalo siwezi kulisamehe. Isipokuwa usimkufuru Roho Wangu Mtakatifu. Ukifanya hivyo hutasamehewa, kwa maana Roho Mtakatifu yuko hapo sasa hivi. Ndani ya chumba chako, ndani ya Nyumba yako, akingojea akisikiliza useme Yesu, Yehova nawapenda. Kwa maana atakusaidia, wakati wowote, usiku au mchana. Jaribu, unaweza kuipenda. Kutosheka kunahakikishwa.

Niambie unachomaanisha, unachosema kwa maana najua kilichoko Moyoni mwako. Najua inapokuwa maneno matupu, kwa sababu nasoma moyo. Siangalii mwili wako. Nakupenda, naweza kusikika kuwa mkali, lakini kuna upendo mwingi ndani Mwangu. Unitafute uniguse, Nami nitakugusa, na tutaishi mahala hapa pa ajabu paitwapo Mbinguni, niliyopotengeneza maalum kwa ajili ya wale wanitafutao na kunigusa. Nawapenda ninyi Watoto Wangu, muwe wema ninyi kwa ninyi. Kwa maana siku na saa ya mwisho imewadia, kumbukeni hicho. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.