81. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 8 Juni 1992 saa 8:45 usiku Jumatatu katika lugha ya ya Kihispaniola.

Ndiyo Mwanangu, kimeanza, nilichokuambia wewe, je, unakumbuka? Kuhusu Nabii mbili, ambazo hivi sasa zimeanza kutimia. Bado nina mengi ya kukuambia, ila uwe na subira, usijali, kwa sababu Mimi niko pamoja nawe hapo. Uko kwenye mikono Yangu ila niombe, omba na Mimi nitaongea nawe. Nitakuambia nini ufanye na lini ufanye. Kwa maana kutakuwa na Watu watakao kukimbiza wewe kwa meno yaliyo kenyuliwa na watataka kukurarua na kukutafuna.

Ukweli utawatwanga kwa nguvu sana kiasi cha kijisikia vibaya, lakini nataka ukumbuke kuwa Mimi ndiye Mungu wa yote, wa dunia yote, wa Mbingu yote, wa kila kilicho Changu. Ninaweza kufanya lolote kwa kila kilicho changu, na wewe ni Wangu na hakuna atakayeweza kukuumiza. Hakuna mtu atakayeweza kukufanyia lolote kwa sababu kama watakufanyia lolote, Mimi Mungu wa kila kitu, wa dunia nitasahihisha.

Uwe na subira kwa sababu tuko karibu sana na wakati wa Mwanangu. Ninakutazama na kukulinda, kila dakika ya kila siku. Najua una machozi, na kuwa haya yanakuumiza moyo; kuhusu yale ambayo itabidi uyafanye, kwa sababu unajua kuwaitabidi nikutume. Ujipe moyo uwe imara, Mimi niko pamoja nawe, kwa maana muda tayari uko hapa.

Naupenda moyo wako, wewe ni msafi Reymundo, na hicho tu ndicho ninacho kiangalia, vitu ambavyo ni visafi. Najua Moyo wako, lakini tazama mwanangu nakwenda kukupa zawadi fulani fulani na kwa zawadi hizo unaweza kuzitumia ili ujitetee. Najua huna nguvu. Omba kwa moyo wako wote, kwa akili zako na kwa kila kitu ulicho nacho. Usijali kuhusu utakachosema. Siyo maneno yako; ni maneno Yangu. Kama huwezi kusema kitu chochote usiseme, kwa sababu Mimi natatumia midomo yako.

Najua utatishika yatakapo tokea, lakini inabidi uniamini Mimi. Unajua na Mimi najua kuwa nimekuwa nikikufundisha wewe kwa miaka kiasi hadi hivi sasa. Najua umeumia sana. Najua umepoteza marafiki wengi hivi sasa. Najua walitaka kukutafuna wewe, kwenye kanisa lile ulilokuwa ukienda kuomba hapo awali. Inakubidi uwe ujiimarishe na uwe imara, kwa sababu siku imefika ambako nitataka utembee juu ya maji. Mkono Wangu utakuwa pale kukusaidia. Najua unaimani ya kuweza kutembea juu ya maji, lakini Mwanangu Yesu yuko pale pembeni mwako na mkono Wake.

Omba tu pale unapotaka msaada, kwa sababu yatakuja, mawe, lakini usijali kwa sababu mawe hayatakutwanga, kwa sababu Niko pale na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Usilie, uwe imara. Kila nilichokuwa nikikuambia kuhusu watu wale wote kitatokea kwa sababu Mungu wako hasemi uwongo. Najua ni vigumu sana kuniamini Mimi, lakini najua moyo wako. Inakubidi unitafute kila siku na Mimi nitakuonyeshea nini cha kufanya. Kila hatua siyo hatua yako, ni hatua Yangu. Je umenisikia Mimi! Reymundo? Hatua ni zangu, na siyo zako.

Nitakutumia watu wa kukusaidia kwa fedha, kwa subira kwa kila kitu unacho kihitaji, kwa sababu najua unacho hitaji. Nasikia maombi yako kwa sababu hujui siku hadi siku ni nini utakachokula, au nini utakachofanya na ambacho hutafanya. Kwa hiyo usijali kwani utatembea juu ya maji. Hutakuwa peke yako. Utadhani uko peke yako lakini hutakuwa peke yako.

Unisikilize Mimi kwa masikio yako, kwa moyo wako. Nakwenda kukuonyeshea dunia na yale yote ambayo utayafanya kwa ajili Yangu; Mungu wako wa kila kitu. Kuna mambo mengi ambayo nataka wewe unifanyie. Hapa tumeanza tu, chukulia katika mawazo yako kuwa ni kama hatua tu ya Mwanzo. Nataka siku hadi siku uweke macho yako kwa Mwanangu, Yesu Kristu, na Roho Mtakatifu na kwangu Mimi. Siyo kwa yale watu wanayokuambia, ila Kwangu Mimi tu, Mungu wako wa Dunia yote, wa Mbingu, wa yote yaliyoko, na yatakayo kuwapo. Mimi ni Neno la kwanza na ni Neno la Mwisho.

Nataka ukumbuke kuwa; watakujakukuambia wewe kuwa ni mwenda wazimu. Watakwenda kukuambia kuwa wewe hujui sheria. Watakuambia kuwa inakubidi kufanyakazi chini ya Mchungaji, lakini Mchungaji wako ni Mungu wako, Yesu, Roho Mtakatifu, na Baba yako. Kama utaelekeza mawazo na akili yako kwa yale wasemayo Wachungaji na kwa wale wanaojifunza na kukariri Biblia Shetani atakutafuna; kumbuka hilo, Reymundo. Ebu lenga mawazo yako na roho yako kwa Mungu wako na Mimi nataka ukumbuke hilo. Kamwe sitataka usahau hilo!

Mungu wako wa Mbinguni alifanya kila kitu, lakini tayari nafahamu nini utakacho kwenda kufanya; hata kabla hujafanya. Usijali kwa sababu kamwe kamwe huta mkimbilia mwingine ila Mimi tu. Kwa sababu niliyaweka hayo akilini mwako, moyoni mwako, kabla hujazaliwa, na kamwe hutaniacha Mimi. Uko imara katika hilo, niliiweka moyoni mwako. Kumbuka hilo Reymundo, hilo ninalo kuambia. Upendo wa Baba yako wa Mbinguni, nilikupa wewe. Nilikupa wewe, Mimi Baba yako wa kila kitu, wa Dunia, wa Mbinguni, pamoja na upendo Wangu na upendo Wangu. Najua unanipenda Mimi kwa moyo wako wote, lakini Mimi nakupenda kuliko unavyonipenda Mimi.

Ebu nyanyuka Reymundo, nyanyuka na uanze kazi. Andika Neno Langu kama nilivyokuambia. Nitakusaidia. Usijali kuhusu fedha, chakula, marafiki wa kike, ila weka tu fikra zako na mawazo yako kwa Mungu wako, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Kisha kila kitu kitaenda sawa. Niamini Mimi kwa machozi yako, kwa roho yako, kwa moyo wako, kwa akili yako, kwa sababu ikiwa watakukimbiza watanikuta Mimi! Kumbuka hilo! Huyu ni Mungu wako na Upendo wa mbinguni.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.