82. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 8 Juni 1992 saa 1:34 mchana, Jumatatu katika lugha ya Kiingereza.
Nakupenda. Nakupenda Ray. Ebu jaribu kuvumilia kwa kitambo kidogo zaidi, kwa sababu kuna mambo fulani lazima niyaseme. Nakili Maneno Yangu kwa usahihi kadri utakavyosikia kwa kadri ya uwezo wako wote. Najua kuwa ni vigumu kwako, lakini kumbuka Mungu wako yuko upande wako, na kwa hivyo hutaandika chochote ambacho ni chako. Kwa hiyo ebu jiachie. Ebu jiachie na wala usiwe na wasiwasi na fanya kazi yako. Kwa maana nawapa thawabu Watakatifu wangu wanaolitii Neno langu.
Kwa maana tangu wakati ulipoanza; wale Watakatifu walio lipokea Neno langu, wamekuwa wakipata matatizo kulitekeleza. Kwa maana Dunia haiwezi kuyaelewa na kuyatafakari mawazo na njia za Mungu Yehova. Kamwe hawajawahi kuelewa na wala hawatakaa waelewe. Kwa maana wanaishi katika dhambi na dhambi haiwezi kuelewa kilicho cha haki, kilicho chema. Kwa hiyo Mimi nitakuvumilia kama wewe unavyo ni vumilia.
Najua uliudhika nilipokuweka kwenye ile sherehe ya kuzaliwa ya siku ya Jumapili, lakini Ray inakubidi uwe mtiifu. Najua ulikuwa unajisikia vibaya. Najua walikutenga, lakini sikiliza Ray, dunia hii, Sayari yenu hii muda wa uwepo wake umekaribia kwisha. Manabii wa kale walipitia kwenye mambo mabaya zaidi kuliko haya unayoyapitia. Kwa hiyo kumbuka kila apelekaye ujumbe kutoka Kwangu lazima atateswa, lakini Mimi niko pamoja nawe, kumbuka hilo. Kubali kazi na madaraka ya ofisi yako, kwa maana nadhani unafanya kazi nzuri.
Najua bado una wasiwasi, lakini hapo ndipo mahala unapohitaji kuwa na imani Ray. Inabidi uwe na imani. Inabidi uniamini Mimi, lakini mimi nitakupa zawadi ya Karama fulani fulani ambazo unaweza kuzitumia kujilinda mwenyewe utakapo shambuliwa na Wanatheolojia fulani, Wakristu fulani, Wanaharakati fulani wa nyakati mpya (New Agers), Wachawi fulani, Mapepo fulani. Najua umekuwa ukipambana na nguvu za mapepo mara kwa mara kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. Najua ulichanganyikiwa kabisa hapo mwanzoni, lakini sasa unavaa silaha zako vizuri, Ray. Hawakuchezeichezei tena kama walivyokuwa wakifanya hapo mwanzoni, kwa sababu nimekuwekea ulinzi imara. Bado naelewa unavyojisikia. Kwani wakati wakikupata na mishale yao ile na wakikupata ukiwa umevua silaha zako zile. Ila unafanya vizuri, unafanya vyema
Nilikuahidi vitu fulani fulani na nitakupatia. Saa na siku yakukupatia vitu vile imekwisha kuwekwa. Uwe na subira Ray, kwa maana saa na siku ziko mbele ya pua yako. Nitakupa maagizo ya jinsi ya kutoa Unabii huu, na namna na jinsi ya kupokea Unabii huu. Ila kwa wakati huu nataka tuu uandike Unabii huu. Ebu usiwe na wasiwasi mwingi namna hiyo, kwa maana hakuna chochote wala lolote Ulimwenguni, Mbinguni, kwenye Manyota kitakachoweza kuingilia na kuvuruga kazi Yetu.
Kwa maana Neno Langu nililolinena hakuna kitakachoweza kulivunja, lakini saa imefika ile iliyoandikwa katika Biblia kwa miaka maelfu iliyopita, kwani kuja kwa Kristu katika Mawingu kumewadia. Sitakuambia lini. Ebu wewe andika tuu yale nikuambia, wakati nikuambiao, na uniombe Mimi, Ray. Uniombe Mimi kwa sababu najua unataka unifahamu vyema zaidi, ila ebu jaribu tu kuwa na subira. Ila kumbuka utakuja kupokea zawadi za karama fulani fulani kutoka kwa Roho Mtakatifu. Zitakushtusha mwanzoni na kukushangaza, ila uzitumie karama hizo kwa busara. Kwa maana najua unajisikia kuwa huna msaada, lakini Mimi sijakuacha, wala sitakaa niwaache Mitume Wangu, Manabii Wangu, Watakatifu Wangu; Neno hilo halitawahi kuvunjwa. Hivyo amani na iwe pamoja nawe.
Kumbuka, mbele ya pua yako, yako pale yale yote niliyokuahidi. Amani na iwe nawe Mwanangu. Kwa maana tutaongea nawe tena baadaye. Huyu ni Yehova. Huyu ni Mungu wa yote, Wakwanza na Wamwisho kwa yote yaliyoko Ulimwenguni. Kwa upendo na Amani, nakuaga hadi wakati mwingine utakapo omba. Nakupenda.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )