Sehemu hii ya sauti 85 ni ya dakika kama 10:35 (1.2 MB) imehaririwa (kufupishwa) kutoka kwenye habari yenyewe ya dakika 24 ya kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Kwanza fanya majaribio kutoka: sound.htm kuona kama mitambo yako ya kutoa sauti inafanya kazi sawasawa. Kuna sauti ya kukwaruza kwenye kanda au faili hii. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispaniola na lugha isiyoeleweka. Soma ujumbe wa hapa nchini wakati unaposikiliza mkanda huu wote iliuweze kupata matokeo mazuri.
Ilikusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4
au 28.8 kwenye komputa yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia
mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.

85. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 11 Juni 1992 saa 8:35 usiku katika lugha za Kihispaniola, na Kiingereza.
Kihispaniola:
Safina! Safina! Safina! Mtumbwi fulani utaingia kupitia mlango wa daraja la San Francisco. Muuangalie Mtubwi huo kwa sababu saa na wakati umekwisha wekwa. Muuangalie kwa macho ya umakini kwa sababu utakwenda kuwatisheni ninyi, Mtubwi chini ya Daraja la San Francisco. Utakuja sasa na uchafu, na machozi yake, na maumbwa shujaa na hodari. Maumbwa, maumbwa wabaya, maumbwa wachafu watakuja kwa Boti San Francisco, Waangalieni kwa macho ya umakini, kwa sababu mtakuja kuogopa sana. (lugha isiyoeleweka?)
Kiingereza:
Sasa sikilizeni Watoto Wangu, siku ile niliyokuwa nikiizungumzia katika Unabii mwingine na kwa njia mbali mbali, na kwa namna mbali mbali, ni wa uhakika. Nataka mtege masikio. Nataka msikilize Nabii huyu, nataka msikilize Unabii huu kwa sababu mmekuwa na wakati wa raha sana mpaka sasa. Kwa kweli mmekuwa na wakati wa raha na mna amini mambo yataendelea kuwa hivyo hivyo tu, lakini nasikitika kuwakatishia matumaini yenu hayo, kwani mambo hayatakuwa hivyo siku zote. Njia pekee ya Mimi kuwatayarisha ni kuwaonya ninyi, kuhusu kitakacho kuja kutokea hapo baadaye.
Kwa maana Nawapenda ninyi nyote, lakini Wale tu walio wasafi, Wale walio Wanyoofu, Wale ambao hawana lawama ndio pekee watakao kwenda kumlaki Mwanangu Mawinguni. Kwa maana saa na siku itawajia ghafla bila mategemeo, bila ishara yeyote. Itatokea kwa ghafla, fumba na kufumbua; na kisha mwanzo wa mwisho utatokea. Mmezoea shughuli zenu za nini leo ufanye na nini kesho ufanye, lakini inakuja siku ambako hakuta kuwa na kesho tena kwa Sayari hii.
Akili zenu nasikitika kusema imefungwa kabisa. Mnaona maovu. Mnakimbiza maovu kila mahali hata kama mmefungwa mikono na miguu, bado mtakimbiza uovu. Lakini Mimi, Mungu wenu wa kila kitu kilicho Safi, na Takatifu na Kinyofu wala hamnitafuti Mimi. Wakati Nabii Wangu anapokupa Neno langu, kwa mkono wake wa kulia, na machozi machoni mwake, akijua anaweza kupoteza mkono wake kwa kukupa Neno Langu, lakini huo ndio ukweli wa Dunia hii.
Ninyi Wachungaji Wanyoofu, ninyi Wanatheologia Wanyoofu, ninyi watu mlio na Mungu wenu ndani ya boksi na hamwezi kuona nje ya maboksi yenu hayo; katika sheria na utaratibu wenu; Ninyi ambao mnatembea juu ya vipofu, na mnawakanyaga viziwi; ambao hamuoni shida kukimbizana na Dola (shilingi), kukimbizana na fedha zile. Mnaotumia Biblia kushibisha matumbo yenu. Lakini je, mnawafuata Watakatifu Wangu walioko mitaani, ambao wanakula uchafu, ambao wanalala nje juu ya ardhi (badala ya kulala kwenye nyumba na juu ya vitanda), kwenye baridi bila nguo, bila kuwa na kitu cha kula? Nitamwajibisha kila Mchungaji, kila Kasisi, kila afisa aliye na madaraka katika Mwili wa Kanisa la Yesu Kristu wa Nazareti.
Wakati wako utakapo kuja, wakati goti lako litakapo inamishwa kwenda chini, itakuwa aheri yako kama utakuwa unajibu sahihi, kwa sababu Yesu Kristu wa Nazareti alikupa wewe maagizo kamili. Alikuambia nini la kufanya. Na Mimi Baba, mwumbaji wa Mbingu na Dunia. Sioni kama unafanya yale uliyotakiwa kufanya.
Naona Manabii Wangu wakipondwa pondwa, wakikanyagwa, wakipigwa mateke na kufukuzwa makanisani, wakichapwa kwa maneno, wakizomewa, wakidhihakiwa, wakishutumiwa hadharani kwa kutangaza Neno Langu.
Hasira ya Mungu iko nyuma ya visigino vya viatu vyenu, inawezekana humisikii, lakini kuna siku inakuja ambako, ambako goti lile litabidi liinamishwa na ulimi ule, ambao ulitumika kwa ujanja na kwa ustadi mkubwa ili kujaza matumbo yenu, uzungushwe kwenye shingo zenu. Yakumbukeni Maneno Yangu. Kama kweli Jina Langu ni Yehova, Jina Langu ni Yehova na Jina la Mwanangu ni Yesu Kristu wa Nazareti, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana, Neno Langu halitanirudia bure; halijawahi kurudi tupu na kamwe halitawahi kurudi tupu.
Kwa maana hali ya Kanisa la leo, ambalo Mwanangu alilianzisha, liko kwenye hali ya vurumai kubwa kwa sababu yenu ninyi Wanatheologia, ninyi Wachungaji, na ninyi Makasisi. Embu jiangalieni, ninyi watu mnaojifanya kuwa Wanyoofu ambao mmepotea kabisa, mlio na Biblia mkoni kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine miguu yenu iko Jehanamu.
Je, ni mara ngapi kwa wiki mnaenda kuwatembelea Wagonjwa? Mara ngapi kwa wiki, mnaenda mitaani kuwasaidia Watakatifu Wangu? Mara ngapi kwa wiki, mnawalisha wenye njaa? Je, ni mara ngapi kwa wiki mnawavika wale wasio na nguo?
Lakini je, ni mara ngapi mnakusanya fedha zile kwa wiki ilikujivika nguo ninyi wenyewe, kujitunza wenyewe na kushughulikia mahitaji yenu? Mara ngapi kwa wiki mnanyoosha mikono yenu, na NI MARA NGAPI KWA WIKI MNAWAENDEA NA KUWAHUDUMIA KABISA?
Muda wenu itabidi muutolee hesabu yake. Kumbukeni hayo! Mikutano yenu hiyo midogo, vyama vyenu hivyo vidogo, je, ni roho ngapi zimepotea kwa sababu tu mlikuwa na shughuli nyingi? Kwenye mikutano yenu midogo ya karamu za chakula cha mchana, za jioni, na hizo shughuli zenu za kijamii na za kibinafsi, ni watu wangapi Mitaani wamekufa bila kupata nafsi ya kuungamishwa dhambi zao?
Pamoja na Machozi, Machoni, na Upendo Moyoni Mwangu, Ninauangalia urasimu ulioko Makanisani. Kwa maana jinsi Kanisa linavyozidi kuwanyongonyea/ndogo ndivyo hivyo hivyo naye Shetani anavyozidi kuwa mkubwa, lakini yote hayo yanafikia kwenye kikomo/tamati. Unaweza kututumua kifua chako mbele. Mnajifanya kuwa watu Wanyoofu, na munajivunia na kujidai kuwa ninyi ni Watu wa Nguo (Watakatifu). Mtu wa Kweli, Mchungaji wa Kweli wa Yesu Kristu wa Nazareti anabeba Msalaba wake Mitaani, kwenye vichochoro, maeneo ambako watu wenye hali nzuri hawapatikani au wanapatikana kwa nadra sana. Maeneo hayo ndiko Mwanangu alikowatuma ili kutafuta Kondoo wake waliopotea, wale waliona mahitaji. Nataka mkumbuke hayo niliyowaambia sasa hivi.
Wakati ujao utakapotoa ile hotuba yako nzuri kuhusu jinsi utakavyo barikiwa ukitoa kwa Kanisa, kwa kila Dola (shillingi), kila senti ambayo utakusanya itabidi muitolee hesabu, na ile ambayo haijaenda kwa Kondoo Wangu itabidi muilipe mara sabini, mara sabini kwa kila senti, kila Dola (shilingi) ambayo umeitumia vibaya.
Kwa hiyo weka tangazo hilo kwenye kapu la Sadaka. Hivyo ndiyo Anenavyo Yehova, Bwana wa Mabwana, Mfalme wa Wafalme, na Roho Mtakatifu, Kwa maana naenda kufunga maisha ya Sayari hii ndogo. Kwa maana njia za Binadamu zimefikia tamati yake, Nasema Maneno hayo kwa Moyo wa huzuni. Nasema kwa ukali. Nasikika mbaya, lakini huwezi kusema kwa maneno mazuri wakati unakanya, lakini ninawapenda. Kumbukeni hayo pia. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )