86. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 11 Juni 1992 saa 8:51 usiku wa siku ya Alhamisi, katika lugha ya Kihispaniola.
Nyumba, Nyumba Yangu. Viko tayari, vyumba huko Mbinguni kwa ajili ya Watakatifu Wangu. Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Yote ni safi, na kila kitu kiko tayari. Siku ile mtakapokuja Mbinguni na Mwanangu, kila kitu kitakuwa kisafi, kwa maana huku Mbinguni hakuna kitu kichafu. Nawe unaweza kuishi Mbinguni kwa siku zote ambazo kutakuwa na siku. Unaweza kufanya lolote unalotaka kufanya. Unaweza kufanya kazi. Unaweza kula. Unaweza kwenda likizo. Unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya, lakini kila kitu ni kisafi. Watakatifu Wangu inabidi wawe wasafi, hicho pekee ndicho ninachotaka. Ni lazima wawe wasafi. Kuna furaha kubwa sana pale.
Huyu ni Baba Yenu pamoja na Yesu na Roho Mtakatifu. Mnisikilize Mimi! Mbingu inawangoja kwa sababu muda umefika, ambao niliwaambia Mababu wa Mababu wa Mababu wa Mababu. Kwa maana ninachosema ni cha ukweli, lakini Mimi nataka muwatafute Kaka zenu na dada zenu. Nataka muwaambie kuhusu Kristo Mwanangu, kwa maana hawawezi kuja Mbinguni bila ya kumtafuta Mwanangu Yesu. Kristu (Mfalme) wa Dunia yote, wa kila kilichoko.
Ndiyo. Mnisikilize Mimi! Waiteni Kaka zenu na Dada zenu, kwa simu, kwa barua, kwa njia yeyote ile unayotaka. Anza sasa hivi kwa sababu muda unapita. Harakisheni! Waandikieni Ndugu zenu, Marafiki zenu, kwa marafiki zenu wa kike, waambie Mbingu iko wazi, kwa yeyote anayempenda Mwanangu Yesu Kristo, na Mimi Baba pamoja na Roho Mtakatifu. Kwa maana hakuna chochote kingine kitakachoweza kuwaokoa Duniani humu, kuna kifo tuu, pamoja na shetani.
Je, Mmenisikia? Basi ebu zibueni na kusafisha macho yenu na masikio yenu hayo, kwa sababu siku ile inakuja ya Yesu Mwanangu. Ndiyo, iteni! Muwaiteni kila mtu mnayeweza kumwita; waiteni walioko mitaani; walioko barabarani; walioko kwenye migahawa, ndiyo, na wale walioko kwenye treni, kwenye mabasi, popote walipo. Waambieni kuhusu Kristo, kuhusu Mbinguni, kuhusu Baba yenu, kuhusu Roho Mtakatifu, kwa sababu tuna Wapenda kwa Mioyo yetu yote. Na kila kitu hapa ni kisafi na tayari. Vyumba vyenu! Vyumba vyenu, vitanda vyenu, meza zenu, viti vyenu; ambavyo mnavipenda sana. "MIMI" Huyu ni Baba Yenu pamoja na Mwanangu Yesu, pamoja na Roho Mtakatifu.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )