Sauti 89

 Sehemu hii ya sauti 89 ni ya dakika kama 7:23 imehaririwa (kufupishwa) kutoka kwenye mkanda wangu mdogo wa kurekodia. Unabii huu uko katika lugha ya Kiingereza, Kihispaniola na lugha isiyoeleweka.

Ili kusikiliza mkanda huu unahitajika uwe na Kadi ya sauti, na Modamu ya 14.4 au 28.8 kwenye kompyuta yako. Ili kupata "the RealAudio Player" ya kusikilizia mkanda huu kama haipo kwenye komputa yako, bonyeza kwenye kitufe hiki.


 

89. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 12 Juni 1992 saa 8:31 usiku wa siku ya Ijumaa katika Kiingereza.

Naam! Ray, Nasikia maombi yako. Najua una wasiwasi kuhusu fedha. Najua ni shida, lakini Mimi najua vyema hali halisi kuliko unavyoweza kuniamini. Mimi nitalishughulikia swala la fedha uniachie; ila wewe endelea kuandika na kufanya kazi hiyo kama ulivyokuwa ukifanya siku zote.

Kwa maana utakuwa unautuma na kuugawa Unabii huu kwenye maeneo nitakayo kuelekeza. Nitakupa maelekezo hayo; wakati huo ukifika. Kwani shughuli za kuanza kuziweka kwenye karatasi; zitaanza pale ambako utakapo kuwa umemaliza kufanya yote niliyokuagiza kufanya.

Utakuwa unaendelea kupata ujumbe zaidi na zaidi na zaidi kutoka Kwangu; kwenye maeneo mengi tofauti tofauti ya maisha, ambayo naona yanaudhi, lakini kumbuka Mungu wako yuko nawe siku zote pamoja na Mwanangu, na Roho Mtakatifu, Yehova muumba wa kila kitu kilichopo, na kila kitu ambacho kitakuja kuwepo, ni Neno la Kwanza na Neno la Mwisho.

Nimehisi Roho yako ikibadilika katika wiki hizi chache za mwisho. Umeanza kuwa imara. Umeanza kuelewa zaidi mambo yajayo. Unaanza kweli kuamini moyoni mwako, kwa sababu Mimi nasoma Moyo Ray.

Najua imekuwa ngumu sana kwako. Ukijaribu kuwaza kama ni mambo ya ukweIi au ni ya uwongo, au labda utakuja kumpotosha mtu mwingine. Najua hupendi kufanya hivyo. Najua hujisikii vyema kwa sababu hujui unaandika nini.

Kumbuka maandishi ni Mimi, Yehova, Yahwe, Ndimi Mimi, Ndimi Mimi, Ndimi Mimi. Siyo wewe. Kama nilihitaji ujue yote; Ninge kuambia yote. Kwa wakati huu wa sasa kuna mambo fulani tu ninayotaka uyafahamu, na kuna mambo mengine sitaki uyafahamu. Ninakuambia kwa lugha usiyoelewa yale ambayo sitaki uyafahamu ila roho yako inajua na roho yako inakua.

Kwa maana mwili wako ni adui wako. Ni kwa faida yako mwili wako usielewe mambo fulani fulani. Ninaongea na roho yako na roho yako hiyo inakupa ile cheche ya maisha ambayo itakupeleka kwenye eneo linalotakiwa. Ile karama ya utambuzi uliyopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu; itakuongoza kwenye upande ule ambao Mimi nataka nikupeleke. Kwa hiyo ebu jaribu kuwa imara, uwe mjasiri. Maneno ni rahisi kusemwa lakini ni magumu kutekelezwa.

Kwa maana Mimi naangalia Moyo wako. Najua kuwa wewe ni mtu asiyekata tamaa, mara unapoamini. Wewe simama tu kwenye Mwamba, pamoja na Mwanangu na hakuna chochote kitakacho kutikisa. Kwa hiyo ndiyo sababu Mimi nimejaribu kukushawishi pole pole kuwa; unaongea na Yehova, Mungu Muumbaji wa Mbingu na Dunia, wa yote yaliyoko na yatakayo kuwapo. Kwa sababu najua udhaifu wako na uwezo wako, ninakuvua yote mpaka umekuwa si kitu; ili nikujenge upya, kazi hiyo ni yenye maumivu wakati fulani, lakini ninakuhitaji.

Vita vinaendelea kunguruma na Sisi inabidi kuendelea kufanya yale ambayo inabidi kufanya. Usijali, Yehova ndiye anayeongoza yote. Sijawahi kuchelewa wala sitakaa kuchelewa. Kwa hiyo ebu jaribu kuweka wasiwasi mbali. Endelea kuniomba na Mimi nitakujibu. Utapata jibu kama nilivyo sema hapo mwanzoni. Kila nilichokiahidi kitakuja kutimia. Kwa sababu Mimi siahidi kisha nisitekeleze. Kumbuka hilo Ray.

Wewe ebu kunja mikono ya shati lako juu, anza kazi kwenye ile Kompyuta. Inabidi tubadilishe mwelekeo wa Dunia hii uelekee Mbinguni, kwa maana mwisho wa Dunia hii umefika. Inabidi Sisi tukusanye Kondoo, lakini wewe ebu tii; niachie nifanye kazi hii. Inasikika kama Neno rahisi sana Ray, Mimi najua wewe unaweza kufanya kazi hii kama isingelikuwa hivyo nisingeli kuchagua wewe.

Najua kuna nyakati huwa unaangalia nyuma, ukiwaza ya nyuma jinsi ulivyokuwa na jinsi ulivyo hivi sasa, lakini usijali kuhusu marafiki zako uliowapoteza, kwa maana kwanza wale hawakuwa marafiki wa kweli kwa kuanzia. Kaza macho yako kwa Yesu. Yesu Kristu wa Nazareti Mfalme wako na Mimi, Yehova, Roho Mtakatifu atakupa nguvu na Karama ambazo zitabubujika kupitia kwako. Najua itakuja siku ambayo utalazimika kuzitumia ili kujilinda. Hakuna chochote Ulimwenguni, Mbinguni, Duniani kinachoweza kumshinda Yehova, kwa sababu nilifanya vyote, na wewe uko mikononi Mwangu.

Kwa hiyo usijali kuhusu watu hawa wenye machukizo yao madogo madogo, michezo yao midogo midogo, sheria na taratibu zao ndogo ndogo ambazo zinajaribu kuthibiti na kutawala. Inawafanya wajisikie kama miungu midogo. Wewe vuta nguvu zako kutoka Utatu Mtakatifu. Mimi ndiye Mungu Mkuu, Mimi ndiye yule Mimi Ndiye, Mimi Ndiye. Kumbuka hilo. Wakikunyanyasa ni sawa na kuninyanyasa Mimi. Hilo ni rahisi. Hilo ni wazi. Kwa maana Mimi nimeweka muda maalum wa kukusanya kondoo, kwa maana Mwanangu anatayarisha yale ambayo inabidi yafanyike, ili kukusanya Kundi.

Kwa sasa lala vizuri mpaka hapo tutakapo zungumza tena. Ninakupenda wewe. Nitakuchukua wewe na nitakulinda. Kumbuka lile Neno dogo "Amini". Huo ni utani Ray, kwa sababu hilo ni Neno kubwa. Mtu anayemwamini Mungu wake kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu ni mtu asiyeonekana na asiyeshindwa. Laiti kama ungeliona Jeshi la Malaika wa Mbinguni lililoko hapo karibu kuitikia mwito wako kwa kupitia maombi yako, kwa sababu Mimi najibu Maombi. Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme, Mwanangu, Jemedari Mkuu atawaongoza Malaika walioko kwenye madaraka yake; kwa kadri ya hiari yake.

Kwa hiyo Ray, usijali kuhusu yale ambayo huyaoni au hayaonekani, kwa sababu Sisi ni halisi kabisa. Wakati Kristu atakapokuja kwenye Mawingu; utatambua yote niliyokuwa nikikuambia; kwa miaka sasa. Kwako wewe ni miaka mingi lakini Kwangu Mimi; ni muda mfupi kiasi ambacho hata hautoshi kusemwa. Amani iwe kwako. Chukua Mapumziko kidogo. Kwa maana kesho tuna kazi ya kufanya. Kumbuka kuwa Ninakupenda.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.