90. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 12 Juni 1992 saa 6:55 usiku katika lugha ya Kiingereza.
Nakupenda Ray. Kwa kuwa umeshindwa kulala basi na tuongee. Ebu nikuambie kidogo kuhusa Vita, Vita vijavyo. Chui wa aina ya Taiga mwenye meno makali atatekwa; lakini Mnyama na Nguruwe dume; watatumia hila za kijasusi kwa msururu wa Majasusi na Ujasusi ndani Ujasusi kuvuruga na kupindisha uongozi wa Serikali nyingi. Kwa njia ambayo kutakuwa na rushwa kwa wingi; ambayo itakuwa inaendeshwa (kwa siri) chini ya meza na hao Viongozi wa Siasa; ambao wanaendesha Serikali hizo; kwa kiasi ambacho hutaweza kudhania. Wakati atakapopata mamlaka ya kumiliki mafuta na fedha; atatumia nyenzo hizo kunyanyasa na kudhibiti kwa vitisho nchi hizo. Atatumia kila mbinu na hila; ili apate njia yake na atafanikiwa kupata njia yake.
Lakini Mimi; ninamtayarishia mahala kwa ajili yake. Anadhani atakuwa na Dunia mikononi mwake, lakini yote atakayopata ni lile Shimo (la Jehanamu). Mpinga Kristo atakuwa mmoja wa Madikteta wakali na wa kutisha sana, ambaye Dunia imewahi kuwaona. Kwako inaonekana kuwa maneno ya kawaida ambaye hayana maana; maneno ya kijujuu. Hamjawahi kuona dikteta wa kutisha wa aina hiyo, lakini hivyo ndivyo mwisho utakavyo kuja.
Kutakuwa na milipuko katika Miji Mikuu ya nchi, katika Majiji makuu, dunia nzima. Kutakuwa na Jeshi la polisi ambalo halitakuwa na sheria. Ila sheria ya mpinga Kristo, ambayo ni sheria ya shetani. Ataanzisha Ufalme, ambao utakuwa kiini cha Mamlaka yake ambako; atadhibiti ni kitu gani watu wananunua, nini watu wanauza, na ni nani anaishi ndani ya nyumba zao, ni akina nani na wanaishi wapi jamaa zao na wanafanya nini kwa kujikimu kwa maisha yao, wanaenda Makanisa yapi, na ni makanisa yapi hawaendi. Atakuwa na udhibiti wa aina hiyo.
Kisha atatekeleza uwekaji wa mihuri yake ambayo; itawekwa kwenye nyuso za vibaraka wake ambao atawamiliki na kuwaongoza ili wakatekeleze matakwa yake. Kama unathamini maisha yako ya Kiroho; usipokee mhuri huo wa Mnyama. Kwa maana Muhuri wa mnyama utamaanisha mwisho wa miisho kwako. Kwa hiyo jihadhari na Muhuri ambao utawekwa kwenye mkono wako au usoni mwako. Haijalishi wapi utawekewa; kama utaupokea hutaona kamwe Ufalme wa Mungu, Yehova, Mbinguni au majumba yale ya Fahari niliyowatengenezea. Kwa sababu Mwanangu alikufa kwa ajili yenu; kwa ajili ya kusudi maalum ya kuleta Kundi la Kondoo nyumbani Mbinguni. Lakini uchaguzi ni Wako.
USIKUBALI KUWEKEWA ALAMA AU MUHURI WA MNYAMA. Huyu ni Yehova, Muumbaji, Muumbaji wa Ulimwengu. Kwa maana naenda kuifunga Sayari hii iliyonajisiwa na ambayo imeoza, ambayo itaangamizwa na kila kitu kilichoko mbacho siyo Kisafi, Adilifu, na ambacho hakipo sambamba na Neno Langu, Yehova.
Kwa hiyo muwe imara Kondoo Wangu wa Kiume na wa Kike. Kwa maana saa imewadia, nendeni ndani ya chumba kile, funga mlango ulie na uombe. Uombe kanakwamba hujawahi kuomba kamwe kabla, kwa maana muda na siku iko nje tuu ya mlango wako.
Mjilinde wenyewe, ingieni katika Mwili wa Kristu, na Yesu atawalinda, lakini inabidi Muwe wasafi, mliotakata na kutubu. Ile kuitwa Mkristu tu, haina maana yeyote. Nataka kilicho Takata na Kisafi, Moyoni, Rohoni, katika Mawazo, na kilichoweka macho yake yote kwa Yesu Kristu, Roho Mtakatifu na Mimi.
Kwa maana zawadi mtakazopata ni nje ya mategemeo yenu. Kwa hiyo ebu uwe na Imani na Matumaini katika Bwana wako na Mwokozi wako. Kwa maana Yeye atatawala na kuongoza, na kuwalinda Kondoo Wangu wa Kike na wa Kiume. Huyu ni Yehova. Huyu ni Yehova Muumbaji, Muumbaji wa Ulimwengu. Amani iwe Nanyi. Upendo wa Moyo Wangu. Upendo wa Mwanangu. Upendo wa Roho Mtakatifu. Amani na muwapende Kondoo wenzenu wa Kiume na wa Kike. Hivyo ndivyo asemavyo Yehova.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )