91. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 13 Juni 1992 saa 4:15 Usiku katika Lugha, Kihispaniola.
Naam Mwanangu Safina! Safina! Mwanangu umechoka? Mwili wako umechoka. Umefanya kazi kwa masaa mengi, lakini unafanya kazi nzuri. Ninakuangalia. Nakuangalia na ninapenda juhudi yako na huo moyo wa kutokukubali kukata tamaa, kwa sababu utahitaji moyo na nia hiyo ya kutokukubali kukata tamaa kumaliza ninachotaka ufanye, ila kwa sasa ebu pumzika.
Utakuja hapo baadaye kuona vitu katika mawazo yako. Havitakuwa vitu ulivyo viweka wewe mawazoni mwako. Vitakuwa vitu vinavyo toka kwa Mungu. Nataka wewe uviandike na kisha uviweke kwenye kumbukumbu. Nataka watu waone kwa kupitia macho yako. Nataka wakusikie wewe, kwa kupitia kwenye maandishi yako ya yale niliyoyasema. Najua umechoka na isitoshe hujalala na wala hata hujala. Lakini nadhani unafanya kazi nzuri. Nitakuambia wapi uyapeleke maandiko haya na lini.
Tayari umekwisha tuma yale ambayo nilikuambia uwapelekee wale watu wanaokuombea. Nataka wasome yale ambayo ninakueleza wewe kwa sababu utakuja kuhitaji msaada wao. Wewe uko vitani na huwezi kupigana wewe peke yako. Utahitaji msaada wa ndugu zako na dada zako wa Kikristu. Kwa maana mtakapo pigana pamoja kila mtu atakuwa imara zaidi. Kumbuka hilo! Nataka ufanye ninachotaka ufanye, na utahitaji maombi ya Kaka zako na Dada zako.
Najua watu wa Dunia hawatakuamini wewe. Hilo siyo la maana, la maana ni kuwa wewe unafanya ninalokuambia wewe ulifanye, kwa maana siyo ngumu kama unavyodhania. Tayari ninajua kilicho kwenye mawazo yako. Una wasiwasi, lakini kumbuka kuwa; wewe uko kwenye Mikono ya Mungu; Yesu, Roho Mtakatifu na Mimi, Baba yako. Na kama watapigana na wewe watakuwa wanapigana na Mimi.
Najua unadhania kuwa haya ni Maneno matupu tu, lakini siku inakuja ambako nitakuonyeshea miujiza. Una nguvu za Roho Mtakatifu ambaye atakwenda kufanya kazi ndani ya mwili wako. Usiogope kwa maana wakati fulani mwili unatishika wakati nguvu za Roho Mtakatifu zinapoanza kuutumia (mwili huo). Kwa sababu mwili siyo msafi na hali Roho Mtakatifu ni msafi. Kwa hiyo usiogope wakati Roho Mtakatifu atakapokujia kwa maana kutakuwa na miujiza.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )