93. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 15 Juni 1992 saa 9:41 Mchana katika Kihispaniola.
Tazama Reymundo, kama nilivyosema hapo mwanzoni, Sisi ndio kwanza tunaanza na tarehe na siku ambayo hiyo kazi itasimama au kukamilika sitakuambia. Nataka tu; ufanye ninalokuambia. Nitakuwa pamoja nawe. Najua unataabika hivi sasa. Nasikia maombi na machozi yako. Najua unajisikia vibaya moyoni mwako. Wewe huelewi uendako; kama uende hapa au pale, au ufanye kazi, au labda uweke Unabii kwenye Kompyuta. Tazama Mimi kile ninachotaka wewe ukafanye ni kusikiliza Neno Langu na kuitekeleza. Sasa hivi Neno Langu linasema, kaa chini na ufanye kazi. Andika maneno yale Ninayokuambia.
Najua Moyo wako. Najua kuwa unalia kwa sababu umechoka kweli. Unashindwa kunyanyua kichwa chako juu sawasawa; kwa sababu unasinzia sana. Inaumiza Moyo Wangu kuwa inakubidi ufanye kile ambacho lazima ukifanye. Uwe imara kwa sababu Mimi niko pamoja nawe. Sisi (Mimi na wewe) hatuna muda mrefu wa kutosha. Kila kitu lazima kitokee kwa wakati wake; kama nilivyopanga miaka mingi iliyopita. Wakati huo sasa umewadi. Najua kuwa unayo nguvu inayotakiwa kufanya kazi hiyo. Najua unayo uweza wa kufanya lile ninalokuambia. Najua utakuwa unalia kila dakika ya kila siku. Naujua moyo wako. Najua unaweza kufanya.
Ndiyo, mawe yatakuja na wewe utachoka wakati yatakapokuja, lakini Mimi niko pamoja nawe, pamoja na Malaika Wangu. Watakwenda kukulinda. Hakuna mtu atakaye weza kukugusa. Inabidi uniamini Mimi. Utakuja kufahamu kiasi cha Imani ulicho nacho. Nguvu ile utakayokuja kuihitaji itakuwa na wale wanaojidai wakuifahamu Biblia. Watakuja kushangaa kuwa walikuwa wameiona Neno Langu, lakini bado walikuwa hawajaiona kwa usahihi. Watu hawa watakuwa wanajiamini sana vichwani mwao. Hawaamini kuwa wanaweza kufanya kitu chochote kibaya na Biblia. Hii ni kwa sababu shetani amewaingia.
Shetani amewapa mioyo migumu. Wao ni imara kwa mkono wa koshoto na wala si kwa mkono wa kulia. Hawa ndio watu watakao taka kukutafuna. Lakini Mimi niko pamoja nawe na usisahau zile karama nilizokupa. Usiogope kuvitumia. Kwa maana una Mungu wa Mbinguni, wa Dunia, wa Malaika, wa kila kitu kilichopo, na kitakacho kuwapo, mikononi mwako.
Najua wewe siyo mkubwa lakini Mimi nachagua walio wadogo. Kwa maana kwa njia hiyo wao wataamini kuwa Mimi ni Mungu wao. Kwa maana Mungu wa kila kitu hachagui watu walioko juu na wala wakubwa au maarufu. Kwa maana Mimi nawatumia Watu ambao hakuna atakayeamini kuwa wanaweza kutumiwa na Mungu wa Mbinguni. Unafanya kazi kwa bidii sana na kwa makini hivi sasa. Hakuna atakaye weza kukuzuia. Niliweka hilo moyoni mwako na akilini mwako. Kwa maana Maneno Yangu yatakayo toka kupitia midomo yako yanaenda kuokoa mamilioni ya mamilioni, ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya mailioni ya mamilioni ya mamilioni ya mamilioni ya watu. Hiyo ndiyo maana inakubidi uwe imara.
Kwa maana watajakuja na mawe. Pamoja na kila ubaya wanaotaka kukufanyia. Kumbuka Reymundo, Mimi niko pamoja nawe, hiyo ndiyo maana ni ya muhimu sana kwa wewe kuwa imara na kufanya kazi na Kompyuta yako ndogo. Nakupenda sana kwa Moyo Wangu na wewe umo ndani ya Mikono yangu. Najua unaamini wewe uko peke yako. Unadhania kuwa sikusikii kwa sababu unaomba na unalia, na unaomba na unalia, na unaomba na unalia, na huoni lolote linalobadilika. Ebu wewe fanyakazi tu, fanyakazi yako na Mimi nitafanya kazi Yangu, na kila kitu kitakuja kuwa sawa sawa.
Ebu niamini Mimi tu. Huyu ni Mungu Wako. Huyu ni Mungu wako pamoja na Yesu na Roho Mtakatifu. Pamoja na kila kitu kilichoko na kitakacho kuwapo, Mimi ni Neno la Kwanza na Neno la Mwisho. Kumbuka Reymundo. Nina upendo wa Dunia. Nina upendo wa Moyo Wangu ndani ya Moyo wako. Furaha nyingi mwanangu, uwe imara. Tazama inakuja wakati ambako kila kitu kitakuja kukoma. Inabidi uwe imara. Huyu ni Mungu Wako. Huyu ni Mungu wako pamoja na Mwanangu Yesu na Roho Mtakatifu na Mimi. Baba yako atakwenda kukulinda.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )