94. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 16 Juni 1992 saa 9:04 mchana siku ya Jumanne katika lugha za Kiingereza na Lugha isiyoeleweka.
Ramses, Ramses ataanza kusonga kwenda kuelekea mstari wa mbele pale Kunguru atakapo kuwa anaruka kuelekea magharibi lakini Mende atabaki nyuma kwa sababu Mende ameumia na Mende ataanguka. Wakati Safina itakapowekwa mahala pake, Mawingu na Yesu Kristo wa Nazareti watawapokea Wakristu wenye mioyo iliyotakata, mawazo yaliyotakata na miili iliyotakata, wale walio watiifu na wanyenyekevu. Wale wanaonitii Mimi Yehova kwa mambo madogo. Mambo yale mnayopitisha kama, "Sawa, nitayafanya kesho kwa sababu leo nimechoka"; Kwa yale mnayosema, "Hiyo siyo kazi yangu bali ni kazi ya mtu mwingine "; Kwa maana Yehova anaangalia Mioyo, na hakuna njia yeyote mtakayoweza kuibuni ya kunidanganya Mimi.
Kwa maana njia na namna ya Jehova kamwe haitafanana na ya Binadamu. Inakubidi umtafute Yesu Kristu wa Nazareti, naye Roho Mtakatifu atawaonyesheeni njia na kuwaongoza. Watu wa Duniani, sitajali kama wewe ni mtenda dhambi au Mkristu au wa dini ya rika mpya "New Age". Sijali unajiitaje. JINA siyo la maana kwangu Mimi. Kilicho cha maana kwangu Mimi ni kuwa; unafanya kwa wengine, kama wewe unavyotaka ufanyiwe na wengine. Umpende jirani yako. Utubu dhambi zako mara unapoanguka, na umwangalie Yesu Kristu wa Nazareti, Mwanangu.
Kimsingi ni Rahisi. Imenyooka. Ni Nzuri. Ni Safi. Msaidiane ninyi kwa ninyi. Kwanini hiyo iwe ngumu kueleweka? Mna Imani nyingi tofauti, na mna Dini tofauti nyingi katika Jina la Kristu. Kwa hiyo wengi wenu mmechanganyikiwa mno kuhusu Yesu. Mnamtafuta mahala pale na pale. Mnamtafuta Kanisani. Mnamtafuta kila mahali mnapodhania yuko. Kwanni mvipofu kiasi hicho? Yule Mshauri, Yule Mfariji, yuko pale sasa hivi, pamoja nawe SASA HIVI, SEKUNDE HII.
Anakusemesha. Akijaribu kukuonyeshea njia ile ya kwenda kwa Yesu Kristo wa Nazareti. Yote unayotakiwa kufanya ni kuondoa mikono yako kutoka masikioni mwako na kuviondoa machoni mwako. Sikiliza! Sikiliza ile sauti inayokuambia uwe mwema. Sikiliza ile sauti inayokumbia msaidiane ninyi kwa ninyi. Achana na Ulafi, huku kujisifu, huko kujigamba, hata kama ni katika Jina la Yesu kwa maana Yesu hapendi mtu yeyote anayejisifu, yeyote anayejigamba. Mjinyenyekeshe wenyewe, saidianeni ninyi kwa ninyi, wagonjwa, vilema, wasio na mahali pakuishi.
Mna matatizo mengi sana. Nasikitika kusema hakuna yeyote anayemsaidia mwenzake; kwa namna ile iliyoagizwa kwenye Biblia. Kila mtu anaenda njia yake. Mnakuwa na wasiwasi sana kuhusu Kanuni. Mnawasiwasi kuhusu kama mtakubaliwa, na kikundi cha Kanisa lako. Nataka muwe katika kundi la ndani pamoja na wasio na mahali pakuishi, wenye njaa wagonjwa. Hilo ndilo kundi la ndani. Hilo ndilo kundi ambalo Yesu alikuja kuisaidia: Wale ambao hawana mtu wa kuwasidia; wale ambao wananuka wakati unapo wakaribia; wale ambao wamekonda kiasi ambacho wanakuwa hawana sura; wale wanao ganda kwa barafu usiku kwa sababu wanalala nje kwenye mitaa; wale ambao mapepo wamewafunga katika ulevi wa kila aina na umalaya kiasi ambacho hawaelewi wafanye nini.
Niliwapeni uwezo kwa njia ya Roho Mtakatifu kutoa mapepo, kuponya wagonjwa. Karama zote nimewapeni lakini mmekuwa na shughuli nyingi katika mambo yenu binafsi, katika Makanisa yenu madogo mkijaribu kuridhishana ninyi kwa ninyi. Ni aibu ilioje. Ni aibu ilioje. Ni aibu ilioje. Nawapenda wote, na Ninataka ninyi nyote mje mkaishi Mbinguni. Haijalishi ulifanya nini. Haijalishi unafanya nini. Kinacho jalisha ni kama unasikia Neno Langu na kisha hamsahihishi njia zenu. Kwa maana hapo ndipo utakapo kuwa umepotea, kwa maana shetani atakuwa amekuchukua.
Kwa maana Sheria ya Yehova, Sheria ya Yesu Kristu Sheria ya Roho Mtakatifu, ni rahisi sana: Mgeukie Yesu. Kwa Yesu kuna njia ya kuja Kwangu Mimi Yehova. Nguvu za Roho Mtakatifu ziko hapo kwa matumizi yenu. Someni Biblia kwa makini na kwa kujiachia. Usiseme au usitoe imla kwa watu wengine kuhusu nini Mimi nitakachosema, hiyo ni Kazi Yangu. Mimi ndiye ninaye waambia watu nini nataka. SIYO KAZI YENU KUWEKA MANENO KINYWANI MWANGU. Kwa maana Mimi nina uwezo wote wa kujiongelea Mwenyewe.
Ninyi Wanatheologia; ninyi tu ni..., Kwa kweli sielewi jinsi ya kueleza, "Kwa njia gani na wakati gani," matukio yale yatakayotokea. Mahali mtakapo simama na Wapi mtakapo simama imara na kuwaongoza kundi lako kwenye usalama, kwa maana mnayumbishwa kirahisi. Mna haraka sana ya kulaumu, mnapenda sana uhakimu. Mgeukieni Yesu; ni rahisi, imenyooka. Naenda kuwaweka wakfu Kundi (la kondoo kwa kazi ya kuongoza) kwa sababu uongozi umechanganyikiwa kabisa.
Kuna kundi ndogo ambayo bado haijaanguka lakini Wanatheologia wa kweli, wale wafuasi wa kweli wa Yesu hawana yafuatayo: hawana magari ya kuvutia, hawana suti za kuvutia, hawana nywele zilizotengenezwa za kuvutia, maneno ya kuvutia. Wale Wachungaji wa kweli wanaishi kifukara kwenye mitaa ya wafukara; wakila na wanaohitaji misaada. Wamewapa maskini hao mashati ya kutoka migongoni mwao. Wanatembea wakiwa na njaa. Wakitembea kati yao wakiwa hawana nguo lakini wakiwa wananipenda Mimi kweli kweli, kwa mioyo yao yote na nafsi zao zote. Wanapomwona mtu mwenye shida wanakuwa na mzigo mkubwa mioyoni mwao. Machozi yanawajia machoni mwao na kwa uwezo wao mdogo wanasaidia kwa walicho nacho, ambayo kwa kawaida si zaidi ya maombi na misaada midogo midogo; waliyo nayo kama ishara.
Upendo walio nao kwangu wanawapa wale wote wanao nipenda Mimi. Hawa ndio Wachungaji wa kweli wa Kundi Langu. Hawa ndio wafuasi wa kweli wa neno Langu. Siyo wale wanaoishi kwenye nyumba nzuri. Siyo wale wanaosema maneno ya kuvutia. Siyo wale wanaojitukuza wenyewe na kiburu na majivuno, waliojawa na Ubinafsi na kujikweza. Bali wale wanaoishi kwenye mitaa ya maskini na wanahudimu mtu kwa mtu. Ilikumwona; huna haja ya kutoa taarifa kwanza na kupata kibali mapema. Hawana ratiba kali iliyosheheni kiasi kuwa anahitajika Karani.
Kwa sababu wanaishi njia ya Kristu. Wanawasaidia maskini, Wazee. Wengine wao hawafanyi jambo lolote la kutisha kuhusiana na fedha, lakini wanasikiliza. Wanasaidia. Kondoo Wangu kila mmoja wenu anatakiwa afanye VIVYO HIVYO. Ukimsaidia jirani yako, mtoto mwenye kuhitaji msaada, kuwalisha wenye njaa kwa sababu ninyi nyote ni Makasisi, kila mmoja wenu.
Kwa hiyo, kwa hiyo kama kweli Jina Langu ni Jehova, Muumba wa Mbingu na Dunia kwa njia ya nguvu za Roho Mtakatifu, pamoja na Mwanangu Yesu Kristo wa Nazareti, natoa agizo kwa Makasisi Wangu, Watakatifu Wangu, mfanye kama Nilivyoamuru. Msingoje mpaka kesho. Tekeleza sasa hivyo kwa maana mwisho unakuja. Dunia itaisha. Msiwategemee Wachungaji wenu kwa sababu wamepotea. Wao wamejaa kiburi na wamefungwa na kuzamia katika Theologia zao. Ni aibu gani. Ni aibu gani.
Kwa hiyo Kundi Langu, Roho Mtakatifu anakwenda kuanza kuweka cheche za mizigo ndani yenu ya kuomba, ya kuwaombea majirani zenu, ya kuwaendea marafiki zenu na maadui zenu. Yakukusaidia kutubu. Ya kuwasaidia wengine kutubu; kwa maana hiyo ndiyo jinsi Mwili wa Kristo utakavyo kwenda pamoja katika mwili, na siyo katika uongozi, kwa maana uongozi una kwenda kuanguka kwa sababu wamechanganyikiwa na wamepotea.
Kwa hiyo Watakatifu Wangu, chukueni hatua, chukueni mamlaka, nendeni mkagonge kwenye milango, pelekeni habari njema. Pandeni juu ya nyumba, fanyeni lolote ambalo ni lazima lifanyike ili kuwaokoa ndugu zenu wa kiume na wa kike, kwa maana kama Mimi nilivyosema siku nyingi zilizopita, "mwisho utafika wakati ambao hamuutarajii." Waambie Kaka zako, Dada zako, na familia yako ya karibu, kwa maana familia yako ya kribu ni mahali pakuanzia.
Kwa maana Mbinguni ni mahala pa ajabu kwa kila kitu, lakini Jehanamu ni mahala ambako usingependa familia yako iwe, Mama yako, Baba yako, Kaka zako, Dada zako. Kwa maana kama hamtasikiliza Maneno Yangu wengine wenu watakuwa Mbinguni, na Kaka na Dada zenu wengine watakuwa mahala pengine. Hutapenda hivyo, wala Mimi sitapenda hivyo.
Roho Mtakatifu yuko hapo kuwapa ninyi chochote mnachohitaji. Inabidi mumwamini Mungu Yehova, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Kwa maana kutakuwa na matatizo/machafuko na taabu katika Sayari yenu siku za karibuni. Wachezaji (wa kukamilisha fainali ya mwisho wa nyakati) wana majukumu yao na wanayafahamu vizuri. Hasira ya Shetani itamwagwa juu ya kanisa pamoja na machozi kwenye Macho Yangu, ninawaombeni muwe imara, mgeukieni Mwanangu Yesu Kristu. Tubuni! Msiwategemee Wachungaji wenu, viongozi wenu. Kwa maana mtaanguka pamoja nao. Muwe imara; nendeni mkagonge milango; fanya lolote ambalo inawabidi mfanye. Kwa maana zawadi zenu Mbinguni zitakuwa kubwa. Kwa maana najua moyo wa nani ni msafi na wa nani siyo msafi. Na zawadi yako Mbinguni itakuwa kubwa sana. (Lugha isiyoeleweka?)
Asante Baba Yangu. Sifa na Heshima na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Heshima na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Heshima na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Heshima na Utukufu zimwendee Baba. Asante Baba kwa sababu Mapenzi Yangu ni Mapenzi Yako, na Mapenzi Yako yatatimizwa. Kulingana na Neno Lako lilivyoandikwa katika Biblia. Kulingana na kilichoelezwa kwa kupitia Manabii wako mbali mbali. Sifa na Heshima na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Utukufu zimwendee Baba. Sifa na Utukufu zimwendee Baba. Sifa zimwendee Baba.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )