95. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Juni 1992 saa 8:10 usiku katika lugha ya Kihispaniola, Kiingereza na Lugha isiyoeleweka.

Kihispaniola:

Kile kitu ambacho ni, Mwanangu. Kile kitu ambacho ni. Yule binti ni mgonjwa. Yule niliyekuambia hapo awali ni mgonjwa kwa sababu shetani anaweka shinikizo lake kwenye kichwa chake, akimwambia kuwa yeye hana thamani yeyote. Anaumwa sana. Nitakupa hakikisho. Mimi nitakupa hakikisho na kama wewe hutafanya nilicho kuambia, yule Binti ataondoka na uhakika wako na hataweza kufanya kinachobidi akifanye.

Kiingereza:

Kama yeye hatafanya ahadi katika msingi wa nini kinachotakiwa kwake kuhusiana na imani, atateseka zaidi ya mateso aliyoyazoea. Sitamruhusu atumie aina yeyote ya mateso ya kiakili. Ray, sitaruhusu akupe mateso ya kiakili. Sitamrhusu akutese. Itabidi aje kwa hiari yake. Hatafanya anachotaka kufanya kwa sababu ni binadamu mbinafsi aliyepagawa. Anatawaliwa na adui. Itabidi atoe ahadi kwa mahusiano yenu kwako la sivyo hata ruhusu kuingia katika Ulimwengu wako.

Kwa maana wewe una kazi ya kufanya na inabidi akubali kujiweka chini ya maisha yako ya Kiroho. Sitamkubalia akuingilie au akutawale wewe. Sitakubali hilo litokee lakini itabidi aelewe kutii kwa maana njia ya Mungu ni ngumu kama utaasi. Atajaribu kukulazimisha wewe kufikiri kuwa unaweza ukawa katika hali (iliyo kama yake au ovu zaidi) hiyo. Inabidi aache kukutawala kwani yeye pekee hana nguvu wala uwezo wa kustahimili pekee. Kwani ataanguka itakapo fika saa 6:30 asubuhi, kwani wakati huo hataweza kutawala tamaa yake kwako. Atapoteza uvumilivu wa tamaa yake ya kibinafsi na atakutamani sana kimwili. Atakutaka kimwili. Atakuita (kwa simu) kwa mambo fulani ambayo ni kisingizio lakini atakuwa amekuita kwa ajili ya tamaa kubwa mwili wake ulio nao. (Lugha isiyo eleweka?)

Nakupenda Ray. Nakupenda Ray, lakini kutembea katika nyayo za Kristu haijawahi kuwa rahisi. Najua una mapambano kuhusu uamuzi ambao lazima uufanye kulingana na Unabii unavyosema. Utapata nguvu utakapokuwa unahitaji nguvu, Ray. Ebu mwangalie Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Usiruhusu chochote na maanisha chochote kikuyumbishe Kushoto au Kulia. Mwangalie Yesu, Yesu wa Nazareti, kwa maani Yeye ndiye Njia na Barabara. Wewe uko chini ya ulinzi wetu, uongozi wetu.

Tunajua, tunajua ni nini utapitia lakini yote yatakuja kuwa mazuri. Utapokea zawadi. Usijali, Ray. Tayari umekwisha pokea zingine chache. Ni kwamba tu bado hujatambua. Utapokea mengine zaidi utakapo, kwa kadri utakavyokuwa unazidi kuimarika katika Imani, na katika maisha. Mwamini Yehova, Ray. Yehova, Baba, Mwumbaji wa Ulimwengu, uhatafanya makosa kama utamwamini Yehova. Utapata udhibitisho.

Sasa hivi, Unabii uliotuma umeanza kuwagusa watu waliousoma. Wengine wameanza kulemewa uzito wa ujumbe huo. Wengine wameanza kufurahia. Wengine wameanza kuwa na njaa ya kujua zaidi. Hivyo ebu niamini Mimi, Ray. Sisi hatutakuangusha wewe wala wewe hutatuangusha Sisi, hivyo ndivyo asemavyo Yehova.

Kwa mambo yale mengine ambayo nimekuwa nikikuahidi au nilikuahidi. Kwa maana Maneno Yangu siyo maneno yale yanayosema hiki lakini kisha yanafanya mengine. Najua moyo wako, kwa hiyo ebu mwangalie tu Mwanangu na Mimi nitakueleza lakufanya na wakati gani ufanye nini.

Nawe utajua kuwa ni Mimi. Kwa maana karama zingine nitakazokupa zitawashangaza watu kwa sababu mwisho unakuja. Inatubidi kuleta Mwili wa Kristu pamoja. Naenda kuutingisha naenda kuutikisa. Naenda kufanya lolote ambalo linahitajika lifanyike ili kuusafisha. Sitajali cheo ulicho nacho, jina, alama ambazo binadamu ameiweka kwenye Neno Langu. Kwa maana kama nilivyosema, Mimi nina Neno Mmoja. Mimi ni yule leo kama nilivyokuwa jana.

Binadamu anabadili Neno Langu ili akidhi matakwa yake na siku na saa karibu zimewadia. Najua unaogopa kuhusu nini Binadamu atasema na kwa njia atakayo sema kwa sababu huna elimu yakutosha ya Biblia ili ujitetee mwenyewe. Usijali Ray. Una nguvu za Roho Mtakatifu. Hakuna kitu ambacho Binadamu atasema au kufanya inaweza kupambana na Roho Mtakatifu. Najua unawakati mgumu kutafakari usemi huo kwa sababu hujawahi kusikia Nguvu za Roho Mtakatifu katika uweza huo na kwa njia hiyo, na itakushtua itakapo kujia.

Lakini wewe ni chombo changu na Mimi naweza kufanya lolote nitakalo na chombo changu na wewe uko tayari, kwa hiyo naenda kukutumia, Ray. Ebu ng’ang’ania tu kwenye mwamba ule, Mwanangu. Roho Mtakatifu atakuongoza na atakuonyeshea na atakupa amani na utulivu. Kwa maana mtu hawezi kumdhuru Mungu, ila hasira ya Mungu, Neno Langu lilonenwa, linafanya lolote linalosema litakwenda kufanya. Haijalishi kama ni kwa Rais, Mfalme, Mtawala au shetani mwenyewe. Mimi ndiyo Neno la Kwanza. Mimi ni Neno la Mwisho.

Najua unajaribu kwa uwezo wako wote. Nasikia kilio na machozi yako. Nasikia kuchanganyikiwa kwako, lakini Ray, unanguvu zaidi kuliko unavyo jidhania, laiti ungelijua hasara uliyoifanyia milki ya shetani. Kwa kupitia tu sala zako, kwa sala zako tu, lakini hiyo ni hadithi nyingine. Kwa sasa, kazi yako ni kupeleka Neno Langu kwa haraka iwezekanavyo. Nitakusaidia, na nitakuongoza kwa kupitia Roho Mtakatifu. Usifikirie lingine ila tu jinsi ya kumfurahisha Baba yako Yehova.

Kwa maana najua hutafuti zawadi za Mbinguni. Hutafuti kusifiwa na mtu. Unaangalia tu kunifurahisha Mimi. Kwa wazo hilo, kwa roho hiyo, ninaweza kukutumia wewe.

Kwa maana tatizo la kimwili lilikwisha kuwepo tokea enzi za kuanguka kwa Adam lakini wewe unaweza kufanya, Ray. Unaweza kuushinda mwili. Weka macho yako kwa Yesu Kristu wa Nazareti, na siyo kwa lile Binadamu analosema. Nitairudia tena. Kaza macho yako kwa Yesu Kristu wa Nazareti na siyo kwa sheria ya Binadamu kwa kutumia Jina Yesu Kristu. Kumbuka hilo Ray!

Sheria ya Yesu Kristu, iliyowekewa alama na Binadamu itakupeleka kwenye upande wa upotovu. Angalia unyofu na unyenyekevu upendo wa Yesu kwa jirani, kwa wagonjwa kwa waliopotea, kwa wale wenye mahitaji. Kumbuka zile sheria mbili amabazo Kristu alizisema kuwa ni za muhimu sana. Hayo ndiyo yote yaliyomuhimu yatakiwayo, Ray. Mfumo wa uongozi wa Kanisa umefungwa na umepotea UHALISI na katika MAANA. Wamepoteza lengo la kweli ya Yesu, sio wote ila wengi wao wamepoteza.

Kumbuka zile Sheria tatu na zile mbili ambazo ni za umuhimu mkubwa ambazo Yesu alikupa: "Mpende Baba yako Yehova kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, kwa Nafsi yako yote "na "Umpende jirani yako kama wewe unavyo taka wakupende. "Na sheria nyingine inayofuata: waambie "Yule ndugu, jirani yako ambaye hajawahi kumsikia Kristu na umwambie." Rahisi, Iliyonyooka, na ni ya Mmoja kwa mmoja. Tutaongea tena hivi karibuni; jaribu kukumbuka tu Maneno Yangu.

Amani na Upendo na utulivu iwe kwako, Mwanangu mdogo uwe imara, uwe mjasiri kwa maana mawe yatakuja lakini Mimi ni Ngao yako, Baba yako, pamoja na Mwanangu, na Roho Mtakatifu. Kumbuka hayo, mwangalie Yesu Kristu wa Nazareti. Nakupenda Ray, usisahau hilo kamwe. Huyu ni Baba yako Yehova, Muumbaji wa Mbinguni na Dunia, wa kwanza na wa Mwisho. 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.