96. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Juni 1992 saa 8:31 usiku wa siku ya Alhamisi katika lugha za Kihispaniola, Kiingereza, na lugha isiyo eleweka.
Kihispaniola:
Kwa sababu, kwa sababu. Maji yale niliyosema yatakuja, yatakuja. Kutakuja kuwapo wakati wa dhoruba na dhoruba itakuja kupasua na kutupa kila kitu kila mahala. Maji yatakuja kupaa juu na kushuka chini sana, kama milima. Ndiyo Reymundo. Ni ukweli. Sitawaambia tarehe kamili lakini iko karibu sana, kila kitu nilicho kuaambia wewe. (Lugha isiyoeleweka?) Safina. Safina. Safina.
Kiingereza:
Siku ile inakuja, ambayo imekwisha karibia kabisa, na bado ninyi hata hamuitambui. Watoto Wangu inabidi muamke. Inabidi muwaelimishe na kuwafahamisha watoto wenu; kilichoko mbele yenu, kwani janga kuu liko mbele yenu. Kwa maana saa itakapogonga saa 6 usiku, kwa kawaida ni wakati ambako siku mpya inapoanza. Siku mpya ya Dunia mpya na ya Mbingu mpya itakuja kama saa inapogonga saa sita ya usiku na unakuwa na siku mpya. Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati ule wa mwisho. Itakuja ghafla na haraka sana lakini kwa wale walio wazuri, walio wasafi moyoni, wale wa haki, waadilifu, wale ambao wameungama dhambi zao na kuziacha, itakuwa mwanzo wa utukufu.
Kwa maana watakuwa Mbinguni pamoja na Mimi, na Mwanangu, pamoja na Roho Mtakatifu kwa Milele na Milele bila wasiwasi, au mashaka yeyote. Miili yenu hiyo ya leo; haijui au haiwezi kutafakari juu ya jinsi ilivyokuishi katika Amani, Utulivu na upatanifu, na Ndugu zenu wa Kike na wa Kiume, na maumbile yote yale yanayowazunguka. Ni mastaajabu. Unaweza kuwazia, unaweza kufikiria na kudhania lakini ni zaidi sana ya mawanzo na dhana zenu zote. Ni ya ajabu kuliko mnachoweza kuotea kamwe. Hivyo ndivyo vinavyo wangojeeni Watakatifu wa Yesu kristu wa Nazareti.
Kwa maana Yeye ni NJIA. Yeye ni MLANGO WA WOKUVU WA MILELE. Kwa hiyo Watoto Wangu, tubuni dhambi zenu, mwangalieni Yesu Kristu wa Nazareti. Yesu Kristu wa Nazareti pekee, kumbukeni hilo. Mimi kamwe siwezi kutoa maelezo pungufu, mwangalieni Yesu Kristo wa Nazareti, twanga jambo hilo kwenye vichwa vyenu. Kwa maana Sheria za Binadamu, njia za Mwanadamu mwishoni; zitawaongoza kwenda kwenye shimo (la Jehanamu). Ninyi ombani, na muendelea kuomba. Roho Mtakatifu atawaonyesheeni, atawaongoza, atawaelekezeni. Yesu Kristu wa Nazareti ni Njia. Na wala siyo sheria za Binadamu, choma, piga chapa jambo hilo kwenye vichwa vyenu, kwenye akili zenu.
Yesu Kristu wa Nazareti anao ufunguo wa Ufalme, na wala siyo sheria ya Binadamu, maagizo ya Binadamu, mizigo ya Binadamu. Kwa vile tu wametumia Jina la Yesu, haiwafanyi wao kuwa wanyoofu na waadilifu. Roho Mtakatifu, Mshauri, Mpaji wa Ukweli yuko pale pamoja nawe pale lakini lazima ufanye maagano ya ahadi dhabiti na ya uhakika moyoni mwako, katika akili yako. Ni Lazima umhitaji Yesu kweli kweli na wala siyo kusema tu kwa mdomo.
Kwa maana Yeye ni Njia, na siyo sheria na taratibu ambazo haya Makanisa yaliyojiwekea au waliyo nayo. Makanisa mengine kwa kweli yamepotoka. Na mengine yanaendelea kuhangaika. Wana wazo zuri lakini yamejiwekea sheria na taratibu hizo juu yao. Wana nia njema lakini wamepoteza mtazamo na lengo. Haijalishi wanadai kusema kuwa wako huru kiasi gani. Hakuna hata mmoja wao aliyehuru hata mmoja. Inabidi mbadili uelekeo wenu macho yenu na masikio yenu myaelekeze kwa Yesu wa Nazareti. Sielewi nisema kwa namna gani zaidi na kwa njia ngapi hadi muelewe lakini Mimi nitaendelea kusema hadi hapo mtakapo nisikiliza.
Nasema hivyo hivyo kwa ninyi Wachungaji, kumbukeni Jina la Yesu Kristu wa Nazareti, ambaye ni Njia, na Barabara, ni Mlango, ni ufunguo wa Mbinguni; siyo sheria zenu, utaratibu wenu. Haijalishi bidii mlizo nazo au mnavyofanya kazi kwa umakini kiasi gani, au mnavyocheza. Wekeni umakini wenu kwa Yesu. Sheria ya Binadamu ni sheria ya Binadamu. Sheria ya Yesu ni Wokovu. Usijaribu, tafadhali usijaribu kufanya Biblia kuwa kitu cha kuhalalisha unavyotaka wewe uwe. Biblia ina majibu lakini inawabidi muisome kwa akili zilizo wazi, Mioyo iliyowazi. Mara unapomweka Mungu katika sanduku au boksi utakuwa umepotea.
Mnaweza kufanya mambo makuu zaidi kuliko akili zenu hizo ndogo zinavyoweza kutafakari. Kwa hiyo Watoto Wangu ebu tulieni, pumueni kwa nguvu na kisha mtafakari na kumwangalia Yesu wa Nazareti, Roho Mtakatifu atawaongozeni. Kumbukeni hilo! Huyu ni Baba yenu, Yehova. Muumbaji wa Mbingu, na Dunia, wa yale yote yaliyoko na yatakayo kuweko. Nawahitaji mje Mbinguni. Kweli Nawahitaji, lakini inabidi muwe waaminifu, Laiti mngeliweza kuona ninayoyaona Mimi kwenye Mioyo hiyo, Kwa kweli kamwe hamwezi kumdanganya Mwanangu au Mimi. Nitakuwa nawangojeeni ninyi nyote Mbinguni. Huyu ni Baba yenu. Nawapendeni Ninyi. Nawahusudu ninyi, lakini kumbukeni Mwanangu, Yesu Kristu. Mwananagu wa pekee ambaye alikufa kwa ajili yenu.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )