97. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Juni 1992 sa 4:04 asubuhi siku ya Alhamisi katika lugha ya Kihispaniola.
Gari. Gari la Nguruwe. Gari la Nguruwe. Nguruwe ana gari. Gari analolitumia kujua watu wanasemeje. Gari analolitumia kusikia watu wanasemeje. Gari analolitumia kujua ni nini kinatendeka nyuma ya milango na kuta kwa sababu anataka kujua kila kitu. Nguruwe anataka kujua kila kitu. Siku imefika ambako wewe hutaweza kusema chochote, na utakuwa na uwoga wa kusikia kinachotokea kwa sababu masikio ya Dunia yatakuwa kila mahali. Hutaweza kumwamini mtu yeyote. Kwa maana Kaka zako, Mama yako, Baba yako, Mke wako anaweza kukupeleka jela kama huta fikiri kama Nguruwe. Ni aibu gani, ni aibu.
Baba yako anafahamu kila kitu. Baba yako anafahamu nini kitatokea hata kabla hakijatokea. Niliviumba kila kitu; Wanangu wa Kiume na wa Kike, Nyota, Dunia, Mbingu, kila kitu unachokiona na unachokigusa. Kila kitu ni Changu kwa sababu kwa Neno Langu, Niliifanya pamoja na Mwanangu na Roho Mtakatifu. Wakati utakuja ambao utakuwa mgumu sana, utakuwa mgumu kiasi ambacho utafikiri "Kwanini nimezaliwa, kwa sababu maisha ni magumu sana. Nashindwa hata kupumua. Nashindwa kupumzika kwa sababu kuna watu nyuma yangu kila dakika. "
Siku hizo zitakapokuja nataka ninyi mkumbuke Baba yenu wa Mbinguni, pamoja na Roho Mtakatifu na Mwanangu Yesu Kristo. Kwa maana Neno langu linasema lililo la Haki, na Mimi sidanganyi, kila ninalosema litakuja kutokea. Nataka mkumbuke wakati huo kuwa Mimi nitakuwa pale daima. Mlango wa Mbinguni ni Mwanangu, Yesu. Inakubidi muelekeze mawazo yenu kwa Yesu. Yeye atawasaidia pamoja na Roho Mtakatifu kwa sababu kila kitu kitaenda vibaya.
Kisha nitamtuma Mwanangu. "Yeye atakwenda kusafisha kila kitu" Kumbuka hilo! Mwanangu Yesu ana nguvu. Ana Neno Langu la kufanya Ninalomwambia Yeye. Nitamwambia asafishe kila kitu kilicho kichafu. Nataka kitu kisafi
tu.Waliobakia naenda kuwa weka pamoja na shetani kwenye shimo kwa muda wote ambako kuna muda. Shimoni ndipo mahali watakapo enda kuteseka kwa muda wote ambako kuna muda. Watu wengi hawapendi kusikia hili! Hawaamini kuwa Mungu anaweza kufanya hivi! Lakini Angalia! Watu watakaoenda Shimoni ni wale ambao hawanitafuti Mimi. Waliomtafuta shetani, nao wamempata yeye. Watakatifu Wangu waliweka Akili zao kwa Mungu wao, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu.
Baba anafahamu kila kitu. Baba hataki uwe pale. Ana Upendo wa Ulimwengu wote, lakini wewe una uhuru wa kufanya lolote unalotaka kufanya. Sitakushawishi ubadilishe mawazo yako ya nini unataka kuchagua. Inabidi uchague wewe mwenyewe lakini Mimi nitakuambia ukweli. Nitakumbia ukweli mpaka uchoke kusikia ukweli huo, lakini ni ukweli.
Kama Mwanangu atakupeleka Mahala pale usije ukasema sikujua. Kwa maana Mimi ni Mungu wa kila kitu, na dakika hii ya sasa Ninakuambia ukweli. Roho Mtakatifu anaweka Cheche ile ndani ya Moyo wako. Sasa hivi! Kwa maana sitapenda uniambie kuwa sikujua. Katika shimo lile utateseka kwa muda wote ulioko. Kuna watu wengi ambao hawaamini hili. Ni aibu gani, kwa maana ni ukweli.
Shetani hapendi mjue ukweli, kwa maana kama hamwamini yeye atawala baadaye. Mna nafasi ya kuweka mawazo yenu kwa Mungu. Yule aliyeumba kila kitu kwa Neno Lake au kwa shetani ambaye alipeleka kila kitu alicho kigusa shimoni. Inabidi mchague. Kwa Upendo wa Moyo Wangu, Kwa Upendo wa Mwanangu, Yesu, Kwa Upendo wa Roho Mtakatifu, Tunawaambieni ukweli. Ninawaambieni kwa Neno ambalo, mtajua kuwa ni Ukweli.
Nawapendeni kwa Moyo Wangu wote. Nitaenda kulia kama nitawapoteza ninyi. Lakini kilicho cha ukweli ni ukweli. Hakuna kitakacho weza kubadilisha kilicho cha ukweli. Mimi, pamoja na Mwananagu, na Roho Mtakatifu, Sisi ni Ukweli. Hakuna kati yetu anayetaka kuwapelekeni ninyi kwenye mahala pale. Kila aliye Mbinguni anapenda mje pamoja Nasi Mbinguni. Ni shetani pekee ndiye anayetaka ninyi muishi naye, lakini hivyo ndivyo itakavyo kuwa.
Nisikilizeni! Nisikilizeni! Huyu ni Baba yenu. Baba yenu pamoja na Mwanawe, na Roho Mtakatifu, pamoja na Moyo wa Dunia, pamoja na Moyo wa kila kitu ambacho ni chema. Nawaambieni ukweli. Nisikilizeni Mimi! Nisikilizeni Mimi! Huyu ni Baba yenu.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )