98. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Juni 1992 sa 5:00 asubuhi katika kiingereza.
Nakupenda wewe. Ufundi/ustadi wa Upendo ni rahisi. Ustadi wa Upendo ni kujitolea kwa mwenzio mmoja kwa mmoja. Kutoa maisha yako yote kwa ajili ya mwenzio bila kufikiri hata mara mmoja, hiyo ndivyo Upendo ulivyo. Ni kutoa siku zote bila kutarajia kupokea chochote. Upendo ni kitu kilicho juu ya ubinafsi. Upendo hauwezi kuzuiliwa. Upendo unaenda kama mto unaokwenda kwa kasi. Upendo ni mwanzo wa kuzaliwa. Upendo na matendo ya kufanya Upendo si kitu cha kimwili.
Ni Maumbile ya Mwumbaji. Kwa maana Muumbaji ni Upendo halisi. Upendo unakusaidia ukue. Upendo unakufanya uwe imara. Upendo unakufanya uwe na busara. Upendo unakuleta karibu na Yehova, Yesu Kristo, kwa Roho Mtakatifu. Upendo ni kitu ambacho kila Mkristo anatakiwa ahangaikie, Upendo wa Kristo, Upendo wa Roho Mtakatifu, Upendo wa Baba, Yehova. Mungu Wenu siyo mgumu kufahamika. Mungu wenu ni mrahisi Kufahamika. Upendo uliorahisi. Hiyo siyo ngumu kufahamika. Inabidi ujisahau mwenyewe.
Najua watu wengi kamwe hawawezi kutafakari usemi huo ingawa huo ni usemi rahisi mno. Kila mtu anao. Kila mtu anaweza kuutumia. Kila mtu anauhitaji. Lakini kama hufanyi mazoea ya Upendo wako kwa binadamu mwenzie hata kwa vitu vile vitu vidogo, Nafsi yako kamwe haitatosheka. Siku zote utakuwa na ule uchu/tamaa kubwa sana ya kutaka kupata zaidi na zaidi kwa sababu kile unachotoa kwa mwenzio, katika njia ya Upendo, unakihitaji ili ikijaze Roho yako.
Ukimwendea au ukimtafuta Mwanangu Yesu Kristu kwa sababu ya Upendo, Naye atakuendea au atakutafuta kwa Upendo. Atakuendea wewe bila hata wewe kufahamu. Mimi pia nitakuendea wewe, naye Roho Mtakatifu atakuendea wewe. Sisi sote tumefungua mikono yetu ilituwaokee. Tunataka kuwa kumbatia. Tunataka kuwagusa. Tunataka tuwapende. Tunataka kuwa hudumia. Tunataka kuwalinda ninyi, wote kutoka katika lile Neno mmoja, Upendo.
Lakini inabidi mchague kutupenda Sisi au la. Neno lenyewe kwa msingi ni rahisi, lakini Binadamu amefanya maana ya maneno mengi kuwa magumu ambayo kimsingi ni marahisi sana. Kwa maana kama kweli mnataka kwenda Mbinguni, ninabidi mjue jinsi ya kupenda bila kutarajia chochote badala yake. Fanya hivyo kwa kuwa unataka kufanya hivyo, kwa sababu Kristu anakupenda wewe. Alikufa kwa ajili yako kwa sababu alikupenda kwa sababu ananipenda. Alikufa kwa ajili yenu. Nilimtuma Mwanangu afe kwa ajili yenu kwa sababu Niliwapendeni ninyi.
Ninaongea nanyi sasa hivi kwa sababu nina wapenda. Nataka msikie na muelewe Upendo uliopo kwenye mdomo Wangu. Kwa maana kama kuna kitu kitakacho waokoa ninyi, kitakuwa ni Upendo unaokuwa ndani ya Mioyo yenu, ambao unawasiliana Nami. Siyo kitu kile ambacho Mtu anakwambia, Wachungaji, Wanadheolojia, Wanasiasa. Mnavitambulisho vingi, na vyeo vingi lakini hilo siyo la maana.
La maana ni kunipenda Mimi zaidi ya kila kitu kingine. Na wewe utakuwa salama katika mateso na majaribu, katika heka heka za dunia hii. Kwa maana sitakuaja kamwe kama Unanipenda na Mimi nitakupenda. Tutaunda mnyororo kati yetu Mimi na wewe ambao kamwe hakuna kitakacho weza kuuvunja katika Ulimwengu huu. Kwa maana hata kama wewe utakimbia Mimi sitakuachia wewe kwa sababu nakupenda. Kwa sababu najua kuwa utarudi tu. Kwa sababu unanipenda.
Watoto Wangu ni rahisi. Ni rahisi sana. Mpenda Baba yako wa Mbinguni, Muumbaji wa Mbingu na Dunia, pamoja na Mwanangu Yesu Kristu wa Nazareti na Roho Mtakatifu. Hiyo pekee ndicho nilicho mwagiza Adamu na Eva, Mnipende tu na Mimi nitawapenda, lakini toka ule mwanguko, lakini tokea ule mwanguko wa Bustani ya Eden, kila kitu kimechanganywa, kimepinduliwa juu chini na yule adui wetu Mkuu shetani. Lakini Mimi naunda Bustani yangu Mpya ya Eden, Mbingu Yangu mpya, dunia Yangu mpya, na Ninaanza upya, kwa usafi. Imekaribia kabisa.
Natumaini Mnanisikiliza Mimi kwa moyo ulio wazi kwa sababu mioyo yenu imefungwa sana. Imefungwa sana. Itawatisha sana kama mngelijua tarehe. Lakini inakuja kwenye lile Neno la msingi lililotumika kwenye bustani ya Eden. "Upendo." Hilo Neno litasimikwa upya kama ilivyo kwa bustani ya Eden, katika miaka mingi iliyopita, wakati ulle ambako Wazazi wenu waliponikataa, lakini sikilizeni, haimaanishi kuwa yamekwisha. Ila ina maanisha kuwa tunakaribia hatua/ngazi mpya, Dunia Mpya, Bustani mpya.
Tayarisheni mioyo yenu na mpande kwenye Safina. Mkumbukeni Nuhu. Alinipenda Nami nilimpenda. Siku za Nuhu zimewadia kwa mara nyingine. Kumbukeni Ninawapenda. Hayo ni yote. Hicho ndicho cha maana. Kamwe usimwache Baba yako, Mfalme wako wa Wafalme, Bwana wako wa Mabwana, Yesu Kristu wa Nazareti, msimamiaji wa sheria. Kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, nitawaleteni ninyi nyumbani hivi karibuni. Hivi karibuni. Nawapendeni, msisahau hilo kamwe. Yehova anawapenda. Mungu wenu wa Milele.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )