99. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 18 Juni 1992 katika lugha ya Kihispaniola.
Ebu angalia! Najua unataka kunigusa Mimi, Reymundo. Najua unataka kufanya kile kilicho cha haki, lakini usijali kuhusu jinsi gani utaandika Unabii huu. Mimi niko pamoja nawe. Mkono wako ni Mkono Wangu. Midomo yako ni Midomo Yangu. Najua unataka kuyaandika maneno ya Unabii huu kwa usahihi, lakini unakuwa na wasiwasi juu ya kila kitu. Najua unalofikiria. Unafikiria kuwa usipoyaandika Maneno ya Unabii huu ninaokupa kwa usahihi kabisa, Mimi nitakuua pale pale mbele ya Komputa yako hiyo. Usiwe na wasi wasi kiasi hicho. Nataka Mimi nifanye kazi na wewe, lakini kama utakuwa unapigana na Mimi itazidi kuwa vigumu. Ebu jaribu kuvuta pumzi kwa nguvu, pumzika na uanze upya kwa maana unazidi kufanya kazi hii kuwa ngumu zaidi kwa jinsi hiyo, kuliko ilivyo. Mimi ninakuambia kile kilicho sawa sawa, lakini wewe una wasiwasi mwingi kuwa labda utakuja kukosea na kuwa hutaweza kufanya lolote.
Tazama Reymundo, Nina mambo mengi ya kukueleza wewe, na Mimi nataka uyaandike hayo kwa usahihi. Inakubidi uwe mvumilivu. Kwenda haraka au polepole siyo la maana. La maana nikuwa uwe na subira na unanisikiliza Mimi. Mimi nitaweka Neno Langu mawazoni mwako kwa njia ambayo Mimi nataka uiandike. Mimi najua. Najua kuwa wewe hujuia kutumia Kompyuta. Mimi najua. Najua kuwa hujui Kiingereza. Mimi najua. Najua kuwa hujui Kihispaniola. Hiyo ndiyo maana Mimi nataka kukutumia, kwa sababu hujui kitu, kama ungelikuwa unajua Mimi nisingelikutumia.
Kila mtu katika Dunia hii anadhania kuwa anajua kila kitu. Nitaenda kuwaonyeshea Utukufu Wangu, ya kuwa Mimi natumia kile ambacho kila mtu hataki. Na kwa hicho naendesha Dunia kwa kutumia watu ambao hakuna mtu anayedhani kuwa Mimi ningeliweza kuwatumia. Kila mtu anafukuzia kupata vitu vikubwa na Mimi na anangalia vile vitu vidogo, lakini hivyo ndivyo njia za Mungu zilivyo, pamoja na Mwanangu Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Mimi nataka uangalie mwili wako na roho yako katika mamabo madogo. Kwa njia hiyo, ukiomba Mimi nitakusikiliza. Kwa maana ukiviangalia vitu vidogo najua kuwa vitu vikubwa utaviangalia pia.
Reymundo, usijali, uwe na subira na uvumilivu, kwa maana Mimi nitaenda kukuambia mambo mengi. Hivi sasa, ni kwanza ndiyo tunaanza, na Mimi nataka nianze vizuri na wewe. Nataka kusahihisha mambo kabla wasiwasi wako hauja fanya ubadili mawazo yako. Kwa maana unaridhaa ya kufanya unalotaka kufanya. Huna haja ya kuandika lolote kama hupendi kufanya hivyo. Mimi silazimishi mtu yeyote afanye lolote asilopenda kufanya, lakini najua moyo wako. Unanikimbilia Mimi kwa kasi kubwa ambayo hujawahi kufanya hivyo katika maisha yako yote. Kwa maana moyo wako una njaa kali ya kutaka kunijua Mimi. Hukujua kuwa Mimi najua lakini Mimi najua kila kitu. Najua wewe una njaa ya kunijua Mimi. Nataka kukuonyeshea lakini inabidi uwe na subira.
Harakisha, amka na uanze tena lakini mwanzoni fanya pole pole kisha Mimi nitakuonyeshea jinsi ya kwenda kwa haraka zaidi. Nataka Mimi kufanya kazi na wewe, Sisi wawili. Tutakuwa wa wazo mmoja. Kwa maana inabidi tuwaambia Dunia kuhusu Neno Langu, Mungu yule aliyefanya kila kitu, Dunia, Nyota, Mbingu. Kwa maana Mwanangu ana amri ya nini Yeye afanye, na Malaika, pamoja na Mwanangu hivi sasa wako vitani mbinguni. Kila kitu kinaenda vizuri, lakini kuna vitu fulani fulani inabidi vitokee kwanza kabla vitu vingine havijatokea. Kila kitu kina mipangilio yake na kwa namna na njia ambayo itabidi itokee.
Kazi yako ni kusema Neno Langu kwa Dunia yote, lakini usijali, kwa maana uko Mikononi Mwangu. Nitakulinda wewe, familia yako, na ile familia mpya ambayo utakayo kuwa nayo. Kwa maana najua njaa uliyo nayo kwa ajili Yangu Mimi. Na Mimi nina njaa kwa ajili yako na Sisi wawili kwa msaada wako tutaokoa wengi. Je, umenisikia Mimi, Reymundo? Usijifanye kiziwi kwa sababu Mimi na wewe tuna kazi kubwa yakufanya. Najua umechoka sana na hujalala lakini ni jambo muhimu sana unayoyafanya.
Najua kuna wakati hudhanii hivyo, kwa sababu shetani anakutupia risasi yake na kuna wakati risasi hiyo inakupiga rohoni mwako, kwa maana silaha zako za kinga ulikuwa umevua. Najua inauma na wewe hujui nini la kufanya. Inakubidi utembee na silaha za Mungu kila dakika ya siku zote ambazo nitakuwa Mimi naongea nawe, kwa maana shetani anataka kukupiga kwa risasi zake. Unao Malaika wengi wanaokulinda. Najua huwaoni lakini wako pale. Kila dakika ya kila siku, kwa maana Maneno yangu lazima yasemwe kwa Watakatifu Wangu. Muda ni mfupi. Niliwaambia katika Biblia. Ningeliwajulisha na kuwalinda.
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )