1085. Occurrence given to Raymond Aguilera on 26 July 1997 at 2:53 PM.

The Anointing of Mount Zion:

I awoke early this morning, and the Lord instructed me to thoroughly wash myself, and to Anoint myself with the same bottled Olive Oil I purchased the day before. He instructed me to Anoint myself, on the forehead, hands, and both feet in the Name of the Father Jehovah, Jesus Christ, and the Holy Spirit. Then He told me everything would go well.  

The Oil I used.

(More Photographes)

This morning our tour group was going out early. We planned to cover the old town of Jerusalem. And we would end up going through Mount Zion. I prayed to myself the whole day for instructions on where, and how to Anoint Mount Zion. The Lord kept me uninformed the whole day. Since the Lord was not saying anything. I just figured He wanted Mount Zion Anointed the next day, since I had a free day to do what ever I wanted.  

Well, we were coming to the end of the Mount Zion area. And still the Lord was silent. I had my Anointing Oil in my pocket, and my camera ready to photograph the site. Then, when our tour guide said we were heading for the tour bus, I began to get nervous! For one thing, there weren’t many rocks around to gather, and there were many people around looking at everything! I had noticed what I thought was a rest room, and since Jerusalem was very hot, and we were all drinking a lot of water, I asked the tour guide if I could go to the rest room before I got on the bus. I was hoping the Lord would show me the Anointing Site with some stones before we left Mount Zion!

Anna the tour guide said, "Yes, if you really need to."

And for some reason, I handed her my camera, and left running for the rest room. I could not find the rest room I had seen earlier, and I hurriedly began to pray to the Lord for the location, and the day of the Anointing.

Then my brain went into gear, "You stupid person! Where is your camera? You dummy." I said to myself!

So I concluded, the next day was the day of the Anointing of Mount Zion. But I kept praying in the Name of the Father, the Son Jesus Christ, and the Holy Spirit - to tell me what to do! I knew everyone was on the bus by now, and waiting for me, so I headed back. Then, I saw a group of stones on the ground, on a clean and well kept area. Then I knew that was the place for the Anointing! I didn’t know how I knew, but I KNEW that was the Anointing site.

So quickly into my pocket my hand went. Out came the Anointing Oil, and within thirty seconds, the stones and ground was Anointed. I could not believe how fast the whole thing went! Then as I threw the empty bottle of Oil onto the Oiled stones and ground, I began to feel guilty. For I remembered, I did not have my camera to photograph the Anointed site. All that kept going through my mind was, all the months, money, and film for that moment in time, and it was lost. In my heart I felt so bad, and sad, and I guess my heart tried to apologize to the Lord for failing Him.

When I reached the bus people were still trying to settle in. And Anna looked at me and said, "That was quick!" 

But all that was on my mind was, that I had to rent a cab tomorrow, and come back with my camera. 

Once everyone got settled on the bus, Anna said she had a special treat for us, and asked if we wanted to see the Garden of Gethsemane. That location wasn’t on our tour. But she asked us if we want to go. Everyone said in a loud "Yes!" And off we went. I was happy to go to Gethsemane, but my mind was still back at Mount Zion.

The Garden of Gethsemane is a beautiful little place with olive trees, and a church on the grounds. Once our lecture on the church, and the grounds was over, we were release to explore. I felt so bad. I could of cried thinking about how stupid I was in giving my camera to Anna. I kept telling myself over and over - tomorrow I’ll get a cab, and come back, and photograph the Anointing site. I went inside the church and began to pray, and apologize to the Lord for failing him. Then during the prayer the Lord spoke and said, "No, you do not have to go back, and photograph the Anointing site. Not all things and locations were meant to be shown. Now, I release you - go, and enjoy yourself and have a good time the rest of the trip."  

The Garden of Gethsemane.

I Anointed Mount Zion on 26 July 1997 at 2:53 PM., and I finally realized it was the Lord who made me give Anna my camera. I will say it again, I will never understand why the Lord does certain things. (over)

1085. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 26 Julai 1997, saa 8:53 mchana.

Kuwekwa Wakfu Mlima Sayuni:

Mimi niliamka asubuhi na mapema asubuhi ya leo, na Bwana akaniagiza kuwa nikaoge vizuri mwili mzima, na kujiweka Wakfu kwa kujipaka Mafuta, kwa mafuta yale yale ambayo mimi niliyanunua jana yake. Aliniagiza nijiweke Wakfu kwa mafuta hayo usoni, mikononi, na kwenye miguu yangu yote miwili katika Jina la Baba Yehova, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu. Kisha Yeye akaniambia kuwa mambo mengine yote yataenda vizuri.

Mafuta niliyoyatumia.

(Picha zaidi)

Asubuhi hii; ziara ya kundi letu hilo ilikuwa inatakiwa kuondoka asubuhi na mapema. Sisi tulikuwa tumepanga kuzuri Mji Mkongwe wa Yerusalemu. Nasi tungeliishia kupitia Mlima Sayuni. Mimi niliomba kwa siku zima hiyo ilikupewa mwongozo wa ni wapi na ni kwa namna gani nipaweke Wakfu Mlima Sayuni. Bwana wala hakunijibu siku ile yote. Kwa vile Bwana alikuwa hajasema lolote; mimi nikaelewa kuwa Bwana labda alitaka Mlima Sayuni uwekwe Wakfu siku inayofuta; kwa vile Mimi bado nilikuwa na siku hiyo mmoja ya kufanya lolote ni pendalo kulifanya.

Naam, sisi tulikuwa ndiyo tunafikia kwenye mwisho wa safari yetu hiyo ya kuutembelea eneo la Mlima Sayuni. Na bado Bwana alikuwa yuko kimya. Mimi nilikuwa na Mafuta yangu tayari ya kuweka Wakfu kwenye eneo nikalo elekezwa mfuko mwangu. Na kamera yangu ilikuwa iko tayari; ili kupiga eneo hilo la kuwekwa Wakfu. Kisha pale kiongozi wetu wa safari aliposema sasa tunarudi kwenye basi letu; mimi mara nikaanza kuingiwa na wasiwasi! Kwa uhakika kitu cha kwanza ni kuwa; pale hapakuwa na mawe mengi ya yaliyokusanywa pamoja; na pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiangalia hili na lile! Mimi mara nikaona kitu kilichokuwa kinaonekana kama sehemu ya kujisaidia pale, na kwa vile Yerusalemu kwa wakati huo ilikuwa na joto kali; nasi sote kwa vile tulikuwa tukinywa maji mengi, mimi nikamwomba ruhusa yule kiongozi wetu ya kwenda msalani kabla ya kupanda kwenye basi.  Mimi nilikuwa natumaini kuwa labda Bwana angelinionyeshea eneo ambalo Yeye anataka liwekwe Wakfu, ambayo ina rundo la mawe kabla ya kutoka hapo kwenye Mlima Sayuni!

Anna ambaye ni kiongozi wa msafara wetu huo akasema, "Sawa, kama umeshindwa kuvumilia."

Na kwa namna ambaye mimi sifahamu, mimi mara nilimpa huyo kiongozi kamera yangu, na kisha nikaondoka kutoka hapo mbio kuelekea msalani. Mimi nikashindwa kuona msala ule nilio kuwa nimeuona hapo awali, nami haraka haraka nikaanza kumwomba Bwana ili anionyeshee ni wapi anataka nipaweke Wakfu, au labda anieleze ni siku ipi aliyochugua ya kupaweka eneo hilo Wakfu.

Kisha akili yangu mara ikaanza kuamka, "Wewe mjinga! Kamera yako iko wapi? Wewe juha." nikaanza kujiambia mwenyewe!

Kwa hiyo kwa vile sipati jibu, mimi nikafikia kwenye uamuzi wa kuwa siku inayofuta ya kuweka Wakfu Mlima Sayuni itakuwa kesho yake. Lakini mimi niliendelea kuomba katika Jina la Baba, Mwanaye Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu – ili nipate kuambiwa ni fanye nini! Mimi nilijua kuwa kila mtu alikuwa yuko kwenye basi tayari na kuwa labda wakati huo watakuwa wananingojea mimi tu, kwa hiyo mimi nikaamua kurudi. Kisha, mimi niliona rundo la mawe ardhini, katika eneo lililokuwa safi na linalotunzwa vizuri. Kisha mimi nikajua kuwa hiyo ndiyo sehemu ninayo paswa kupaweka Wakfu! Mimi sielewi jinsi nilivyoijua, lakini MIMI NILIJUA kuwa ndiyo eneo haswa ninalopaswa kupaweka Wakfu.

Kwa hiyo mimi kwa haraka nikaingiza mkono wangu mfukoni na kutoa ile chupa ya Mafuta ili kupaweka pale Wakfu. Na mara chupa hiyo ya mafuta ilipotoka na katika muda wa kiasi cha sekunde thelathini tu, yale mawe pamoja na ardhi ile ikawa imekwisha kuwekwa wakfu. Mimi sikuweza kuamini jinsi haya mambo yalivyo fanyika katika muda mfupi kiasi hicho! Kisha mara nilipoitupa ile chupa tupu ya mafuta kwenye rundo hilo la mawe hayo yaliyo wekwa Wakfu pamoja na ardhi yake, mimi mara nikaanza kujisikia kuwa nimefanya makosa. Kwa maana mimi nilikumbuka kuwa, mimi nilikuwa sijachukua kamera yangu ili kupiga picha ya eneo hilo lililowekwa Wakfu. Yote yaliyokuwa yanaendelea katika mawazo yangu ilikuwa ni kuwa muda wa miezi hii yote ya matayarisho, fedha pamoja na filamu kwa ajili ya wakati huo muhimu; yote yamepotea. Katika moyo wangu mimi nikaanza kujisikia vibaya, nadhani moyo wangu ulijaribu kuomba msamaha kwa Bwana kwa kumwangusha Yeye.

Mimi niliporudi kwenye basi letu lile nilikuta watu ndiyo kwanza wanajaribu kukaa kwenye viti vyao. Naye Anna akaniangalia mimi na kusema, "Hiyo ilikuwa ni haraka kweli kweli!" 

Lakini yote yale yaliyo kuwa yanaenda katika mawazo yangu ilikuwa nirudi kwa teksi hapo kesho yake pamoja na kamera yangu ili nikapige picha eneo hilo.

Mara kila mtu alipotulia kwenye vitu vyao, Anna ambaye ni kiongozi wa safari yetu hiyo, akasema anataka kutupa zawadi, na kuuliza ni wangapi wanataka kwenda kuona Bustani ya Gethsemane. Hiyo eneo halikuwa kwenye ratiba yetu. Lakini yeye akatuuliza kama tunataka kwenda. Kila mtu akasema kwa sauti kubwa "Ndiyo!" Na mara tukaondoka. Mimi nilifurahi kwenda kwenye bustani hiyo ya Gethsemane, lakini akili yangu yote ilikuwa bado iko kule kwenye Mlima Sayuni.

Bustani ya Getsemani ni mahali padogo lakini pazuri sana, iliyokuwa na miti ya mizeituni, ikiwa na kanisa ndani yake. Mara maelezo ya kuhusu kanisa na eneo hilo yalipoisha kutolewa, sisi tuliachiwa tuangalie eneo hilo. Mimi nilijisikia vibaya sana. Nilitaka hata kulia kwa kufikiria jinsi nilivyokuwa mjinga kwa kumwachia Anna kamera yangu. Mimi nikawa naendelea kjiambia mwenyewe tena na tena kuwa – kesho mimi nitachukua teksi na kurudi mahala pale nilipo paweka Wakfu; ili nikapapige picha. Mimi niliingia ndani ya Kanisa lile na kuanza kusali, na kumwomba Bwana msamaha kwa ajili ya kumwangusha Yeye. Kisha wakati wa maombi hayo Bwana akasema, "Hapana, wewe huna haja ya kurudi tena ili kupiga picha ya mahala pale ulipopaweka Wakfu. Siyo kila kitu na kila sehemu uliyo weka Wakfu inatakiwa kuonyeshwa. Sasa Mimi nakuachia huru ukajifurahishe na uwe na wakati mzuri kwa muda wote wa safari hii."  

Bustani ya Getsemani.

Mimi niliuweka wakfu Mlima zioni tarehe 26 Julai 1997 saa 8:53 Mchana, nami nikatambua kuwa ilikuwa ni Bwana aliyenifanya nimpe Ana kamera yangu. Mimi nasema tena, mimi kamwe sitakaa kufahamu ni kwa nini Bwana anafanya mambo mengine (kwa namna isiyotegemewa). (Mwisho).

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.