1122. Occurrence given to Raymond Aguilera on 14 November 1997 at 8:30 PM.

For the past two weeks, I have had many people call and write for prayers. I also noticed, that I would cry during most of these prayers. Most of the time I did not even realize that I was crying until well into the prayer. It seemed like they were empathy type of prayers, where your body would physically get into the prayer and cry.

Well - Friday night Carl, a friend of mine, asked me if I wanted to go to hear a well known prophet speak in San Jose. I told him yes, and then I proceeded to his house. I noticed the heavy traffic, and mentioned it to Carl. We decided to stay home and pray, and have Communion.

Occurrence/Vision:

During our prayers is when this occurrence/vision happened. Most of the time; I feel like the biggest sinner in the world. I do not know why the Lord does this to me, when I least expect it!

This experience was so real in the spirit, I cannot fully explain it in words. But during prayer before Communion, the Lord gave me the "HONOR AND PRIVILEGE", to see Him in the Spirit, during the taking the Holy Wine with His Disciples at the Last Supper in the upper room.

As I looked at the Lord, I could see Him from about the wrist up, but He looked like He was sitting on the floor, but I am not sure. I knew beyond a shadow of a doubt, that it was Him. But, His Body had no shape; you could identify. I know, I sound strange, and not making any sense, but I knew exactly - who He was, and what He was going doing. I also knew that it was the Last Supper of the Lord, and the world's first Communion service given directly by the Lord. This all sounds very strange doesn't it!

What was shown to me was the moment after the taking of the Bread (His Body), and just before the Wine (His Blood) was given out. How - can I explain this without sounding like a crazy man! I was seeing Jesus Christ from the wrist up, but He had no identifiable features in the flesh, in His Face or Body, but I could see His Face CLEARLY in the Spirit. But as I looked at His Spiritual Face, it looked so quite, calm, peaceful, and tranquil, but yet I could sense tears in His Face. As I watched Him, He slowly and patiently took a long deep look at each of the Disciples before He passed the Wine. It seemed to me that He was looking down deeply into everyone soul. It also seem to me - that this look showed what each Disciple was going to do and suffer for His Name sake. Maybe that was why He had that tone of Tears in His eyes too. The whole place became TOTALLY QUIET; and no one made any sound as if the HOLY SPIRIT was filling the whole room as they watched.

All that kept running through my mind was; "I HAVE NO BUSINESS HERE; seeing such a HOLY MOMENT!" I began to feel so dirty and undeserving seeing this happen. I wish, I could explain all of this in words, but I cannot. These kinds of experiences make me wonder, "WHY me!!!!" For reading it in the Bible was enough, and I believed. That was enough for me! But yet your spirit gets so hungry for a personal closeness to the Lord, that it never gets enough.

It was like; when not a word is spoken, and you see someone with love or pain in his body, and no one has to tell you, but the both of you know what is going on inside the person. I could sense the Lord's Eyes search deeply into the enter depths of each Disciple with the Love of His Heart. Wow, this was great! This whole occurrence lasted about 10 seconds, but it seemed like 10 to 15 minutes.

The hair on my arms started to rise, and I wanted to cry!! Why - am I such a cry baby, when it comes to these kinds of things? All I wanted to do was run and run as fast as I could. Does that sound like a holy man seeking the Lord? Well - I could not type this up until today. I could not even shave my face or take a shower for about three days. I found myself out of focus every time I tried to type it up. But where can a person run or hide from the Lord? And why would they want too! I am WAY OVER my head and body in my Christian Spiritual walk again. I am beginning to believe our bodies are NOT MADE to experience some things in the SPIRIT! For it really breaks us!

I kept asking myself, "WHY", is the Lord doing this to me? I was in such "Awa", at being able to see this occurrence, and at the same time my mind was saying, "I am NOT worthy to see this! Why, is the Lord doing this to me!!! (over)

Vision:

Then I saw the Lord weeping, and I wondered if that was why I had been crying the past several weeks.

Vision:

Then the Lord showed me a nuclear explosion of some sort. Then this pillar of fire came down from Heaven, which extended miles and miles from the sky. It was cylindrical in shape, and the flames circled in this cylindrical shape. And as I watched this nuclear explosion; this pillar of fire went around the perimeter of the nuclear blast. Then the Lord informed me that was why He was crying. (over)

 

1122. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 14 Novemba 1997, saa 2:30 usiku.

Kwa muda wa wiki mbili zilizopita, mimi nimekuwa nikipata simu na Barua kutoka kwa watu mbali mbali kwa ajili ya kutaka niwaombee. Mimi pia nimeona kuwa wakati wa maombi hayo nimekuwa nikilia kwa sehemu kubwa ya maombi hayo. Wakati mwingi nimekuwa sitambui kuwa mimi nimekuwa nikilia hadi ninapo karibia kumaliza maombi hayo. Ilikuwa inaonekana kama maombi ya aina ya huruma hivi, hali ambayo inafanya mwili wako wote unaingia kwenye maombi na kulia.

Naam – siku ya Ijumaa usiku rafiki yangu Carl, akanikaribisha kwenda naye kumsikiliza nabii maarufu kule San Jose. Mimi nilimwambia ndiyo, na kisha mimi nikaelekea kwenda kwenye nyumba yake. Mimi nikaona magari yalikuwa mengi sana, na kumweleza Carl. Basi sisi tukaamua kubaki hapo nyumbani kwa Carl na kufanya maombi na kupokea Komunio.

Matukio/Maono:

Wakati wa maombi yetu hayo, ndipo Matukio/maono hayo yalitokea. Wakati wote huo; mimi nilikuwa najisikia kuwa mtenda dhambi mkubwa sana katika dunia hii. Mimi sijui ni kwa nini Bwana ananifanyia hayo, wakati ambako mimi nilikuwa wala sitarajii hayo!

Tukio hilo lilikuwa ni kama kitu kilichokuwa halisi sana katika ulimwengu wa Kiroho; kiasi ambacho mimi nashindwa kuieleza kinaganaga kwa maneno. Lakini wakati wa maombi kabla ya Kumunio, Bwana alinipa "HESHIMA NA BAHATI", ya kumwona Yeye Bwana katika ulimwengu wa Kiroho, wakati ule Yeye na Mitume wake walipokuwa wanashiriki kunywa Divai Takatifu (ambaye ni Damu Yake) pale kwenye Karamu ya Mwisho kule (Yerusalemu) kwenye chumba cha Ghorofani.

Nilivyo mwangalia Bwana, nilikuwa naweza kumwona Yeye kuanzia kwenye Kiganja Chake cha Mkono kwenda juu, lakini alikuwa anaonekana kama amekaa chini kwenye sakafu, lakini mimi sina uhakika. Mimi nilijua kwa uhakika kabisa yakuwa alikuwa ni yeye. Lakini Mwili wake ulikuwa hauna chcochote cha kumtambulisha Yeye. Najua nasikika kuwa wa ajabu, na ya kuwa si eleweki, lakini mimi nilijua kwa uhakika – ya kuwa Yeye alikuwa ni Nani, na kile alichokuwa anakifanya. Mimi pia nilijua kuwa ilikuwa ni Karamu ile ya Mwisho ya Bwana, na ya kuwa ilikuwa wakati ule wa sherehe ya Misa ya Komunio ya Kwanza ya dunia ambayo ili fanywa na Bwana Mwenyewe.  Haya yote najua yana sikika kuwa mambo ya kigeni ama sivyo!

Nilicho onyeshewa kilikuwa ni yale ya wakati ule baada ya kusherehekea ule Mkate Mtakatifu (Mwili Wake), na kabla tu ya Divai (Damu Yake) kutolewa. Sasa – sijui nielezeje haya bila ya kuonekana kama mwenda wazimu! Mimi nilikuwa na mwona Yesu Kristo kuanzia kwenye Kiganja kwenda juu, lakini hakuna lolote la kumtambulisha katika mwili, katika Uso Wake au Mwili Wake, lakini mimi hapo hapo nilikuwa naweza kuuona Uso Wake kwa UWAZI katika Ulimwengu wa Kiroho. Nilipo kuwa ninauangalia Uso wake wa Kiroho, ulikuwa unaonekana kutulia sana, wenye amani, na utulivu, lakini bado nilikuwa naweza kuhisi Machozi Usoni Mwake. Nikiwa bado namwangalia Yeye pole pole aliwatazama Mitume wake mmoja mmoja na kwa uvumilivu mkubwa kabla hajapitisha kikombe kile cha Mvinyo. Ilikuwa inaonekana kwangu kama Yeye alikuwa anaangalia kila nafsi ya wale Mitume Wake. Ilikuwa pia inaonekana kwangu kuwa – kule kuangalia ilikuwa inaonyesha kila Mtume kazi anayoenda kuifanya na jinsi atakavyo enda kutesekea kwa ajili ya Jina Lake. Labda hiyo ndiyo sababu alikuwa na Majonzi na Machozi hayo Machoni Mwake pia. Mahala pale pote PALIKUWA KIMYA KABISA; na hapa kuwa na yeyote aliyeweza kutoa sauti au hata kujikuna kana kwamba ROHO MTAKATIFU alikuwa anajaza chumba chote kile huku wao wakiwa wanaangalia.

Yote yale yaliyo kuwa yanapita kwenye mawazo yangu yalikuwa ni; "MIMI SISTAHILI KUWA HAPA; na kuuona WAKATI HUO MTAKATIFU!" Mimi nilianza kujisikia kuwa mtu nliyekuwa mchafu sana na ambaye hastahili kuona haya yote yakiwa yanatokea. Laiti kama ningeliweza kueleza hayo yote katika maneno lakini nashindwa. Matukio kama haya yananifanya mimi kujiuliza, “KWANINI IWE MIMI!!!!” Kwa maana kule kuisoma ndani ya Biblia ilikuwa inanitosha, nami nina amini. Hiyo pekee ilikuwa inanitosha mimi. Lakini bado roho yako inakuwa na njaa sana kwa ajili ya kutaka kuwa karibu na Bwana kibinafsi, na ambayo haiwi karibu ya kutosha.

Ilikuwa kama wakati ambako hakuna neno lolote linalo semwa, na unamwona mtu akiwa na upendo au maumivu mwilini mwake, nawe unakuwa huna haja ya kuambiwa lakini unajua kwa uhakika, nanyi wawili mnajua kunaendelea nini ndani ya mtu huyo. Mimi nilikuwa na hisi kuwa Macho yake yakichunguza undani wa kila Mtume; kwa Upendo wa Moyo Wake. Loo hili lilikuwa kubwa! Tukio hili lote ilidumu kwa sekunde 10 hivi, lakini lilikuwa linaonekana kama kitu kilicho dumu kwa dakika 10 hadi 15 hivi.

Malaika za nywele kwenye Mikono yangu zikaanza kusimama na kusisimka, nami nikataka kulia!! Kwanini – hivi mimi nakuwa kama mtoto mdogo, wakati ninapo kumbana na mambo kama hyo? Yote niliyotaka kuyafanya ilikuwa ni kwenda kukimbia kwa kasi iwezekanavyo. Hivi hiyo inasikika kama tabia ya mtu mtakatifu anaye mtafuta Mungu? Naam – nilishindwa kuandika tukio hili hadi leo. Nilishindwa hata kunyoa ndevu zangu au hata kuoga kwa muda wa siku tatu. Mimi nilijikuta kama mtu aliye pumbazika na kukosa mwelekeo au tuseme nilikosa umakini kila mara nilipojaribu kuandika habari hii. Lakini ni wapi ambapo binadamu anaweza kwenda kukimbia na kujificha kutoka kwa Bwana? Na ni kwa nini watake hivyo! Mimi NIMECHANGANYIKIWA kichwani na mwilini katika safari yangu ya kiroho katika maisha ya kikristo. Mimi naanza kuamini kuwa miili yetu HAIKUFANYWA kuhisi mambo fulani fulani katika Ulimwengu wa KIROHO! Kwa maana kwa kweli ina ivunja vunja miili yetu hiyo!

Mimi nikawa ninajiuliza “NI KWANINI”, Bwana ananifanyia hivi? Mimi nilikuwa na “mstuko” kwa kule kuona tukio hilo na wakati huo huo akili yangu ilikuwa inasema, "Mimi SISTAHILI kuona haya! Kwanini Bwana ananifanyia haya!!! (Mwisho).

Maono:

Kisha mimi nikamwona Bwana akiwa analia, nami nikaanza kuwaza kama hiyo ndiyo maana mimi nimekuwa nikilia kwa muda huo wote wa wiki kadhaa zilizopita.

Maono:

Kisha Bwana akanionyeshea mlipuko wa Kinuklia wa aina fulani. Kisha mnara fulani wa moto ukaja chini kutoka mbinguni, ambao ulienda kwa maili na maili kutoka angani au mawinguni juu. Ilikuwa na sura ya mviringo kama tanki, nao moto ulikuwa unazungukia mnara huo wenye sura ya mviringo; ulio kwenda juu kama. Na wakati nikiwa ninautazama mlipuko huo wa kinuklia; mnara huo wa moto ulienda na kuzunguka kwenye eneo hilo la mlipuko. Kisha Bwana akanieleza kuwa hiyo ndiyo sababu ya Yeye kulia. (Mwisho).

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.