|
1206. Occurrence given to Raymond Aguilera on 10 September 1998 at 2 AM. I went to bed about 1:35AM. this morning and during my prayers I got attacked in the spirit. I had just finished praying when without warning my body became paralyzed. The only thing that I could use was my voice. As soon as I realized it was a spiritual attack my prayer language began to speak out, in my warfare tongue! This warfare took me into this spiritual world and I could sense this enormous battle in the spirit. But at the same time I kept trying to move my physical body in this world, but without success. At one point, I sensed that the prayer language fought off the spiritual attack for it subsided, but then I was hit again with this counter attack which was more pointed. Then my prayer language just went crazy with some strange sounds that sounded like a machine gun. Then the prayer language changed again into short but direct sounds that sounded like the prayer language was sending out powerful bombs into the spiritual world. Finally my body came back to normal and I went to sleep. (over)
|
1206. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 10 Septemba 1998, saa 8 usiku. Mimi nilienda kulala wakati wa kama wa saa 7:35 za usiku wa manane na wakati wa maombi; mimi nilipatwa na mashambulizi katika ulimwengu wa kiroho. Mimi nilikuwa ndiyo kwanza nilikuwa nimemaliza kuomba, ndipo mara kwa ghafla mwili wangu ulianza kupooza na kushindwa kujisogeza. Kile pekee nilichokuwa naweza kukitumia kilikuwa ni sauti yangu. Mara nilipotambua kuwa ilikuwa ni mapambano ya kiroho; kwa ghafla lugha yangu ya mapambano mara ikaanza kusema, katika lugha au ndimi ya mapambano! Mapambano hayo ya kiroho yalinipeleka kwenye ulimwengu wa kiroho, nami nikawa naweza kuhisi mapambano haya makubwa sana katika ulimwengu wa kiroho. Lakini wakati huo huo; nilikuwa najaribu kusogeza mwili wangu katika ulimwengu huu wa mwili, lakini bila ya mafanikio. Kuna wakati mimi nilihisi kuwa ile lugha yangu ya mapambano ili weza kufukuza mashambulizo hayo ya kiroho, kwani yalianza kupungua kasi, lakini kisha mara nikaanza kushambuliwa tena kwa mara nyingine; ambayo yalikuwa ni makali zaidi. Kisha sauti ya maombi yangu ya kilugha ya mapambano ikaenda kwa kasi kubwa sana; ikitoa sauti kama ya bunduki ya rashasha. Kisha sauti ya maombi yangu ya lugha ikabadilika na kuanza kutoa sauti ya milio mifupi fupi mikali; ya mmoja kwa mmoja kana kwamba sauti hiyo ya lugha ya maombi ilikuwa inatupa mabomu mazito mazito katika ulimwengu wa kiroho. Mwishoni mwili wangu ulirudi hali yake ya kawaida nami nikaendelea kulala kama kawaida. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )