1212. Occurrence and Visions given to Raymond on 6 October 1998 at 1:00 PM.

I was working on the computer and suddenly I became very sleepy. Usually this means I am tired or the Lord wants to speak to me. So I laid down and began to pray. I figured if the Lord wanted to say something He would or I would fall asleep praying and nothing would happen. Well, in this tired sleep state while praying I began to see many visions.

Vision:

I saw these enormous wings open up in the sky. Each wing looked like it was miles wide. In front of these large wings, I could a white horse with someone riding it, and moving toward me. As I looked closer at these wings, they looked like eagles wing’s. There seemed to be an enormous eagle flying behind this rider, and behind this eagle there were these enormous clouds in the sky. I could see many, many people standing on these large blooming clouds. It was very beautiful. These beautiful clouds reminded me of some of those old renaissance printers who painted those blossoming expanding colorful clouds with angelic angels coming from the sky. It was a beautiful sight.

Occurrence:

So I began pray some more and during this prayer time my left hand started lifting into the air off the bed surface. In the Spirit, I could see the Lord’s Hand reaching down from heaven and take hold of my left wrist. I do not know how to explain it other than I could see this from outer space. I was seeing this in the spirit, the Lord was holding my wrist as if I were outside my body and watching the Lord and I hold hands. Sounds crazy doesn’t it! Then I could see the planet earth fall away from under my feet. Leaving me stationary holding onto the Lord’s Hand with my left hand. I could see the planet moving away from under my feet and going on it’s orbit around the sun. It was as if I was stopped at that point in space and time and the earth kept moving around the sun. As I looked down at my feet the earth just got smaller and smaller until I could not see it anymore. I did not understand, but I was left in space holding onto the Lord’s Hand.

Then I sensed being taken into…, I do not know - this higher realm, heaven maybe (outside the galaxy). I could see many spirits which looked like white clouds and they could fly. I saw many, many, many of these white clouds or spirits move about. This was very very strange. This place did not seem to have a ground as we know it.

Vision:

Then I saw this enormous Light coming over and through these moving white clouds or spirits. This mountain of White Light seems to cover these spirits or white clouds as it moves towards me from my right side. I could also see some kind turbulence with these spirits as the White Light moved over them. I believe this was Jehovah moving over Heaven. I also could sense this enormous Power. Then when the Light passed by me, my left hand came down to my side on the top of the bed.

Vision:

Then in the spirit, I saw myself with wrist bands around each wrist. As I watched myself, I could see the wrist bands move up both of my arms by themselves. Then I saw something I cannot explain. These two wrist bands moved up my arms through my upper chest across to the opposite arm (they went through my chest and through each other) and exchanged arms and moved down to the wrists.

Vision:

I saw an Adam’s apple inside of someone’s mouth with the sides of the mouth having some kind of layers of skin that look like flames.

Vision:

Then the mouth image changes into a Caucasian woman’s birth canal and she was giving birth and delivering a black baby. I saw the black head of the baby being delivered.

Vision:

The next image was of a serpent, that closed it’s mouth very fast onto these dark clouds. It looks almost like a dragon with smoke coming from the sides of it’s mouth or like it ate something.

Vision:

Then I saw a vision of some kind of naval ship, maybe a destroyer, moving very rapidly over the water.

Vision:

Still in the spirit, I saw the inside of a volcano and saw everything that goes with that type of sight. I did not sense the heat though and I cannot explain it.

Vision:

I see the silhouette of mountains or large rocks, but the sky is so unusual in color. The sky looks violet with colors of dark blackish purple, but transparent in color.

Vision:

Then I saw an image of a fox with a black eye. His right eye had been blacken. (over)

 

1212. Matukio na maono aliyopewa Raymond tarehe 6 Oktoba 1998, saa 7:00 mchana.

Mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye kompyuta yangu na mara nikaanza kusinzia. Kwa kawaida hiyo inamaanisha kuwa mimi nimechoka au Bwana anataka kuzungumza na mimi. Kwa hiyo mimi nikajilaza na kuanza kuomba. Nilifanya hivyo nikiwazia kuwa aidha kama Bwana anataka kuzungumza na mimi atasema au kama nimechoka nitashikwa na usingizi huku nikiwa ninasali (na bila kutokea chochote). Naam, nikiwa katika hali hiyo ya uchovu na huku nikiwa ninaomba mimi mara nikaanza kuona maono mengi.

Maono:

Mimi niliona mabawa fulani makubwa sana yakijifungua kule angani. Kila bawa lilikuwa linaonekana kana kwamba lilikuwa na upana wa maili kadha. Mbele ya mabawa hayo makubwa; mimi nilikuwa naweza kumwona farasi fulani mweupe pamoja na mpanda farasi wake; akiwa ananijia mimi. Nilivyozidi kuyaangalia mabawa hayo zaidi, niliona kuwa yalikuwa yanaonekana kama mabawa ya tai. Hivyo inaonekana kuwa kulikuwa na tai fulani mkubwa sana aliyekuwa akiruka nyuma ya huyo mpanda farasi, na nyuma ya tai huyo kulikuwa na mawingu fulani makubwa angani. Mimi nilikuwa naweza kuona watu wengi wengi sana wakiwa wamesimama juu ya mawingu hayo makubwa na yaliyokuwa yanachanua. Yalikuwa ni mazuri sana sana. Mawingu haya mazuri yalinikumbusha mimi michoro ya picha zile za zamani (ya kwenye makanisa ya kale ya nyakati za ‘renaissance’) ambayo ilikuwa inaonyesha mawingu yaliyokuwa yanachanua na kupanuka na yaliyokuwa na rangi nzuri nzuri na juu yake kukiwa na malaika walio kuwa wanatoka angani. Ilikuwa ni kitu kilicho kuwa kinapendeza sana machoni.  

Matukio:

Kwa hiyo mimi nilianza kuomba zaidi, na wakati wa maombi hayo mara mkono wangu wa kushoto ulianza kunyanyuka kwenda juu hewani kutoka juu ya kitanda. Katika Ulimwengu wa Ki-Roho mimi nilikuwa naweza kuona Mkono wa Bwana ukija chini kutoka Mbinguni na kushika mkono wangu wa kushoto. Mimi hata sijui jinsi ya kuyaeleza hayo zaidi ya kusema kuwa mimi nilikuwa ninayaona hayo kutoka kwenye anga za juu. Mimi nilikuwa naona hayo katika ulimwengu wa kiroho, Bwana alikuwa ameushikilia mkono wangu kana kwamba mimi nilikuwa niko nje ya mwili wangu na huku nikiwa naona Bwana na mimi tukiwa tumeshikana mikono. Ina sikika kama jambo la kufikirika na ya uwenda wazimu siyo! Kisha nikaona sayari ya dunia ikiwa inaondoka kutoka chini ya miguu yangu. Mimi niliachwa nikiwa nimeganda hapo hapo nikiwa nimeushikilia Mkono wa Bwana kwa mkono wangu wa kushoto. Mimi nilikuwa naweza kuona sayari ya dunia yetu hii ikiwa inaenda zake kutoka chini ya miguu yangu na kuenedelea na safari yake ya kawaida ya kuizunguka jua. Ilikuwa inaonekana kama mimi nilisimamishwa angani sehemu ile na wakati ule; na huku dunia ikiwa inaendelea na safari yake ya kuizunguka dunia. Nilivyo angalia kule chini kwenye miguu yangu nikaona dunia ikizidi kuwa ndogo zaidi na zaidi hadi hapo inilipo shindwa kuiona tena. Mimi wala sikuelewa, lakini mimi niliachwa nikiwa angani na huku nikiwa nimeushikilia Mkono wa Bwana.

Kisha mimi nikapatwa na hisia ya kuchukuliwa ndani yake …, kwa kweli sijui – nadhani ilikuwa ni huko kwenye anga za juu, labda kwenye mbingu za juu (nje ya malimwengu). Mimi nilikuwa naweza kuona roho nyingi zilizo kuwa zinaonekana kama mawingu myeupe; nazo roho hizo zilikuwa zinaweza kuruka. Mimi niliweza kuona mawingu hayo meupe mengi, mengi, mengi sana au labda roho zikiwa zinaruka juu. Hii ilikuwa ni kitu cha ajabu sana sana. Sehemu hiyo ilikuwa inaonekana kama haikuwa na ardhi kama ardhi hii tunayo ifahamu.

Maono:

Kisha mimi nikaona Mwanga fulani mkubwa na wenye Nguvu sana ukiwa unatembea na kupita ndani ya mawingu haya meupe au roho hizo. Mlima huo wa Mwanga Mweupe ulikuwa unaonekana ukifunika roho hizo au mawingu hayo meupe; wakati zikiwa zinanijia mimi; kutokea kwenye upande wangu wa kulia. Mimi pia nilikuwa naweza kuona aina fulani ya mawimbi yaliyo chafuka yakipita pale kwenye roho hizo wakati Mwangu huo Mweupe ulivyokuwa unapita juu yao. Mimi naamini alikuwa ni Yehova akiwa anatembea Mbinguni. Mimi pia nilikuwa naweza kuhisi Nguvu hii kubwa sana. Kisha wakati ule ule Mwanga uliponipitia; mkono wangu wa kushoto ukaja chini upande wangu juu ya kitanda changu.

Maono:

Kisha katika ulimwengu wa roho, mimi niliona utepe katika kila kiganja cha mikono yangu kwenye sehemu ile ya kufungia saa. Nilivyozidi kujiangalia mwenyewe, niliona tepe hizo zilizokuwa kwenye viganja vya mikono yangu zikijisogeza zenyewe kwenda juu na chini. Kisha mimi niliona kitu fulani ambacho nashindwa jinsi ya kukielezea. Hizo tepe mbili mara zika anza kupanda juu ya mikono yangu na kupitia kwenye sehemu ya juu ya kifua changu na kupita na kuingia kwenye mikono yangu ya kila upande kwa kubadilishana (zilipita ndani ya kifua changu na kukutana na ule utepe mwingine na kuingiliana zenyewe kwa zenyewe na kubadilishana) na kutelemka hadi kwenye kila kiganja kwa kubadilishana.

Maono:

Mimi niliona sehemu ya ndani ya koromeo la kwenye mdomo wa mtu fulani ikiwa na matabaka ya ngozi ambayo ilikuwa inaonekana kama miali ya mioto.

Maono:

Kisha sura hiyo ya maono ya mdomo wa mtu ikabadilika na kuwa sehemu au mfereji wa kizazi cha mwanamke wa aina ya ki-“Caucasian” naye alikuwa akijifungua mtoto mweusi. Mimi niliona kichwa cheusi cha mtoto aliyekuwa anazaliwa.

Maono:

Maono yaliyo futa yalikuwa ni ya joka; ambaye alifunga mara mmoja kinywa chake juu ya mawingu fulani myeusi. Ilikuwa inaonekana kama joka aliye fanana sana na yule joka wa aina ya “dragon”; ambaye moshi ulikuwa unatoka kwenye sehemu ya upande wa kinywa chake au nikama alikuwa akila kitu fulani.

Maono:

Kisha nikaona maono ya kitu kama meli ya vita, labada aina ile ya mizinga (destroyer), ikiwa inatembea kwa haraka sana juu ya maji.

Maono:

Lakini bado katika ulimwengu wa kiroho, Mimi niliweza kuona ndani ya mlipuko wa kivolkano na kuona mambo yote yaliyo kuwa yanafanyika ndani yake. Mimi nilikuwa wala sisikii joto lile la volkano nami nashindwa jinsi ya kuielezea vizuri.

Maono:

Mimi naona kivuli cha milima au miamba mikubwa, lakini mawingu yenyewe yalikuwa na rangi ambayo siyo ya kawida. Mawingu yalikuwa yanaonekana kuwa na rangi ya zambarau iliyokuwa nyeusi lakini ilikuwa inapitisha mwanga.

Maono:

Kisha nikaona maono ya mbweha aliyekuwa na jicho jeusi. Jicho lake la kulia lilikuwa limefanywa kuwa jeusi. (Mwisho).

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.