1366. Occurrence given to Raymond Aguilera on 22 July 1999.

During my prayer times in the City of Jerusalem, I was having a very hard time focusing on the Lord, but I could sense this invisible Dome of protection around me. The Old City of Jerusalem was in walking distance from my hotel, and I could sense this incredible war in the spirit over the City during my nighttime prayers. Every night I would read the Bible before I went to sleep and this helped a lot. I was reading the Book of Jeremiah, and the more I read Jeremiah, the more I wondered what happened during Jeremiah's time. Realizing that Jerusalem was surrounded when this happened - it made me wonder even more! I have no idea if Jeremiah sensed the same spiritual warfare I was sensing every night, but the whole city seemed to be in an uproar and mad at Jeremiah. The other prophets that were saying the opposite of what Jeremiah said must have believed that what they were hearing was from God also. The frightening thing was Jeremiah was the only one who was hearing the Lord clearly. This made me more determined to stay focused!

Every night I had demonic spirits tell me this and that until I was beginning to doubt which was the Lord and which were the devils. I prayed and I prayed and I tried to focus the best I could, but I felt like I was on this roller coaster that went racing up and down. Then out of nowhere, I realized what the Lord was doing with me. He was showing me how strong the demonic forces are in Jerusalem and how they fooled the other prophets in Jeremiah's time. These are very strong and powerful lying spirits and now I could see how the other prophets got fooled. They must of really believed they were hearing from God too.

So I prayed to the Lord, "How am I to tell it is you or tell the difference between you and them with all of this interference from these demonic spirits? And how can I even trust your Voice now? I don't even know the next place to Anoint. How can I proceed?"

Then Lord said, "Seek and you will find!"

All I could say in return was: "Lord, - I am a fish out of water here! If I make a mistake do not say I didn't warn you. These deceiving spirits are very, very good and I can truly say I am walking on water now! I can truly see how the prophets of Jeremiah's time got fooled. The more I read the Book of Jeremiah the more I understand his obstacles in the spirit. I am going to need some confirmations if I have some doubts."

And the Lord said, "Don't worry, We are with you!"

I said to the Lord, "Please don't get mad if I test and test and re-test your Word during my stay in Israel."

Comments: I might add that I knew the importance of my mission in Israel and walking into all of this unusual powerful spiritual warfare was frightening. But yet, I could still sense this powerful Dome of protection around me. As if a nuclear bomb could have gone off in my lap it would not have hurt me. I could really sense this protection very tightly around me, but yet - these demonic forces could still speak to me. This is very strange stuff!

1366. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Julai 1999.

Wakati wa saa ya maombi nikiwa ndani ya Jiji la Yerusalemu, mimi nilikuwa na pata matatizo makubwa ya kuweka umakini wangu kwa Bwana, lakini mimi nilikuwa naweza kuhisi ukuta au bakuli la ulinzi lisilo onekani ambalo lilikuwa limenizunguka mimi. Jiji Kongwe la Yerusalemu lilikuwa karibu kiasi cha mwendo wa miguu kutoka kwenye Hoteli yangu niliyokuwa ninakaa, nami nilikuwa naweza kuhisi vita hivi vikubwa wakati wa maombi yangu ya usiku. Kila usiku nilikuwa nasoma Biblia kabla ya kwenda kulala na hili lilinisaidia sana. Mimi nilikuwa nasoma Kitabu cha Yeromia, na jinsi nilivyozidi kusoma Kitabu cha Yeromia, ndivyo kwa jinsi hiyo hiyo mimi nilivyopatwa na hamu ya kutaka kujua kulitokea nini wakati wa enzi za Yeromia. Nikiwa na tambua kuwa wakati huo Yerusalemu ilikuwa imezungukwa na majeshi ya adui – hii ilizidi kunipa hamu ya kujua kulitokea nini hasa hasa! Sielewi kama Yeromia alikuwa anahisi vita hivyo vya kiroho kama hivi mimi nilivyo kuwa ninaihisi kila usiku hapa, wakati huo mji wote ulikuwa unaonekana uko kwenye hasira kubwa wakiwa wamemghadhikbikia sana Yeromia. Manabii wale wengine waliokuwa wakitabiri kinyume cha kile Yeromia alicho kisema lazima wao waliamini kwa uhakika kuwa kile walichokuwa wanakisema lazima kilikuwa kimetoka kwa Mungu pia. La kutisha ni kuwa Yeromia peke yake ndiye aliyekuwa akimsikia Bwana kuwa ufasaha. Hili lilinifanya mimi nizidi kung’ang’ania na kuwa umakini mkubwa!

Kila usiku mimi nilikuwa naambiwa na mapepo wachafu hiki na kile mpaka kufikia kiasi cha mimi kuanza kuwa na mashaka kuhusu ni ipi ni ya Bwana na ipi ni ya mashetani. Mimi niliomba na kuomba nami nikajaribu kuweka umakini wangu kwa bidii kwa kadri niwezavyo, lakini mimi nilikuwa najisikia kama niko kwenye bembea ambayo ilikuwa inaenda juu na kisha chini na juu tena na chini. Kisha bila ya kutarajia, mimi mara nikang’amua ni nini Bwana alichokuwa ananifanyia. Alikuwa ananionyeshea ni kwa kiasi gani mapepo walioko pale Yerusalemu walivyo na nguvu kuwa na ilikuwa ni kwa namna gani walivyoweza kuwadanganya Manabii wa nyakati za Yeromia.  Hawa walikuwa ni mapepo wa undanganyifu wenye nguvu kubwa sana sana na hivi sasa naweza kutambua ni kwa namna gani jinsi hao Manabii wengine walivyoweza kudanganyika. Lazima wao waliamini kwa uhakika kabisa kuwa wao walikuwa wanasikia kutoka kwa Mungu pia.

Kwa hiyo nikamwomba Bwana nikisema, "Mimi nitakutofautishaje Wewe na hao mapepo katikati ya vurugu hizi zitokazo kwa mapepo wachafu? Nami nitaaminije kuwa ni Sauti Yako sasa? Iwapo mimi hadi sasa hata sifahamu eneo linalo fuata la kuwekwa Wakfu. Sasa nitaendeleaje?"

Kisha Bwana akasema, "Tafuta nawe utapata!"

Yote ninayo weza kusema kwa majibu ni kuwa: "Bwana, - mimi ni samaki nitokaye kwenye maji hapa! Kama nitafanya kosa usije ukasema kuwa sikukuonya. Hao mapepo wa udanganyifu wanajua kwa uhakika kabisa jinsi ya kuhadaa; hivyo mimi hivi sasa ninasema kwa uhakika kuwa ninatembea juu ya maji! Mimi sasa hivi na tambua jinsi wale mitume wa nyakati za Yeromia walivyo danganyika. Kwa jinsi ninavyozidi kusoma Kitabu cha Yeromia ndivyo ninavyozidi kuelewa vikwazo aliyokuwa navyo katika ulimwengu wa kiroho. Mimi nitahitaji udhibitisho kama nikiwa na mashaka.”

Na Bwana akasema, "Usijali, Sisi tuko pamoja nawe!"

Mimi nikamwambia Bwana, "Tafadhali usinikasirikie kama nitalijaribu na kulijaribu na kilijaribu tena na tena Neno Lako wakati wa kukaa kwangu hapa kwenye nchi ya ya Israel."

Ilani: Labda ni ongezee kwa kusema kuwa mimi nilikuwa na fahamu fika; umuhimu wa safari yangu hiyo katika nchi hii ya Israel, na kuingia kwenye mapambano haya makali na jeshi la mapepo wa wachafu ilikuwa inatisha sana. Lakini bado, mimi nilikuwa naweza kuhisi Kifuniko kama cha Bakuli cha ulinzi ikiwa imenizunguka mimi. Kana kwamba hata bomu la kinukilia ingenipasukia miguuni mwangu; mimi nisingeli weza kudhurika kutokana na ukuta huo wa ulinzi. Mimi naweza kuhisi ukuta huo wa usalama ukiwa umenizingira mimi kwa uhakika, lakini bado – hawa mapepo wachafu walikuwa wanaweza kujipenyeza na kunisemesha mimi. Hili ni jambo la ajabu sana!

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.