|
1367. Occurrence given to Raymond Aguilera on 22 July 1999 at noon. I figured that the hardest place to Anoint would be the areas in Jordan, for we needed visas to get into the country and a car to move around undetected. So we decided first to go to a tourist agency at the beginning of our mission trip to find out the cost in getting a private tour. When the tour agency started asking us questions on why we wanted a private tour and the reasons for this trip (for he had cheaper tours where more people went), we answered him the best we could. We had to watch our wording for everyone in Israel is worried about terrorists. After we received the price for our private tour, we decided to leave the agency to pray to the Lord about this tour package. We went to an outside café and we prayed. And the Lord gave me this Word: "Anoint only Mt. Nebo". "The rest is just worthless pagan desert."So we prayed again to be sure if we should take the next available private tour. And the Lord said, "When you pluck a feather from a goose does it jump?"So we understood the above as a yes and we purchased the private tourist package from the tourist agency. The Anointed areas: We left the tourist agency and proceeded toward Tel Aviv to begin the Anointing on the 30-mile perimeter from the Old City of Jerusalem. We stopped at Yavne and the Lord said, "Anoint here". This was in a park neighboring a synagogue.
When we arrived at Qiryat Gat the Lord said, "Fine"Then we drove past a park and the Lord said, "Keep moving!"Then we drove into Uzza and the Lord said, "Seek and you will find!" Then the Lord led us to another park, which had a large water tank and synagogue and we Anointed an area in the park.Then we drove towards Edn Dhahiriya. We were about 8 Km into the West Bank and past the military checkpoint, and I was a little nervous because we were driving a rental car, (which was clearly labeled on the side doors). We were told by the rental agency not to drive the car into these areas for it was dangerous (Muslim cities in the West Bank). Well, we drove in this forbidden area until the Lord said, "Do not go much further!" So we did a U-turn at the next intersection and I quickly poured the Olive oil as quickly as possible onto the ground from the back door of the car. For it looked like many workers were returning home from work and we did not want any trouble if some of them saw us Anointing the ground. And there were soldiers out there with REAL guns. So there we were, three Christians, Anointing a small Muslim area for the Lord. I don't really believe they would have understood what we were doing. They were more likely to believe we were terrorists. So we left the area as quickly as possible. I remember Carl once said that the Israelis and the Jordanians would find it easy to believe he and Mark were terrorists, but that I didn't fit the part. (I wonder if he was saying I was to old and out of shape? <Smile>) So then we drove on highway 31, and away from the potential trouble. Then as we were driving the Lord said, "Pull over and park in a safe place!" So as we drove looking for a safe place to park - the Lord said, "What goes up comes down!" So we kept driving looking for that safe place to park the car, then as we were still driving the Lord said, "Shake the dust off your shoes!" I saw a watermelon stand in the distance and I suggested we stop and buy a watermelon for it looked like a safe place to stop. So we purchased a watermelon and we shook the dust off our shoes when we climbed in the car as the Lord had told us to do. By this time it was about 9 or 10 PM and Carl was getting sleepy so we stopped at a resort hotel at the Dead Sea about 5 miles south of Massada. It was very, very hot at this place, so we rested a little and we prayed, and the Lord said to move on. So we began on our late night drive again and as we proceeded toward the next Anointing spot, I heard a demonic voice say, "You don't have to stop here!", "You quack!" Then when we reached our destination I heard a demonic voice say, "You don't want to do this!" So we stopped the car at the side of the highway and I opened the back door and Anointed the ground in the Name of the Jehovah, Jesus Christ and the Holy Spirit. I remember Carl and Mark had gotten out of the car and I guess they were going to take pictures or something, when I heard the Voice of the Lord say, "Now - leave here quickly!" I told Carl and Mark what the Lord had said and we drove away from that place as quickly as we could. Then some time later the Lord said, "Thank you good and faithful servants!" This was a very strange drive back to our hotel. We were all tired and Carl was still a little sleepy as he drove the car and it seemed like we would never get back to our hotel. Then I heard another demonic voice say, "Slow down and stop. Take a break!" For some reason the demons wanted us to stop and the Lord wanted us to quickly leave. We drove for another hour or so and we stopped at a gas station and rested a little before we reached our hotel. It was a very long day, but we covered a lot of area and Anointed three or four spots. |
1367. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Julai 1999 mchana. Mimi nilitarajia kuwa eneo ambalo litakuwa gumu sana kuiweka Wakfu itakuwa ni eneo lile la Yordani, kwa maana sisi tulitakiwa kuwa na kibali (Visa) cha kuingia huko nchini Yordani na pia kupata gari la kusafiria kwenye eneo la nchi hiyo bila ya kugunduliwa. Kwa hiyo sisi tuliamua kwanza tuende kwenye ofisi ya Wakala wa kitalii kabla hata ya kuanza safari hiyo ili kupata makisio ya gharama ya kukodisha gari. Pale Wakala wa magari ya kukodisha walipoanza kutuuliza maswali kuhusu ni kwanini tunahitaji usafiri huo wa kibinafsi kwa safari hiyo (kwa maana yeye alikuwa na usafi wa pamoja ambao ni wa gharama nafuu na ambao watu wengi huwa wanapendelea kuchukua), sisi tukajaribu kumpa majibu ya kumridhisha kwa kadri ya uwezo wetu. Ilitubidi tujihadhari na maneno yetu kwa maana kila mtu katika nchi hiyo ya Israeli alikuwa na wasiwasi na usalama kwa ujumla. Baada ya sisi kupokea makisio ya gharama ya kukodisha gari kwa ajili ya usafiri wa kitalii wa kibinafsi, sisi tuliamua kuondoka kutoka pale kwa wakala wa kitalii ili kwenda kumwomba Bwana kwa ajili ya kupata maelekezo ya tufanye nini kuhusu gharama ile. Sisi tulienda nje ya mgahawa na kuomba. Kisha Bwana alinipa Neno hili: "Uweke Mlima Nebo Wakfu pekee". "Yaliyobaki mengine ni jangwa tupu la wapagani ambalo halina dhamani yeyote."Kwa hiyo sisi tuliomba tena ili kuwa na uhakika kama tuchukue usafari binafsi unaofuata wa kitalii. Naye Bwana akasema, "Unapo ng’oa unyoya wa bata mzinga je, yeye anaruka?"Kwa hiyo sisi baada ya hapo tulielewa maelekezo hayo kumaanisha kuwa ni ndiyo ya kutoka kwa Bwana, nasi tuka nunua usafi wa kibinafsi wa kitalii kutoka kwa wakala wa usafiri. Eneo lililowekwa Wakfu: Sisi tulitoka kwenye ile ofisi ya wakala wa kitalii na kuelekea Tel Aviv ili kuanza safari ya kuweka eneo lile lenye nusu upenyo wa maili 30 kutoka Jiji la Yerusalemu. Sisi tulisimama pale kwenye mji wa Yavne na Bwana akasema, "Wkeni Wakfu hapa". Hii ilikuwa ni kwenye eneo lililokuwa wazi karibu na Sinagogi.
Tulipofika pale Qiryat Gat Bwana akasema, "Sawa"Kisha sisi tukaendelea mbele kupita kwenye uwanja wa mapumziko ambako Bwana akasema, "Endeleeni mbele!"Tuliendelea mbele hadi mji wa Uzza na Bwana akasema, "Tafuteni nanyi mtapata!" Kisha Bwana akatupeleka kwenye sehemu nyingine ya kiwanja cha kupumzikia, ambayo ilikuwa na tanki kubwa la kuhifadhia maji, pamoja na Sinagogi nasi tukapaweka Wakfu eneo hilo; lililokuwa karibu na kiwanja hicho cha kupumzikia.Kisha sisi tukaelekea kwenye mji wa Edn Dhahiriya. Sisi tulikuwa tuko kiasi cha kilometa 8 ndani ya eneo la Ukingo wa Magharibi na tulikuwa tumevuka kwenye kizuizi cha usalma cha Wanajeshi cha mpakani, nami nilikuwa na uwoga kidogo kwa sababu sisi tulikuwa tukiendesha gari lililokodishwa (ambayo ilikuwa imewekewa alama kubwa kwenye milango yote ya gari letu hilo). Nasi tulikuwa tumeagizwa na kampuni ya gari letu hilo kuwa tusiende na gari lao hilo kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi kwa maana ilikuwa ni eneo la hatari (Kwani ni eneo la Kiislamu la Ukingo wa Mangharibi). Naam, sisi tulisonga mbele kuelekea sehemu hiyo ambayo imekatazwa hadi pale Bwana alipotuambia "Msiendelee zaidi ya hapo!" kwa hiyo sisi tuligeuza gari letu kwa kupiga "U-turn" na kurudi tulipokuwa tunatoka kwenye eneo la makutano iliyokuwa mbele yetu na kwa haraka tuka mimina mafuta yale ya mizeituni na kupaweka Wakfu kwa haraka iwezekanavyo; kutoka kwenye mlango wa nyuma wa gari letu hilo. Kwa maana ilikuwa inaonekana kuwa kulikuwa na wafanyikazi wengi walio kuwa wanarudi nyumbani kutoka makazini mwao; kwa hiyo sisi hatukutaka matatizo yeyote hapo watakapotuona tukiwa tunaweka Wakfu ardhi hiyo. Na kulikuwa na askari halisi wakiwa na mabunduki HALISI. Naam sisi tulikuwa hapo Wakristo watatu tukiwa tunaweka Wakfu eneo la Waislamu kwa ajili ya Bwana. Mimi naamini wao wasingeliweza kuelewa kile sisi tulichokuwa tunakifanya. Wao kwa kweli wangeliweza kuamini kwa urahisi kuwa sisi ni magaidi. Kwa hiyo sisi tuliondoka kutoka kwenye eneo hilo kwa haraka iwezekanavyo. Mimi nakumbuka kuwa kuna wakati Carl aliwahi kusema kuwa ilikuwa ni rahisi kwa Waisraeli na Wayordani kuamini kuwa yeye na Mark walikuwa ni magaidi, na ya kuwa mimi sikuwa naweza kudhaniwa hivyo. (Mimi sielewi kama yeye alikuwa akijaribu kusema kuwa labda mimi ni mzee na kuwa sina sura ya kuwa gaidi na mwili unaofanana na gaidi? <Tabasamu>) Kwa hiyo baada ya hapo sisi tulielekea kwenye Barabara Kuu Na. 31, na kuelekea kwenye lile eneo la hatari kubwa. Wakati tulipokuwa tunaeleka huko kwa gari letu, Bwana akasema, "Simameni na egesheni gari lenu kwenye eneo lililo na usalama!" Kwa hiyo wakati tulipokuwa tunaendesha gari letu huku tukiwa tunatafuta eneo lenye usalama la kuegeshea gari letu – Bwana akasema, "Kile kinachoenda juu kitarudi chini!" kwa hiyo sisi tuliendelea kuendesha gari letu tukiwa tunatafuta eneo lililo na usalama la kuegesha gari, wakati tukiwa bado tunaendesha Bwana akasema tena, "Kung’uteni vumbi iliyoko kwenye viatu vyenu!" Mimi niliona tikiti maji kwenye eneo fulani mbele yetu nami nikashauri kuwa tusimame hapo na tununue hiyo tikiti maji kwa maana niliona kuwa ni sehemu yenye usalama. Kwa hiyo sisi tulinunua tikiti maji hiyon na kukung’uta vumbi kutoka kwenye viatu vyetu pale tulipokuwa tunapanda kwenye gari letu kama Bwana alivyotuagiza sisi tufanye. Hdi wakati huo ilikuwa ni kiasi cha saa 3 au 4 na Carl alikuwa ameanza kusinzia kwa hiyo sisi tukaamua kusimama na kupumzika kwenye hoteli ya kitalii kwenye eneo la mgahawa wa kwenye Ziwa la Chumvi kiasi cha maili 8 kusini mwa Massada. Ilikuwa ni sehemu yenye joto kali sana sana, kwa hiyo sisi tuka pumzika na kuomba, na Bwana akasema songeni mbele. Kwahiyo sisi tuliendelea na safari yetu ya usiku wa manane tena, wakati tulipokuwa tunakaribia kwenye eneo linalofuata la kuwekwa Wakfu, mimi nilisikia sauti ya pepo mchafu ikisema, "Ninyi hakuna haja ya kusimama hapa!", "Ninyi matapeli!" kisha sisi tulipofika eneo letu linalofuata mimi nilisikia sauti ya pepo ikisema, "Ninyi natumaini hampendi kufanya hivi!" Kwa hiyo sisi tulisimamisha gari letu pembeni mwa hiyo barabara kuu na kufungua mlango wa nyuma wa gari na weka Wakfu ardhi ya eneo hilo katika Jina la Yehova, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Mimi nakumbuka Carl na Mark walikuwa wametelemka kutoka kwenye gari na ninadhani walikuwa wanajitayarisha ili wapige picha au kufanya kitu fulani, ndipo nikasikia Sauti ya Bwana ikisema, "Sasa – ondokeni kutoka hapo kwa haraka sana!" mimi nilimwambia Carl na Mark kile Bwana alicho kisema nasi tukaondoka kutoka pale mbio. Kisha wakati fulani Bwana alisema, "Asanteni watumishi waaminifu!" Ilikuwa ni safari ya ajabu sana wakati wa kurudi kwenye hotelini yetu. Sisi sote tulikuwa tumechoka na Carl aliyekuwa anaendesha gari alikuwa bado anasinzia, nasi tulikuwa tunajisikia kama hatungelifika pale hotelini kamwe. Kisha mimi nikasikia sauti ya pepo mwingine ikisema, "Punguzeni mwendo na msimame. Mkapumzike kidogo!" kwa sababu ambayo sielewi mimi; pepo alitaka tusimame na Bwana alitaka tutoke mahala pale haraka. Sisi tuliendesha gari letu kwa saa mmoja tena na kusimama kwenye kituo cha mafuta na kupumzika kwa muda mfupi; kabla ya kufika kwenye hoteli yetu. Ilikuwa ni siku iliyokuwa ndefu sana, lakini sisi tulifanikiwa kutembea na kuweka Wakfu maeneo matatu au manne hivi. |
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )