1410. Occurrence given to Raymond Aguilera on 28 August 1999.

E-mail to e-mail list:

Hello Brothers and Sisters,

The warfare around my home has intensified again. Every time I try to type any new material my right arm begins to really hurt. I had to change the use of my mouse to my left hand. The other day I went to the Post office to get my mail and found my mailbox empty.

Then before I locked it, I heard a demonic voice say, "I am going to stop all funds going to this ministry!"

Then I heard the Lord say, "No he isn't!"

I might say this surprised me and I locked up the P.O. Box and drove home wondering what was going on. Since I returned from Israel, there has been nothing but warfare and more warfare. My right arm is always hurting and at times I cannot sleep.

Then the next day I went to the Post Office again and I heard the same voice say, "Didn't I tell you that I was going to stop the funds going to this ministry!"

For the P.O Box was empty again. This time the Lord said nothing, but in my spirit and flesh I remembered what the Lord had said the day before. It was as if the Lord was saying to me in my spirit, "DO YOU TRUST ME?" When I get this sense in the spirit, I know better than to ask the Lord for clarification. For He had already told the answer I needed to hear the day before.

I am going to need more prayers through these hard times, because I am going to try to begin to type the new material again. I guess, it is time to carry my cross and follow the Lord, even if it hurts. Come to think about it - I have been getting e-mail and a letter from a few brothers, who wrote to me that the Lord told them to send me something extra. I found their letters strange and wrote them back telling them I was all right. Maybe I am not all right and I do not even know it!

Then after receiving some hate mail a few days ago, I began feeling down and out. Then a good friend and brother in Christ began telling me his doubts and to my surprise the Lord lifted me and reveled all the prophecies He had given over the past ten years about days like this. Praise the Lord!!! For the Lord showed up and not only lifted me up, but He gave me the added strength I needed to run not to walk after Him. Praise the Lord again and again!

Yours in Christ,

ray

1410. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 28 Agusti 1999.

Barua Pepe kwa orodha ya Barua Pepe:

Wapendwa Kaka zangu na Dada zangu katika Kristo,

Mapambano ya kiroho kuzunguka nyumba yangu yameongeza kasi tena. Kila wakati ninapojaribu kuandika mambo mapya mkono wangu wa kulia unaanza kuuma sana. Imenibidi kubadili utumiaji wa chombo cha kuwasiliana na kompyuta iitwayo “mouse” kutoka mkono wa kulia na kubadili iende mkono wangu wa kushoto. Siku iliyopita nilienda posta ili kuchukua barua zangu kwenye sanduku na kukuta sanduku langu likiwa tupu.

Kisha kabla ya mimi kufunga kisanduku changu hicho, mimi nilisikia sauti ya kishetani ikiwa inasema, "Mimi nitaenda kuzuia fedha zote zisije kwenye huduma hii!"

Kisha nikasikia Bwana akisema, "Hapana yeye hataweza kuzuia!"

Labda niongeze kusema kuwa hili lilini shangaza mimi nami nikafunga kisanduku changu hicho cha Barua na kuondoka kwa gari langu kurudi nyumbani; nikiwa ninawaza kuhusu ni nini hasa kinacho endelea huko. Toka nirudi kutoka safari yangu ile ya nchini Israel, ilikuwa ni mapambano baada ya mapambano. Mkono wangu wa kulia unauma kila wakati na kuna wakati hata ile kulala nilikuwa nashindwa.

Kisha siku iliyofuata mimi nilienda tena Posta; nakusikia sauti ile ile ikisema, "Si nilikuambia kuwa nitaenda kuzuia fedha zisiingie kwenye huduma hii!"

Kwa maana sanduku langu la barua lilikuwa tupu tena. Safari hii Bwana hakusema lolote, lakini ndani ya roho yangu na mwili wangu wa nyama mimi nilikumbuka kile Bwana alicho kisema jana yake. Ilikuwa ni kama Bwana alikuwa anasema ndani ya nafsi yangu kuwa, "JE, UNANIAMINI MIMI?" Mara nilipopata ushuhuda huu moyoni mwangu; mimi nilijua ni vizuri nisidhubutu kumwuliza Bwana tena kuhusu kupata ufafanuzi. Kwa mana Yeye alikwisha nipa jibu nililotaka kulisikia siku iliyopita.

Mimi nitaenda kuhitaji maombi zaidi katika siku hizi za shida, kwa sababu mimi nitajaribu kuanza kuandika unabii zaidi tena. Nadhani ni wakati wangu wa kubeba msalaba wangu na kumfuata Bwana, ingawaje inaumiza. Nimeanza kukumbuka kuwa – nimekuwa nikipokea Barua pepe kadha za kutoka kwa ndugu fulani fulani zikiwa zinasema kuwa Bwana amewaambia kuwa niwatumie fedha zaidi. Mimi niliona Barua hizo ni za ajabu na kuwajibu kuwa yeye hakuwa na shida ya fedha. Labda nilikuwa sijajielewa na kuwa ni kweli nilikuwa na shida nami bila ya mimi kujua!

Kisha baada ya kupokea Barua kadhaa za chuki siku chache zilizopita, mimi nilianza kujisikia vibaya na kuanza kukata tamaa. Kisha rafiki yangu mwema na ndugu katika Kristo akaanza kuniambia kuhusu mashaka yake na kwa mshangao wangu Bwana aliniinua upya na kunifunulia kwa kunikumbusha kuhusu unabii mbali mbali aliyowahi kunipa kwa muda wote wa miaka kumi hii, kuhusu siku za namna hii. Bwana asifiwe!!! Kwa maana Bwana alijitokeza na siyo tu alininyanyua bali alinipa nguvu za ziada ambazo nilikuwa ninaihitaji ya kukimbia na wala siyo ya kutembea kumfuata Yeye. Msifuni Bwana tena na tena!

Wenu katika Kristo,

ray

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.