1413. Occurrence given to Raymond Aguilera on 13 October 1999.

This occurrence has to do with trust. The past three weeks, I have been putting in many, many hours into formatting the Prophecy material into book form. Finally I finished last week and I felt great. I have not answered my e-mail or have I done anything else but work on these two Prophecy Books.

Well, during this time, I kept thinking about what the devil had said to me about a month or so go, "I am going to stop the funds to this ministry", or something like that. During this time my arm had been hurting so much I could not do much even sleep. Then the Lord totally healed my arm one night at 3 AM in the morning by telling me to stretch to the right, then to turn and stretch to the left. Well, like I have said once before in an e-mail to the people on the e-mail list. My back began to pop like popcorn and instantly my arm was totally healed. Boy - was this a wake-up call to me, for I was really down and out on almost everything.

Then guess what happened? A door opened up for getting these prophecies published. With my arm healed, I began to organize all the prophecy data into some kind of book form. After speaking to the Book Publishers a few times I had an idea of how they wanted the book data. Well, after three weeks of hard work I finished the two Prophecy Books.

I was really feeling GREAT! So I called my friend Carl for prayer. We generally try to get together several times a week for prayer. So I began to tell him about all the work I had been doing and for some reason I had not mentioned to him about my arm being healed. He was really amazed, for he had seen how much pain I had been in. All he kept saying was, "Praise the Lord", over and over.

Well, we began to put together our prayers and I began to tell him that Irene had called and had given me some bad news. That she had lost her job and then she got robbed and that she called me for some financial help. I told him how I had paid most of my bills and sent Irene some money and I still had $20 dollars in my checking account. This reminded me of what the devil had said that he was going to stop the money to this ministry. But he lost again, for I still made it through the month and I still had $20 dollars left in my checking account. This made Carl praise God even more and he mentioned how the Lord has helped this ministry over the past 10 years. I might say I did get a little worried for a lot of the ministry support just stopped last month, but as always, the Lord came through. This is why we all need to trust and trust in the Lord always. For if the Lord is on your side, who can stand against you!

Then to put frosting on the cake I told Carl, that Omar, our guide in Jordan sent me a letter with some post cards of Mount Nebo. Mount Nebo was one of the places we anointed on the Israel mission trip. Well, Carl was surprised again for he did not believe I would get my pictures from Omar. So Carl and I had a good prayer time and I told him I was going to finish uploading the Finish Translation data onto the web site and proceed with documenting the Israel mission trip on Monday.

Guess what happened next? The next day the Lord informs me that the work I did on the Prophecy Books was wrong! To my surprise - the Lord was right again! I had made a mistake in formatting the Prophecy Books. So for the next 6 days I had to redo the two Prophecy Books and now I have THREE Prophecy Books after the new formatting. To end this occurrence, I learned again "That I have to keep trusting in the Lord, even if I have to do the work twice!" God bless you all!!!

1413. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 13 Oktoba 1999.

Tukio hili lina uhusiano na uaminifu. Katika wiki tatu zilizo pita, mimi nimekuwa nikiweka masaa mengi sana sana; katika kutengeneza habari hii ili ikae kwa muundo wa Kitabu cha Unabii. Mwishoni wiki iliyo pita nilifanikiwa kuikamilisha na kujisikia vizuri. Mimi sikiweza kujibu Barua pepe wala kufanya kazi yeyote zaidi ya kufanya kazi kwenye vitabu hivi viwili vya Unabii.

Naam, wakati huo wote; mimi nikawa nafikiria kuhusu kile shetani alichokuwa ameniambia kiasi cha mwezi mmoja hivi uliopita kuwa, "mimi nitaenda kuzuia fedha zisije kwenye huduma hii", au kitu kama hicho. Wakati huo mkono wangu ulikuwa unaniuma sana kiasi ambacho nilikuwa na shindwa kufanya kazi hata ile kulala. Kisha Bwana akawa amenitibu mkono wangu kabisa; usiku mmoja kwenye saa 9 ya usiku, kwa kuniambia ni nyooshe mkono wangu kuelekea kulia, na kisha mimi nijigeuze na kujinyoosha kuelekea upande wa kushoto. Naam kama mimi niilvyo kwisha kusema hapo awali kwa Barua pepe kwa watu walioko kwenye orodha ya Barua pepe. Mgongo wangu ukaanza kulipuka kama mahindi ya kuchoma au bisi na kwa ghafla mkono wangu ukawa umepona kabisa. Ndugu yangu – naama sielewi kama hili lilikuwa ni kengele ya kuamka, kwa maana mimi nilikuwa nimekata tamaa ya karibia kila kitu.

Kisha unadhani ilitokea nini? Mara mlango ukafunguka wa kuchapishwa kwa vitabu hivi vya unabii. Na huku mkono wangu ukiwa umeponywa, mimi nikaanza mara kutayarisha mandiko yote kwa ajili ya kuchapwa kwenye kitabu. Baada ya kuongea na Wataalamu wa Kuchapa Vitabu mara kadhaa; mimi sikuwa naelewa wao walitaka yale maandko nayaweke katika muundo au sura gani. Naam, baada ya wiki tatu hivi ya kazi ngumu, mimi nilimaliza kutayarisha vile vitabu viwili vya unabii.

Mimi kwa kweli nilikuwa ninajisikia VIZURI NA MWENYE RAHA! Kwahiyo nikampigia simu ndugu yangu Carl kwa ajili ya kufanya naye maombi. Mimi na yeye huwa mara kadhaa kwa wiki tunakuwa pamoja ilikufanya maombi. Kwa hiyo mimi nikamweleza kuhusu kazi ile niliyokuwa nafanya, lakini kwa sababu nisiyoifahamu, mimi sikumwambia kuhusu habari ya mkono wangu kuponywa. Yeye kwa kweli alishangazwa, kwa maana yeye alikuwa anajua maumivu niliyokuwa nayo hapo awali. Yeye yote aliyokuwa anasema nikuwa “Bwana asifiwe” tena na tena.

Naam, sisi tulianza kuweka maombi yetu pamoja na kuanza kumweleza yeye kuwa Irene alikuwa amenipigia simu kunieleza kuhusu habari mbaya iliyomsibu. Yakuwa yeye alikuwa amepoteza kazi na kisha alikuwa ameibiwa na hivyo alikuwa anaomba msaada wa fedha. Nami nikazidi kumweleza jinsi mimi nilivyokuwa nimelipa sehemu kubwa ya madeni yangu na kumpelekea Irene fedha na bado nikabakiwa na dola ishirini ($20) katika akiba yangu ya cheki. Hili lilinikumbusha kuhusu kile ambacho shetani alichoniambia; ya kuwa yeye angelienda kuzuia fedha zisije kwenye huduma hii. Lakini bado alikuwa ameshindwa kufanya hivyo tena kwa maana mimi bado nilifanikiwa kulipa madeni yangu ya mwezi huu yote na bado nikawa nimebakiwa na dola 20 kwenye akaunti yangu. Hili lilimfanya Carl amsifu Mungu zaidi na zaidi tena na huku akitaja jinsi Bwana alivyo saidia huduma hii kwa miaka hii 10. Labda nisema mimi nilianza kuwa na wasiwasi kidogo kwa maana sehemu kubwa ya ufadhili wa huduma hii; mara ilisimama kwa ghafla mwezi uliopita, lakini kama ilivyo kawaida; Bwana alikuja kutusaidia. Hii ndiyo sababu kwanini inatulazimu kumwamini Bwana siku zote. Kwa maana kama Bwana yuko upande wetu; ni nani atakaye simama kinyume nasi!

Kisha baada ya kuweka mambo sawa na kuamsha hisia mimi nilimwambia Carl, kuwa Omari, yule aliyekuwa anatuongoza katika safari yetu ile ya kule nchini Yordani alituma barua pamoja na kadi za posta za Mlima Nebo. Mlima Nebo ulikuwa ni sehemu mmoja wapo tulipotembela na kuuwekea Wakfu katika safari yetu ile ya Israel. Naam, Carl alishangazwa tena kwa maana alikuwa haamini kama ningeliweza kupata picha kutoka kwa Omari. Kwa hiyo Carl na mimi tulikuwa na muda mzuri wa maombi; nami nikamweleza kuwa naenda kumalizia kuweka tafsiri ya unabii katika lugha ya Kifinish kwenye mtandao na kuendelea kuweka ripoti ya safari ya Israel kuanzia siku ya Jumatatu.

Unaweza kubashiri ilitokea nini baada ya hapo? Siku iliyofuta Bwana alinieleza kuwa kazi niliyofanya kwenye Kitabu cha Unabii ilikuwa na makosa! Kwa mshangao wangu niligundua kuwa Bwana alikuwa sahihi tena! Mimi nilikuwa nimefanya makosa katika kuanda Vitabu hivyo vya Unabii. Kwa hiyo kwa muda wa siku 6 zilizofuata, ilinibidi nikarudie vile vitabu viwili vya Unabii na sasa nina vitabu VITATU vya Unabii baada ya kuyafanyia kazi upya. Kumaliza tukio hili; mimi nilikuja kufahamu upya kuwa “Ilinilazimu kuweka imani yangu katika Bwana, hata kama itanilazimu kufanya kazi mara mbili!" Mungu awakubarikini ninyi nyote!!!

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.