1468. Vision given to Raymond Aguilera on 23 February 2000 at 3:40 PM.

I saw this darkness, I believe I saw it from a very strange angle, for I saw these animals walking at 90-degrees straight up towards Heaven. I saw this horse and this elephant walking side by side next to a cliff, and there was a light shinning on them. This light was shinning directly at me, but these animals were walking between the light and me, vertically up, so I could only see a highlighted shadow of the animals. Then I saw the horse almost fall into the cliff. I could see the horse hanging onto the edge of the cliff with his hind legs dangling over the edge. I did not see the horse fall down off the cliff (the horse was falling horizontally from where I was viewing it), but if he would have, I would not have been able to see where he fell, because everything was so dark. Though I did see the horse climb back onto the edge. These other animals were moving within this white light, but they were moving very naturally, vertically straight up, at a 90-degree angle. And what was so unusual, was that it was so dark outside of the light, it was pitch black, except for this light. (over)

Vision:

I saw this large serpent attack these animals, as they walked vertically straight up. Then this large hammer appeared, and hit the large serpent on top of the head and crushed its head. (over)

Vision:

I saw a stick with a round hoop on one end of it with a net around the hoop. This reminded me of a fisherman's net, and this net was laying on the side of a boat and they were using it for fishing. I could see the net above the water.

Vision:

I saw a vision of a cluster of grapes on the vine with a bunch of bees around them. (over)

Occurrence:

I heard the sound of a bell on this ocean buoy. I could not see it in the spirit, but I could hear it. The water also sounded very rough. (over)

Vision:

I saw these two birds feeding out of this feeder.

Prophecy:

The Lord said, "The only correct way is the Manner of God, and it is to the point!" (over)

Vision:

I saw this small garden tool planting a plant in a vase. (over)

Vision:

I saw this lizard wrap his whole body around this white, glowing, fluorescent ball.

1468. Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 23 Februari 2000 saa 9:40 mchana.

Mimi niliona giza fulani nene, nadhani niliona kutoka kwenye upenyo ambao haukuwa wa kawaida, kwa maana niliona wanyama wale wakiwa wanatembea kwa nyuzi 90 kuelekea juu Mbinguni. Mimi nilimwona tembo fulani akiwa anatembea ubavu kwa ubavu karibu na korongo, na kulikuwa na mwanga uliokuwa unawaangazia wao. Mwanga huo ulikuwa unanimulika mimi mmoja kwa mmoja, lakini wanyama hao walikuwa wanatembea kati ya mwanga na mimi, wakiwa wanaelekea mmoja ka mmoja kwenda juu, kwa hiyo mimi nilikuwa naona mwanga wa uvuli wa wanyama hao. Kisha Mimi nikaona farasi yule almanusa aanguke ndani ya korongo hicho. Nilikuwa naweza kuona akiwa ananing’inia ndani ya korongo lile kutoka kwenye ukingo ule na miguu yake ya nyuma ikiwa inaning’inia kutoka kwenye ukiongo huo. Mimi nikamwona farasi huyo akiwa ameanguka kutoka kwenye ukingo huo (farasi huyo alikuwa akianguka kwa usawa kutoka pale nilipokuwa ninamwangalia) lakini kama angelianguka mimi nisingeliweza kumwona alikoangukia kwa sababu mahali pale palikuwa na giza nene sana. Nadhani nilimwona farasi huyo akipanda tena kwenye ukingo huo mkali. Wanyama hao wengine walikuwa wanatembea na mwanga ule mweupe, lakini walikuwa wanatembea kikawaida na walikuwa wanapanda kwenda juu kwa nyuzi 90 kutoka ardhini. Na kile ambacho hakikuwa ni cha kawaida ilikuwa ni giza nene nje ya mwanga ule, ilikuwa ni giza kali sana, isipokuwa pale kwenye mwanga ule. (Mwisho).

Maono:

Niliona joka mkubwa akiwa anawashambulia wanyama hawa, wakati wakiwa wanapanda kwa wima mmoja kwa mmoja juu. Na kisha nyundo fulani kubwa mara ikajitokeza, na kumtwanga huyo joka mkubwa juu ya kichwa chake na kukiponda ponda. (Mwisho).

Maono:

Niliona fimbo iliyokuwa na kitu kama bangili ya mviringo kwenye mwisho wa fimbo hiyo na ikiwa imefungiwa wavu kuzunguka bangili hilo ya mviringo. Hii ilinikumbusha wavu wa wavuvi, na wavu huo ulikuwa umelala kwenye upande mmoja wa ngalawa na walikuwa wakiutumia kwa kuvulia. Nilikuwa naweza kuona wavu huo ukiwa juu ya maji.

Maono:

Niliona maono ya fungu la mzabibu uliokuwa kwenye tawi la mzabibu na kundi la nyuki wakiwa wameuzunguka. (Mwisho).

Matukio:

Nilisikia sauti ya kengele kwenye boya linaloelea baharini. Mimi nilikuwa siioni katika ulimwengu wa kiroho, lakini nilikuwa nikiisikia. Nayo maji yalikuwa yakisikika kuwa na mawimbi makubwa yaliyo chafuka. (Mwisho).

Maono:

Niliona ndege fulani wawili wakiwa wanakula kutoka kwenye sehemu mmoja ya kulishia chakula.

Unabii:

Bwana akasema, "Njia pekee iliyo sahihi ni Njia ya Mungu, na ni ya Uhakika!" (Mwisho).

Maono:

Mimi niliona chombo fulani kidogo cha bustani ikiwa inatumika kuotesha mmea kwenye chungu cha kuoteshea mimea. (Mwisho).

Maono:

Nilimwona mjusi fulani akiwa ameuzingira mwili wake wote kwenye kitu kama mwanga mweupe ambao unang’ara.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.