|
1477. Prophecy given to Raymond Aguilera on 8 March 2000 at 8:00 PM. I went with Carl to Marilyn's mothers' funeral. Marilyn goes to Carl's Bible study. As I sat in the chapel and prayed and watched the service, it reminded me of my father's funeral a few months ago. This one was totally different, for my father's funeral was held outside and Marilyn's mothers' funeral was held inside. Well, during my prayer time, I asked the Lord if there was any difference in His Eyes between my father's Christian funeral and Marilyn's mothers' Christian funeral or any other Christian funeral. I even asked if there was a difference - if the Christian's body was lost (like if a person is lost at sea or in an explosion where there is no body). Then the Lord said, "They are all the same. I love you Ray." (over) Vision: During prayer the Lord showed me this heavy all wooden cart. I could see that even the two wheels were made of solid wood. As I watched the wheels go around and around, I could see them bounce up and down, as they rolled over the unusually large stones that made up the stone street. (over) |
1477. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 8 Machi 2000 saa 2:00 usiku. Nilienda na Carl kwenye mazishi ya mama yake Marilyn. Marilyn ni mmoja wa washiriki wa kwenye kikundi cha kujifunza Biblia cha Carl. Nilipokuwa nimekaa kwenye Kanisa wakati wa ibaada ya mazishi ya marehemu mama huyo; nami huku nikiwa ninaangalia shughuli hizo na nikiwa ninaomba, ilinikumbusha mazishi ya baba yangu iliyofanyika miezi michache iliyopita. Ibaada hii ilikuwa ni tofauti sana na ile ya baba yangu kwa maana ibaada ya mazishi ya baba yangu ilifanyika nje ya kanisa na wakati ibaada hii ya mama yake Marilyn ilifanyika ndani ya kanisa. Naam wakati wa maombi yangu mimi nikamwuliza Bwana kama kuna tofauti yeyote katika mtazamo Wake kuhusu mazishi ya Mkristo ya baba yangu na ile ya mama wa Marilyn au ya Mkristo yeyote yule. Mimi pia hata niliuliza kama kuna tofauti yeyote – kwa mfano kama mwili wa huyo Mkristo umepotea (kwa mafano kama wale waliopotea baharini au katika mlipuko ambako mwili umetoweka). Kisha Bwana akasema, "Yote hayo ni sawa tu. Ninakupenda wewe Ray." (Mwisho). Maono: Wakati wa maombi Bwana alinionyeshea mkokoteni fulani mzito uliokuwa wa mbao tupu. Naona hata zile tairi zake mbili zote ni za mbao nzito. Nilivyozidi kuangalia zile tairi zikizunguka tena na tena, nilikuwa naona zikidunda kwenda juu na chini wakati zikiwa zinapanda na kushuka kwenye mawe ya barabara ya mtaa huo ambazo zilikuwa kubwa kwa kiasi ambacho hayakuwa ni ya kawaida. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )