|
1501. Occurrence given to Raymond Aguilera on 9 May 2000 at 6:30 PM. I have been working many hours on the computer and I was very tired. So I decided to lay down and rest. Once I was on top of the bed, I asked Eva to fix me something to eat, for I had not eaten much all day. So she went downstairs and I began to pray to the Lord about our finances. A few days ago, I had received a $1000 tax bill for the house, and I was about $850 behind on my monthly bills. I was tired and started to feel depressed. But when I was praying to the Lord, I remembered something about when you are weak in the body, you are strong in the spirit. So I began to pray to the Lord about my needs. All of a sudden my prayer language began to speak strong in the spirit and the Lord gave me a vision I had seen earlier. Then my prayer language began to get louder and louder and I began to see strange things. Then the Lord instructed me to raise my hands into the air and to keep praying. I felt like I was in some kind of spiritual war, but I was not sure because of the strange sounds coming from my prayer language. I could also sense this incredible Power flowing through my body as I prayed. Then I saw what looked like two dinosaurs opening their mouths, but I do not know, if they were evil spirits, but as I watched, their heads were cut off. Then the Lord instructed me to get up from the bed and to stand facing east. So I got up and faced east and prayed. Then the Lord instructed me to face south and pray. Then again I was instructed to face west and pray, and finally I was to face north and pray this very unusual prayer language. Then I was shown the visions below. Vision: I saw myself somehow in the spirit, but I was viewing myself from high in the sky. I could see myself walking through this tall grass swinging my sword and cutting a path through the grass, which was taller than I. As I watched myself from the sky, I could see in the distance a wall of fire moving toward me on my left side. I guess, I could not see it from the ground, because I just kept on cutting my path through the tall grass. As soon as the grass fire or the wall of fire got close to me, I noticed this invisible wall or wind appear between the moving firewall and myself. But I kept swinging my sword and moving forward and not knowing what was going on to the left of me. Vision: Then I saw this very, very large Tree with its roots coming down from Heaven. As I saw the Tree pass me, now I could the Tree below me, and I could see the base of the Trunk of the Tree. As I watched, I saw Lighting or an arc of fire separate the roots from the Tree. Then all of sudden the Tree began to spin in a circular motion, and the Tree changed into a whirlwind in the sky. Vision: Then I saw the Greek letters Alfa and Omega. Vision: Then I saw this Door to Heaven. But what was so strange was this Door shape looked like one of my house doors. This Door to Heaven was so CLEAN and pure White. I could not believe anything could be that clean and white looking. Then I saw this Golden Doorknob on the Door. The Doorknob was also very CLEAN and shiny yellow. I could not comprehend how CLEAN everything was. As I watched this, I noticed that the Golden Doorknob was being removed from the Door. Vision: Then I saw this Whirlwind again, but this time the Whirlwind had a whip somehow tied to the edge of it, and the extended whip spun around and around the outer edge of the Whirlwind. I could see the whip destroying everything that came in contact with it. It reminded me of one of those electric or gas driven weed-eaters that people use to cut grass. Vision: Then I saw a nuclear explosion. (over) |
1501. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 9 Mai 2000 saa 12:30 jioni. Mimi nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi kwenye kompyuta yangu, nami nilikuwa nimechoka sana. Kwa hiyo nikaamua nijilaze kidogo na kujipumzisha. Mara tu nilipojilaza juu ya kitanda changu, mimi nikamwomba mke wangu Eva anitengenezee chochote cha kula kwa maana kwa siku hiyo nzima nilikuwa sijala vizuri. Yeye akaenda kunitengenezea chakula, nami nikaanza kupeleka maombi yangu kwa Bwana kuhusu matatizo ya kifedha niliyo nayo. Kwa maana siku chache zilizopita nilipokea deni la kodi la Dola za Marekani 1000 kwa ajili ya nyumba, nami nilikuwa nimepungukiwa na Dola 850 kwa kulipa madeni yangu hayo ya mwezi. Mimi nilikuwa nimechoka na kuanza kujisikia kukata tamaa. Lakini wakati nilipokuwa ninamwomba Bwana, mimi nilikumbuka kuwa pale unapo kuwa umechoka sana kimwili, kwa upande wa kiroho una kuwa na nguvu nyingi sana. Kwa hiyo mimi nikaanza kumwomba Bwana kuhusu mahitaji yangu. Mara kwa ghafla maombi yangu ya lugha yakaanza kuomba kwa nguvu katika roho na Bwana akanipa maono yale ambayo niliyo kwisha kuyaona hapo mwanzoni. Kisha lugha yangu ya maombi ikaanza kuwa kubwa zaidi na zaidi, nami nikaanza kuona vitu ambavyo ni vya ajabu. Kisha Bwana akaniagiza kuwa ninyanyue mikono yangu juu hewani na niendelee kuomba. Nilijisikia kama niko kwenye mapambano fulani ya kiroho, lakini sikuwa na uhakika kwa sababu ya sauti hiyo iliyokuwa inatoka kwenye lugha yangu hiyo ya maombi. Nilikuwa naweza kuhisi Nguvu fulani ya ajabu kupitia mwili wangu, wakati nikiwa naomba. Kisha nikaona kitu kama wanyama wawili wa aina ya dinasorasi ambao walikwisha toweka kutoka dunia hii wakifungua midomo yao. Mimi sina uhakika kama walikuwa ni mapepo wachafu au lah, lakini wakati nikiwa naangalia vichwa vyao vilikatwa mara. Kisha Bwana aliniagiza niamke kutoka kitandani na niangalie mashariki. Kwa hiyo mimi niliamka na kuangalia mashariki na kuomba. Kisha akaniagiza niangalie kusini na kuomba. Kisha Bwana akaniagiza niangalie mangharibi na kuomba, na mwishoni nikaambiwa ni angalie kaskazini na kuomba kwa lugha hiyo ya ajabu ya maombi. Kisha mimi nikaonyeshewa maono yafuatayo hapo chini. Maono: Mimi nilijiona mwenye kwa namna fulani nikiwa katika ulimwengu wa kiroho, lakini mimi nilikuwa najiangalia mwenyewe kutoka juu angani. Nilikuwa najiona mwenyewe nikiwa natembea katikati ya majani marefu nikiwa ninazungusha upanga na kufyeka kinjia katika majani hayo, ambayo yalikuwa marefu kuliko mimi mwenyewe. Nilivyo kuwa ninajiangalia kutoka angani, nilikuwa naweza kuona kutoka mbali ukuta wa moto ukinijia kutoka upande wa mkono wangu wa kushoto. Nadhani mimi kwa pale ardhini nilikuwa sioni huo moto kwa sababu mimi nilikazania tu kufyeka kinjia changu kwenye majani hayo marefu. Mara tu moto huo wa majani au ukuta huo wa moto ulipo ni karibu mimi, mimi niliona ukuta wa upepo ulizuka kati yangu na huo ukuta wa moto ulio kuwa unakuja. Mimi hata hivyo niliendelea kuuzungusha upanga wangu na huku nikiwa ninasonga mbele bila kujua ni kitu gani kilicho kuwa kinanijia kwenye upande wa mkono wangu wa kushoto. Maono: Kisha mimi ni kaona Mti fulani mkubwa sana sana na mizizi yake yakiwa yanatoka juu Mbinguni. Mara nikauona Mti huo ukiwa uko chini yangu na kuona kitako cha shina lake. Nilipo kuwa ninauangalia Mti huo, nikaona umeme wa radi au cheche ya moto ya kuunganisha vyuma, ikaitenganisha Mizizi hiyo kutoka kwenye Mti wenyewe. Kisha kwa ghafla Mti huo ukaanza kujiviringirisha kwa usawa na kugeuka kuwa kimbunga angani Maono: Kisha mimi nikaona herufi za Kigiriki ya Alfa na Omega. Maono: Kisha nikaona Mlango huu wa Mbinguni. Lakini kile ambacho kilikuwa ni cha ajabu ni kuwa maumbile ya mlango huo ulikuwa unafanana na mmoja wa milango ya nyumbani kwangu. Mlango huo wa kwenda Mbinguni ulikuwa ni MSAFI sana sana na Mweupe. Mimi siamini kama kuna kitu chochote kinachoweza kuonekana kuwa kisafi na nyeupe kiasi hicho. Kisha mimi nikaona Kitasi cha Dhahabu kwenye mlanga huo. Na kitasi hicho nacho kilikuwa ni KISAFI SANA na iliyokuwa na rangi ya manjano inayo ng’ara. Mimi nilikuwa nashindwa kutafakari jinsi mambo yote yalivyokuwa masafi hapo. Nilivyo kuwa nayaangalia hayo nikaona kile Kitasa cha Dhahabu kikiwa kinaondolewa kutoka kwenye Mlango. Maono: Kisha mimi nikaona Kimbuga kile tena, lakini mara hii Kimbuga kile kilikuwa na kibogo cha kuchapia kilicho fungwa kwenye kilele cha kimbuga hicho, na kibogo hicho kikrefu kikawa kinazunguka tena na tena nje ya Kimbuga hicho. Mimi nilikuwa naweza kuona kimbuga hicho kikiangamiza kila kitu kinacho kutana nacho. Kilikuwa kinanikumbusha mashine ile inayoendeshwa kwa umeme au mafuta inayo tumika kukatia majani. Maono: Kisha nikaona mlipuko wa kinuklia. (Mwisho).
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )