229. Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 28 Oktoba 1992, saa 2:52 jioni katika lugha ya Kiingereza.
Kutawalishwa kwa Shetani kutatokea adhuhuri ya mchana (saa 6) wakati Kengele za (Kanisa la) Mt. Petro zitakapokuwa zinalia. Shetani atachukua mamlaka juu ya jeshi lake, juu ya mapepo wake na kwenda kulivamia Nchi Takatifu. Kwa maana njia za shetani ni njia za uovu, njia za ubaya.
Msijali. Msiogope. Kwa maana Yehova yuko hapo, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa maana Uweza, Nguvu na Utukufu una yeye Mungu Yehova, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu. Muwe imara. Muwe Mashujaa. Kwa maana Malaika wote wa Mbinguni wamejitayarisha kwa Mapambano kwa Vita. Kwa maana matokea yamekwisha kupangwa.
Muwe imara. Muwe na Ushujaa. Msiogope. Kwa maana mapepo hawana uwezo wowote, hawana nguvu yeyote, ila Neno la Mungu wenu, Mungu Yehova, Muumbaji wa Ulimwengu, wa Nyota, wa Dunia, Neno lake Lililo NENWA ni LA UHAKIKA! ILEMEKAMILIKA, UWEZA, na MAMLAKA! Ukuu wa Neno lake ni Upendo wa Binadamu. Kwa maana Upendo wa Yehova ni Mkuu. Uweza na Nguvu za Yehova ni Kuu pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu.
Msiogope. Simameni juu ya Mwamba wa Mwanangu, Yesu Kristo wa Nazareti. Muwe Imara. Muwe na Ushujaa. Hivyo ndivyo asemavyo Yehova, Baba, Muumbaji wa Neno la Kunenwa ambalo limeumba kila kitu. Hakuna lolote lililowahi kuwapo, lililowahi kuundwa lililokuwapo bila kuumbwa kwa kupitia Neno lililo Nenwa la Yehova Mungu. NAIWE HIVYO NA IWE HIVYO!
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza
kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )