236. Vision and Occurrence of Raymond Aguilera on 27 November 1992 at 11:37 PM

Occurrence:

I was having Communion with a friend, when all of a sudden I started having a vision of tables with white tablecloths. They were placed in a circle, enough tables to seat thirty to fifty people. They had torches burning at each table. The people were in all white uniforms and hoods like what the Ku Klux Klan wear. They were all standing behind their tables in a circle chanting, or something, and in the center of this large circle of tables there was a drawing of a star with a circle around it.

I stopped having Communion, and I got up from the table where I was, and went in the living room and started to pray, because the Lord said they were praying against me.

The Lord said "Go back and finish having Communion with your friend." Then after Communion the Lord said, "Now go pray against them."

So after we finished Communion, my friend and I started to pray on the living room floor against this ceremony. I don't know how long we prayed against it, maybe twenty minutes, but after this time of prayer each person that was around this circle of tables got up in a single file and went out the door.

This whole event didn't last very long. Then the Lord revealed to me, the reason for my fasting and praying for two days. I guess He knew they were going to pray against me at twelve midnight, that evening. It's unbelievable to me this whole occurrence, the vision, the revelation of what was going to happen. I didn't have a clue to the reason of my fasting and praying, but I obeyed that quiet soft little voice.

I wasn't sure why I did, but I just knew, I had to fast and pray. I had the same impression on both days, so I fasted and prayed. It wasn't until the end of the second day, almost at midnight that the Lord revealed the reason during Communion prayer. He said He would protect me, and so far He has. I just don't understand the ways of the Lord. That's all.

236. Maono na Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 27 Novemba 1992, saa 5:37 usiku.

Matukio:

Nilikuwa nashiriki meza ya Bwana (komunio) na rafiki yangu fulani, ndipo kwa ghafla nilipoanza kuona maono ya meza zilizo kuwa zimefunikwa kwa vitamba vyeupe. Zilikuwa zimewekwa katika mviringo, meza za kutosha kukalisha watu thelathini hadi hamsini hivi. Zilikwa na taa zilizokuwa zinawaka kwenye kila meza. Watu wale walikuwa wamevaa nguo za sare nyupe zilizokuwa na kofia kama zile zinazovaliwa na jamii ya "Ku Klux Klan" (ambao ni wabaguzi wakubwa wa rangi Amerika). Wote walikuwa wamesimama nyuma ya meza zao katika mviringo wakiimba, au wakifanya kitu fulani, na hapo katikati ya kwenye mviringo huo mkubwa; kulikuwa na mchoro wa nyota na mviringo uliokuwa umeuzunguka.

Mimi niliacha kupokea Komunio, nikatoka kutoka kwenye meza pale nilipokuwapo na nikaenda sebuleni kisha nikaanza kuomba, kwa sababu Bwana aliniambia wao walikuwa wanasali kunilaani.

Bwana akasema, "Rudi ukamalize kushiriki kwenye Kumunio pamoja na rafiki yako." Kisha baada ya kumaliza kupokea Bwana akaniambia, "Sasa nenda ukaombe kuwapinga."

Kwa hiyo baada ya kumaliza kushiriki Komunio hiyo, Mimi na rafiki yangu tulianza kuomba pale kwenye sakafu ya sebuleni kupinga sherehe yao hiyo. Sielewi tuliomba kwa muda gani kuwapinga wao, labda kitu kama dakika ishirini hivi, lakini baada ya muda huo wa maombi kila mtu (aliyekuwa kwenye sherehe yao hiyo) alinyanyuka na kuanza kuondoka katika mstari mmoja kupitia mlangoni.

Tukio hili lote halikudumu kwa muda mrefu sana. Kisha Bwana akanifunulia mimi; sababu ya mimi kufunga na kuomba kwa siku mbili. Nadhani Yeye alijua kuwa wao wangeli kuja kufanya maombi ya kujaribu kunilaani usiku wa manane, jioni ile. Lilikuwa jambo ambalo kwangu mimi ni vigumu kuliamini na ni kitu cha ajabu kweli kwangu; kuhusu tukio hilo lote na maono na mafunuo ya yale ambayo yangelienda kutokea. Mimi nilikuwa sijui sababu ya Mimi kufunga na kuomba, ila nilitii ile sauti ya ukimya nyembamba na ndogo.

Mimi sikuwa na uhakika wa kwanini nilifanya hivyo, lakini mimi nilijua tu kuwa, lazima nifunge na kusali. Nilikuwa na hisia hiyo hiyo kwa siku zote mbili, kwa hiyo nilifunga na kusali. Haikutokea kitu hadi siku ile ya pili jioni kabisa karibu na usiku wa manane, ndipo Bwana aliponifunulia sababu ya kufunga na kuomba wakati ule wa sala ya Komunio. Yeye alisema angenilinda mimi na kweli hadi hapa amekuwa akinilinda. Kwa kweli mimi sielewi njia za Bwana. Hayo ni yote.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.