252. Unabii na Maono aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 15 Desemba 1992, saa 2:46 jioni katika Lugha ya Kihispaniola.

Maono:

Naona maono ya aina ya glasi ya zamani ya kunywea mvinyo wa aina "shampeine".

Unabii:

Kisha Bwana akasema: "Mbegu, je, mnajaribu kuniambia Mimi nini? Mimi nitawasikilizeni kwa masikio Yangu, kwa Moyo Wangu, kwa kila kitu kile ambacho ni cha Mbinguni. Mimi nitasikia maombi yeni. Nitasikia machozi yenu. Siku inakuja ambako kila kitu mnachokijua, kila kitu mnachokigusa kitabadilika. Kwa maana kila kitu kilicho kichafu siyo Changu, ila tu kile kilicho Kisafi, na vitu vya Dunia ni vichafu…. Siyo visafi. Mimi nawaelezeeni ninyi kwa machozi ya yale yatakayotendeka, na ni karibu sana. Mimi najua kile ulichonacho Moyoni. Mimi najua kile ulicho nacho kwenye mawazo yako, lakini Mimi nataka wewe uharakishe na kuweka katika kompyuta yako kila kitu kile ninacho kuambia wewe kwa njia ile ninayokuambia."

Kwa maana mwanangu mambo yataenda kubadilika na yanaenda kubadilika kwa kasi sana, na Mimi nataka Watakatifu, Mbegu Yangu, Kondoo Wangu, wasikie Neno la Mungu. Mimi na pendezwa na kufunga kwako, Mimi na pendezwa na maombi yako. Napendezwa na kule wewe kunitafuta Mimi, kule kunitafuta kwa Moyo wako wote, kwa akili yako yote. Hiyo ndiyo njia na mambo ya Mungu, kwa wewe, weka kila kitu mbele ya Msalaba. Wewe anguka kwenye magoti yako na uombe, na uombe, na uombe na ufunge na ufunge. Nauombe kwa machozi ya roho yako. Hiyo ndiyo njia ya Mungu. Hiyo ndiyo namna na tabia ya Watakatifu Wangu, Mbegu Yangu, na Kondoo Wangu.

Kila kitu kile nilichokuambia wewe kuwa; nitaenda kukupa wewe, Mimi naenda kukupa wewe, na zaidi na zaidi. Kwa maana wewe unanipenda Mimi; kwa moyo wako. Kwa maana wewe unafanya kile ninachokuambia. Unalia, na kulia, na kulia, lakini unafanya, kwa machozi ya Mbinguni, kwa Machozi ya Mwanangu, na Roho Mtakatifu, na Baba yako. Wewe unafanya kile Mimi ninachokuambia wewe. Mimi najua wewe hujui mambo ya Mbinguni, lakini Kondoo, Mbengu, ambao wanafanya kile ninachowaambia kwa Imani ya Mbinguni, kwa Imani ya Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, Mimi nitawalinda wao. Mimi nitawalinda kwa kutumia Malaika. Mimi nitawalinda kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mimi nitawalinda kwa njia ya Mwana. Mimi nitawalinda kwa maana; Mimi ni Baba na Mimi nalinda kile ambacho ni Changu.

Usijali kuhusu hatua unayofanya, kwa maana hatua zako ni hatua Zangu, ni hatua za Mbinguni, andika na uweke kwenye maandishi kila kitu ninacho kuambia wewe, kwa moyo wako wote. Kwa maana Neno langu ni Neno la Mbinguni; ni Neno la Mungu wako, na hakuna mtu yeyote awezaye kuzuia Neno la Mungu. Meza kila kitu kinachokupa hofu. Kwa sababu Mungu wako wa Mbinguni, wa Duniani, wa Nyota pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu wako upande wako. Yeye anatembea pamoja na wewe, Mkono kwa Mkono.

Usipoteze subira yako; kwa maana Mimi najua yajayo kabla hata hayajaja. Wewe uko imara, Reymundo. Najua wewe unaamini kuwa huna nguvu, lakini Mimi nasoma moyo wako na moyo wa rafiki yako pia. Yule anayekuombea usiku na mchana. Yule anayelinda mwili wako kwa maana anampenda Mungu wa Mbinguni. Mimi ninakulinda na Ninamlinda huyo rafiki yako pia. Kwa maana ninyi wawili mna moyo wa Mungu na ninyi wote wawili mnalia kwa machozi. Kwa maana ninyi wote wawili hamjui vile vitu mnavyo vihitaji kuvijua, na shetani amewakasirikia sana ninyi. Kwa maana ninyi nyote wawili mmediriki kuomba kwa Mungu wa Mbinguni, pamoja na Baba, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Yeye amekasirika, lakini msiogope kwa maana Mimi niko pamoja nanyi nyote wawili.

Watoto Wangu wa Kiume na wa Kike, Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Kila mtu wa Dunia hii. Mnisikilize Mimi. Huyu ni Baba yenu. Baba yule aliyeumba kila kitu, kila kitu unachokigusa, kila kitu unachokiona, kila kitu unachokihitaji. Yeye alifanya kila kitu, kwa Neno.

Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Fungueni Macho yenu! Kwa maana kila kitu cha dunia, kila kitu ukionacho, kila kitu unachokigusa kinaenda kubadilika. Kinaenda kubadilika kwa haraka sana. Kwa maana shetani yuko huru, anarandaranda kama mbwa mwenye njaa. Ataenda kutaka kuwala Kondoo wa Mwanangu, Mwili wa Mwanangu. Kwa maana kila kitu cha mbwa ni kichafu. Na kila kitu cha Mwanangu ni Kisafi.

Mimi nataka ninyi mjikusanye. Mimi nataka ninyi muache kugombana. Mimi sitaki ninyi mpigane makanisani. Kwa maana makanisa yote yana maneno ya binadamu, na hawana Neno la Mungu. Mimi nataka ninyi mbadili namna mnayofikiria. Mimi nataka ninyi mkamtafute Mwanangu kwa Moyo, kwa akili, kwa kila kitu kile mlichonacho. Kwa maana shetani yuko huru naye anakuja na njaa, kwa meno, kwa ulimi, ulioloana kwa tama ya damu ya Kondoo, ya Mbegu.

Mimi nawaambieni ukweli! Kwa maana Nabii Wangu Reymundo, ni Neno Langu. Mimi ninawaambia ukweli. Mimi ninawaambia ukweli. Mimi ninawaambia kwa Machozi kwa maana kama hamlisikii Neno Langu, ninyi mtaenda kuteseka. Mimi ninawaambia ukweli. Kwa maana Mungu wenu wa Mbingu, wa Dunia, pamoja na Mwana, na Roho Mtakatifu hawadanganyi.

Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Mnisikilize Mimi! Huyu ni Baba yenu, yule aliyefanya kila kitu, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu. Fungueni Macho yenu, Fungueni Masikio yenu! Someni Biblia! Watafuteni kaka zenu na dada zenu. Wale ambao hawana chochote, wale ambao wananjaa, wale wanaohitaji Neno la Mungu, na mtubu, mtubu, mtubu dhambi zenu. Mimi nitawasikia kwa masikio Yangu. Kwa maana Macho Yangu yanaona kila Kitu.

Nifanyieni hisani, Makanisa ya duniani inabidi waache kugombana. Dakika hii! Kwa maana ugovu sio wa Mungu. Ugomvi ni wa shetani, kama unacho kitu cha kugombania ndani ya moyo wako na ndugu zako wa makanisa mengine wewe siyo Wangu. Wewe ni wa shetani na Mimi naenda kukuacha na kukukabidhi kwa shetani. Kwa maana kinachogombana sicho cha Mungu. Iwapo wewe hutaki kanisa fulani kwa sababu walikufanyia uovu. Kwa maana neno wanalo sema siyo neno lako, na kuna ugomvi. Hapo wewe siyo Wangu! Kwa maana wewe unaye Mungu wako ndani ya sanduku au boksi, na wao wana Mungu wao katika sanduku au boksi.

Huna chochote cha Mungu. Huna chochote cha Baba, cha Mwana na Roho Mtakatifu. Wewe ni wa shetani na kwa Midomo Misafi; Mimi nakuambia ukweli, "Mimi nakuambia kwa uwazi na kwa uhakika!" Kwani Mimi naenda kukukabidhi wewe kwa shetani kama wewe hutasafisha tabia, mawazo ya ugomvi.

Mimi nawaambia ninyi, ninyi Wachungaji. Wale wanaodhania wanajua yote. Yote mliyo nayo katika akili zenu, katika midomo yenu, ni kugombana kwa maneno, kwa namna ile ambayo mnaitumia, katika Jina la Mwanangu, kugombana, na kugombana, na kugombana. Mimi ninawaambieni ninyi. Mimi nitaenda kuwakabidhini ninyi kwa shetani. Mimi naenda kuwapeni yeye kwenu, na kisha nitaondoka nielekee upande mwingine.

Mimi ninawaambieni, na ninawaambieni, na ninawaambieni, na ninyi mnaweka mikono yenu juu ya macho yenu na masikio yenu. Na ninyi mnagombana, na kugombana kwa maneno, kwa pointi ile mnayoamini kujua, lakini Mimi ninawaambia dakika hii yakua ninyi hamjui chochote.

Kwa Midomo Yangu Misafi, kwa Midomo ile inayosema kila kitu ambacho kimeelekezwa Mbinguni, mtaenda kujipeleka ninyi wenyewe, ninyi peke yenu, pamoja na shetani. Kwa maana Mimi naenda kugeuza Mgongo Wangu. Kwa maana kitu kinacho gombana sicho cha Mwanangu, sicho cha Roho Mtakatifu, sicho Changu!

"Mimi nataka ninyi mjisahihishe wenyewe kwa tabia. Sasa hivi! Dakika hii!" Kwa maana wachungaji wa Mwili wa Mwanangu; wanafanya kwa njia ya kishetani. Hawafanyi kwa njia ya Mwanangu. Yote wanayofahamu ni kugombana. Angalieni kwa makanisa yote mliyonayo, maneno mliyonayo.

Ni aibu gani! Ni aibu gani! Ni aibu gani! Msije mkasema kuwa Mimi sikuwaambieni ninyi. Angalieni ndani ya Biblia na muone kuwa nilichokisema kama haikutokea. Kwa maana Mungu wenu hadanganyi, na kama nikiwaambia kuwa nitawapelekeni shimoni kwa ajili ya ugomvi wenu, na familia ya Mwili wa Mwanangu, Mimi nitaenda kuwapelekeni ninyi kwa uhakika.

"Hili ni jambo la uhakika!" someni Midomo Yangu! "Mimi nitaenda kuwapelekeni ninyi kwenye Shimo." Iwapo kama hamtaacha ugomvi wenu na Kondoo, na Mbegu. Kwa maana Mimi ninaona kila kitu. Mimi naona Mioyo yenu. Naona mawazo yenu. Najua kuwa ninyi mnachotafuta ni fedha. Fedha hiyo itawapatieni Shimoni. Yote fedha hiyo inayofanya ni kuwanunulieni nyumba kule shimoni. Mimi nitawapelekeni pale pamoja na shetani wenu, kwa maana ninyi hamkuwatafuta kondoo Wangu, Mbegu Yangu. Ila ninyi mliamua kujaza tu matumbo yenu kwa fedha za shetani. Mimi ninawaambieni kwa uwazi na kwa uhakika.

Huyu ni Mungu wenu, Baba, pamoja na Mwana, pamoja na Roho Matakatifu. Someni Midomo Yangu! Someni Midomo Yangu! Someni Midomo Yangu! Someni Biblia. Someni ndani ya Biblia, katika maeneo nliyosema yakuwa vitu vitatokea, kama nilivyosema. Katika siku hii ya leo, katika dakika hii, Mimi ninawaambieni kile ambacho kinaenda kutokea kwenu!! Mimi siongei kuhusu kaka zako na dada zako. Dakika hii ninaongea na wewe! Je, mmenisikia Mimi ninyi Wachungaji? Maneno haya ni kwa ajili yenu. Mimi sijali kama mnayapenda au hamyapendi. Onyo hili ni kwa ajili yenu. Mimi nataka muache ugomvi dakika hii!

Amasivyo Mimi nitawaachieni kwa shetani naye atawapelekeni kwenye Shimo. Mimi nitaenda kulia, na kulia. Kwa maana nitakuwa nimewapotezeni ninyi, lakini kwa dakika hii, Mimi ninawaambia kwa Midomo Yangu, ukweli. Je, Mmenisikia Mimi? Je, masikio yenu na macho yenu yako wazi? Mimi najua…….Kwa maana Mimi nasoma Mioyo yenu dakika hii. Mimi najua ……. Mlicho nacho Mioyoni mwenu, akilini mwenu. Najua …. Wengine wemeogopa, wengine wamekasirika, lakini Mimi sijali kama mmekasirika au mmetishika.

Kwa maana lile Neno Langu lililonenwa, litaenda kutokea. Mimi ninautayarisha Moyo Wako dakika hii ya sasa. Kwa maana Mimi ninasoma kila kitu na wewe unajua ndani ya moyo wako dakika hii, kwa maana Mimi naiweka "yakuwa wewe unajua" yakuwa Mimi naenda kukupeleka wewe shimoni. Neno hilo ni kwa ajili yenu, ninyi Wachungaji. Ombeni na ombeni, iwapo mtaomba kwa usahihi, Mimi nitakuambieni. Mimi nitakuambieni kwa Midomo Yangu yakuwa; Mimi nitawapelekeni Shimoni. Kwa maana Mimi sidanganyi. Iwapo kama hamtajutia njia zenu dakika hii, kwa Nguvu za Roho Mtakatifu, Mimi nitawaonyesheeni njia ya Mungu. Kwa maana Mimi ni Mungu wa yote pamoja na Mwanangu, na Roho Mtakatifu. Mimi naenda kuwatisheni. Mimi naenda kuwapelekeni shimoni. Kwa ajili ya ugomvi wenu, kwa ajili ya fedha, kwa ajili ya njia zenu, kwa maana njia zenu ni njia za kishetani.

Je, mmenisikia Mimi? Kwa machozi, kwa machozi Mimi ninawaambia. Kwa maana Mimi ninawapendeni ninyi kwa Moyo Wangu wote! Lakini Dunia ni Yangu, siyo yenu. Mimi ni Mungu, lakini ninyi siyo, na kile Mimi ninachokisema ndicho kile kitakachotokea. Je, mmenisikia Mimi? Mimi ni Mungu, lakini ninyi siyo chochote. Ninyi ni vitu vya shetani. Kumbukeni kile ninachowaambieni, kile unamnacho kisoma pamoja na Nabii Wangu Reymundo. Kwa sababu Mimi najua kuwa mnaenda kukasirika sana, lakini Mimi sijali.

Kwa maana Mimi nakilinda kile ambacho ni Changu, na iwapo unataka kufanya kitu chochote, Mkono Wangu ni mzito, na Mkono Wangu unajua wewe ulipo. Kwa maana huwezi kijificha na wala shetani hawezi kukulinda, kama Mkono Wangu ukiamua kukutwanga. Je, umenisikia Mimi? Huyu ni Mungu wenu wa Mbinguni, wa Dunia, pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu. Mimi ninawaambieni ukweli. Kwa maana tazama huo unakuja ule mwisho wa yote, na nanyi mna njia zile za shetani na Kondoo Wangu wanahitaji kusikia Neno la Mungu. Lakini Kumbukeni, Mimi ninawapendeni kwa Upendo Wangu, kwa Upendo wa Mbinguni. Hayo ni yote nitakayowaambia kwa dakika hii.

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.B.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza vitabu vya unabii Bonyeza kwenye picha ya kitabu hapa chini

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiwa


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.