410. Matukio yaliyopewa Raymond Aguilera tarehe 27 Februari 1994, saa 3:30 asubuhi.

Wakati wa misa kaninsani Bwana aliniambia nipige hema na kufanya kambi na nilale humo. Hii iliniogopesha kwa sababu kule nje mawingu yalikuwa yanaonekana kana kwamba kungelikuwa na dhoruba kubwa sana saa za alfajiri ile. Bwana akaniambia nimpe dola tatu kwa yule misionari msichana mpya pale kanisani. Yote niliyokuwa nayo ilikuwa ni dola nne tu, hivyo maana yake nibakiwe na dola mmoja kwa ajili ya mafuta ya kwenda nyumbani, kwa maana sikuwa na mafuta. Nilikuwa nahisi kuwa Bwana angenipatia fedha za kuziba pengo hilo. Kama kawaida yake, mimi nilikuwa na mashaka yangu hivyo nikaomba udhibitisho kwa sababu hali ya hewa ilikuwa haionekani kama ni nzuri.

Kwa sababu ya mapambano niliyokuwa nayapata siku za hivi karibuni sikujua kama maagizo hayo yanatoka kwa Bwana au kwa shetani. Kwa hiyo mimi nikaomba Bwana anipe udhibitisho na Bwana akawa anaendelea kuniambia kuwa anataka mimi nipige hema na nilale humo. Kwa hiyo wakati mimi nilipokuwa naenda nyumbani na gari bado nilikuwa na mashaka yangu, na Bwana akawa anaendelea kusema, “fanya hivyo, piga kambi nje na nilale humo kwenye hema.” Lakini hadi wakati ule nilipofika nyumbani nilikuwa nimeridhika kuwa hata kama agizo hilo haitoki kwa Bwana au kama inatoka kwa Bwana, kwa vyovyote Yeye bado angelinilinda mimi.

Kwa hiyo wakati nilipofika pale nyumbani baada ya misa, mimi nikaharakisha kuanza kupiga hema yangu pale nje kabla dhoruba ile haijaanza. Kwa maana mimi nilitaka nipige hema yangu hiyo kabla ya ile dhoruba niliyokuwa ninaitarajia. Wakati nilipoanza kuunganisha hema yangu nikaanza kutafuta matofali ya kushikilia sehemu kipande cha juu au shiti ya juu ya kuzuia maji yasivuje ndani ya hema langu kama kwa bahati mbaya hema yangu ikianza kuvuja kutokana na mvua. Wakati nilipoanza kutafuta matofali ya kushikilia mwisho wa hema langu na kuyakusanya kwa mshangao wangu nikaona karibu na tofali mmojawapo noti mbili za dola mmoja kila mmoja ardhini, karibu na tofali hilo.

Ilinishangaza kweli kwa sababu Bwana alikuwa amenisisitizia kuwa, “Yeye angelifidia fedha zangu hizo kama mimi nitampatia yule msichana mmisionari pale kanisani.” Kwa hiyo mimi niliweka matofali yale kwenye hema yangu na kuendelea kutafuta matofali zaidi. Kisha nikapata noti ya tatu ya dola mmoja ardhini karibu na tofali lingine. Wakati nilipoona dola hizo ya tatu mimi nilishangzwa na kushutushwa sana, kwa maana Bwana ametoa tena. Mwanzoni nilitaka kuuliza wale tunaoshirikiana chumba changu kuuliza kama wamepoteza dola tatu lakini nilikumbuka kuwa Bwana alinisisitizia kuwa angenirudishia fedha zangu hizo nitakazozitoa kwa yule mmisionari. Kwa hiyo siku mwuliza yeyote wa wale ninaoshirikiana chumba hivyo mimi nikachukulia kuwa ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Bwana, kwa maana mimi nilikuwa nimeishiwa kabisa.

Kwa hiyo mimi nikakamilisha kujenga hema yangu na kisha nikaenda nyumbani, na kulala. Mimi nilikuwa nimechoka kwa sababu nilikuwa nikishughulikia Kitabu cha Unabii usiku kucha. Baadaye mchana ule wakati mimi nilipoamka nakuendelea kushughulikia Kitabu changu kile cha Unabii, mimi niliona hali ya hewa ikibadilika na mawingu ya ile dhoroba ikawa imetoweka kabisa.

Ni jambo la kushangaza jinsi Bwana anavyo kujaribu. Yeye atakulinda siku zote anakulinda wewe, lakini yeye anataka wewe uwe mtii katika mambo yote. Mimi nilijisikia kuwa niandike jambo hilo, kwa maana ni mmoja ya mambo hayo madogo madogo ambayo yamekuwa yakitokea, lakini yamenisaidia kunijengea imani yangu katika Bwana kwa maana mimi ninajua kutakuwa na majaribu mengi zaidi na mateso mbele yangu.

Ilani: siku iliyofuata niliwahi kumwuliza mmoja wa wale tuliyekuwa tunashirikiana chumba kama alipoteza fedha yeyote na yeye akasema ndiyo. Kwa hiyo mimi nikampa hizo dola zangu tatu nilizoziokota, lakini "Mimi bado ninakushukuru Bwana kwa ajili ya maagizo yako ya upendo. Mimi ninakupenda. Amina."

Bwana kwa kweli aliagiza tupige kambi hapo kwa siku mmoja tu, lakini mimi nilipiga kambi hapo kwa siku tatu ili kudhibitisha kama mimi naweza kuwa mtiifu.


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.