|
425.
Occurrence, Vision, and Prophecy given to Raymond Aguilera on 5 April 1994
at
9:00 AM.
in English.
A Christian Brother called me and said that he felt we had to go to Mt. Tamalpais, and anoint the top of the mountain with oil. So the next day after breakfast, we left and prayed all the way to the top of the mountain. Once there we parked in the parking lot, had Communion, anointed each other with oil, and prayed for the location that the Lord wanted anointed. So after the parking lot prayer we started walking on the path that circled the top of the mountain, and prayed in tongues as we walked in the spirit. I also heard my Christian friend praying the Twenty Third Psalms as we proceeded. Then about one third of the way around the top of the mountain we walked into some people sightseeing. We waited for them to move on, for we were praying out loud in tongues. For some reason, I said to my Christian brother, "Let's wait here." So we climbed on top of these rocks, to the one side of the path, and waited until the people in front and behind us moved on. We sat there for ten to fifteen minutes praying and looking at the scenery, in the direction of San Francisco. Then as we started to leave, my Christian friend looked to the top of the mountain and said, "I think you should climb to the top of that large rock and place some oil on it." Since my friend didn't bring the right clothes or shoes for climbing I had to try to climb this by myself. This large rock was almost vertical and very difficult to climb. I tried the best I could, but it was just too steep to carry this glass bottle of oil in one hand and try to climb with the other, and I was afraid of falling and breaking the bottle of oil. Then my friend noticed another way around the large boulder with a possible way to the top. So I struggled up, in between these large rocks, and found another boulder higher, behind the one we first saw, and sensed that this was the rock that should be anointed. This newly found path also had a way of reaching the top of this higher boulder. So I proceeded to the top of this second boulder, to the peak and onto the ledge of this cliff, overlooking the east bay. Once I reached the top, I sat on it, and could see all over the east bay. I was facing Mt. Diablo from the Mt. Tamalpais direction. After taking in the sights of the east bay, I started to pray and sensed that this was the real location that had to be anointed. So I anointed the rock in the name of the Father, the Son, and the Holy Spirit, in a shape of a cross, with the oil which quickly changed into a big blob of oil. Then the Lord said, "Dump it all, and turn the bottle upside down and drain all the oil onto the rock." The only problem was there wasn't any place to turn the bottle upside down. Then as I looked, I noticed a perfectly round hole, on top of this solid rock, exactly the same size as the bottle of olive oil. It wasn't a crack in the rock, but a natural hole carved into the solid rock. So I turned the bottle of olive oil upside down, into this hole, and let it drain. Now the bottle could not roll off or slide off, so I left the bottle there draining upside down. I had a sense, in the spirit, that the Lord had made this hole just for this bottle of olive oil, no telling how many hundreds of years ago. So I left the bottle there and climbed my way down the cliff, onto the path, where my friend was standing. He asked me, "Where is the bottle?" So I repeated what the Lord had said, and told him how this whole thing was so strange, from the direction the rock was facing the east bay, to how this place was found, to the hole in the rock to hold the bottle of oil. As we talked, I told him of the two visions I had while we were waiting, on the side of the path, for the people to walk by.
|
425.
Matukio, Maono, na Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 5 Aprili 1994,
saa 3:00 asubuhi katika lugha ya Kiingereza.
Ndugu yangu fulani katika Kristo alinipiga simu na kusema kuwa anahisi kuwa inatubidi tuende kwenye mlima Tamalpais, na kuweka kilele chake mafuta. Kwa hiyo siku iliyofuata baada ya kifungua kinywa, sisi tulienda huku tukisali hadi kwenye kile cha ule mlima. Mara tulipofika tu juu ya kile kile cha mlima; tuliegesha gari letu, tukala chakula cha Bwana au tulikomunika na kujipaka mafuta na kisha tukaomba ili tujue mahala pale ambako Bwana anataka tukapaweke wakfu kwa kuiwekea mafuta. Kwa hiyo sisi baada ya maombi pale kwenye eneo la kuegeshea magari, tuliendela kwa miguu kukwea kwenye kilele cha mlima ule kwa kupitia njia ya miguu iliyokuwa inauzunguka mlima ule, huku tukiomba katika lugha kwa sauti wakati tukiwa tunatembea katika roho. Mimi pia nilimsikia huyo ndugu yangu katika Kristo akisali kwa kufutatilia Zaburi ya ishirini na tatu wakati tulipokuwa tukiendelea na safari yetu. Kisha tulipokuwa tumefika kiasi cha theluthi mmoja ya safari yetu ya kukwea kwenye kilele cha mlima ule; tuliwafikia watu waliokuwa nao wanakwea kwenda juu kileleni kwa ajili ya ziara ya kuona kulivyo huko juu. Ilibidi tuwangojee ili watutangulie kwa maana sisi tulikuwa tukiomba katika lugha kwa sauti. Kwa sababu nisizozifahamu mimi nikamwambia yule ndugu yangu katika Kisto kuwa “Ebe tungoje hapa.” Kwa hiyo sisi tulikwea juu ya miamba hiyo, kwenye upande mmoja wa njia ile, tukawangoja watu wote waliokuwa mbele na njuma yetu wapite na kusonga mbele zaidi. Sisi tulikaa mahala pale kwa dakika kumi hadi kumi na tano hivi; tukiwa tunaomba na kuangalia maeneo yale yaliyokuwa yanayazunguka mahala pale, kutoka upande wa San Fransisko. Wakati tulipoanza safari yetu tena; kwa ghafla yule rafiki yangu akaniambia kuwa, “Mimi nadhani ni vyema kama wewe utakwea juu ya mwamba ule na kuweka mafuta juu yake.” Kwa vile yule rafiki yangu huyo hakuwa na nguo na viatu vinavyofaa kwa kukwea kwenye mwamba huo, hivyo ikanibidi mimi peke yangu nijaribu kupanda kwenye mwamba huo. Mwamba huo mkubwa ulikuwa ni kama uko wima kabisa hivyo ulikuwa mgumu kabisa kuukwea. Mimi nilijitahidi kuukwea ila ulikuwa ngumu sana; kuukwea kwa mkono mmoja na kwa mkono mwingine niwe nimechukua kile kichupa cha mafuta, nilikuwa nimeogopa nisije nikateleza nakuanguka na kuhatarisha kuivunja chupa ile. Ndipo kwa bahati rafiki yangu yule akaona njia njingine kwa upande wa nyuma wa mwamba huo ambako ni rahisi kuitumia kuukwea mwamba huo hadi juu. Kwa hiyo nikajaribu njia hiyo ya pili; na kungundua kuwa katika ya miamba hiyo mikubwa kulikuwa na mwamba mwingine ulionyanyuka kwenda juu zaidi, nyuma ya ule niliouona hapa mwanzo ndipo nikapatwa na hisia kuwa hapo ndipo mahala ambapo mimi ninatakiwa kupawekea wakfu kwa mafuta. Njia hii mpya ambayo tuliigundua ilikuwa pia na njia ya kukwea juu zaidi hadi kwenye kilele cha ule mwamba wa pili. Kwa hiyo mimi niliendelea hadi kwenye kilele cha mwamba ule wa pili uliokuwa mrefu kushinda miamba mingine yote hapo, hadi kwenye ukingo wa juu kabisa ambao ulikuwa unaangalia maeneo ya upande wa mashariki wa ghuba ile. Mara nilipowasili kule juu ya mwamba huo wa pili; mimi nilikaa juu yake, na nikawa naweza kuona maeneo yote ya mashariki ya ghuba ile. Ulikuwa unatazamana na Mlima Diablo kutoka upande wa Mlima Tamalpais. Baada ya kuangalia maeneo ya upande wa mashariki kutoka kwenye mwamba ule mimi nilianza kuomba na kupatwa na hisia kuwa eneo hili haswa ndiyo inayopaswa kuwekwa wakfu kwa kumiminiwa mafuta. Kwa hiyo mimi nikapaweka mahala pale wakafu kwa kupamwagia mafuta kwa Jina Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu katika umbo la msalaba kwa mafuta ambayo yalibadilika ghafla kuwa na umbo la matone matone ya mafuta. Kisha Bwana akasema “Yamimine yote kisha elekeza mdomo wa chupa chini na ili umwage mafuta yote juu ya mwamba huo.” Tatizo pekee lililokuwapa hapo lilikuwa ni mahala au sehemu pakuweza kuiwekea hicho kichupa kichwa chini, kwa kuwa palikuwa ni mwamba mtupu. Kisha hali nikiwa na angalia hapa na pale kuona kama kuna mahala ambako ningeliweza kupapata nikaona shimo fulani ambalo lilikuwa limetengenezwa likiwa ni ya mviringo ambao unawenza kutumbukia chupa ile bila ya shida juu ya mwamba huo, hakiuwa ufa katika mwamba ule, ila ilikuwa ni shimo ambalo limechongwa vizuri kwenye mwamba huo. Kwa hiyo mimi niliigeuza chupa ile kichwa chini kwenye, na kuiacha mafuta yale yamiminike ndani yake. Kwa hiyo chupa ile ilikuwa haiwezi kuanguka au kuviringika, kwa hiyo mimi niliiacha ile chupa kichwa chini ili mafuta yale yamiminikie ndani ya shimo lile. Mimi nilikuwa na hisia katika roho ya kuwa Bwana alikuwa amefanya shimo hilo kwa ajili tu ili hiyo chupa ya mafuta ya mizeutini iweze kuwekwa hapo kichwa chini, hakuna ajuaye kwa miaka mamia mingapi iliyopita. Kwa hiyo mimi niiacha chupa ile pale kwenye shimo hilo nikaanza safari ya kutelemka kutoka kwenye mwamba ule kuelekea kwenye kile kinjia, mahala pale alipokuwa amesimama yule rafiki yangu. Yeye aliniuliza mimi akisema, "ile chupa iko wapi?" Kwa hiyo mimi nikamkariria kile ambacho Bwana alichoniambia, na nikaendelea kumweleza jinsi mambo haya yalivyokuwa ya ajabu sana kwa jinsi uelekeo wa mwamba ule ulivyokuwa unauelekea upande wa mashariki wa ghuba ile na jinsi mahala hapo ilivyopatikana, na kuhusu shimo lile kwenye mwamba ule; ilikuwezesha kusimamishwa chupa ile ya mafuta kichwa chini kama Bwana alivyoagiza. Wakati tulipokuwa tukiyaongelea mambo hayo, mimi nikamweleza kuhusu maono mawili ambayo mimi niliyaona wakati tulipokuwa tukingojea pale pembezoni mwa njia ile, ilikuwapisha watu wale wapite.
|
e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza
hapa.
au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.
Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza
kwenye kitabu 
Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw
Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.
Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)
Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )