434. Occurrence, Vision and Prophecy given to Raymond Aguilera on 17 April 1994 at 11:13 AM.

As the airplane was landing in Detroit, the Lord gave me a vision. The Lord showed me some kind of bottomless transparent sink hole with water flowing into it along the sides. Later I could see some kind of debris behind the water.

Prophecy
The Lord said, "It is done."

Vision

We picked up the rental car and proceeded to Toronto. And as we were driving on highway 401, about 100 km southwest of Mississauga, Canada, my warfare prayer language started up without warning. So we stopped the car and took my praise tape out of the trunk and placed it into the car tape recorder and the warfare started once again, as we proceeded toward Mississauga. We were no more than five minutes on the highway when I got hit in the throat, which made me gag, for I stopped breathing, within a few seconds my lungs filled with air, and the warfare proceeded. It got louder and louder, and with power with that Japanese samurai tongue, which I have heard so many times.

During this battle the Lord showed me a torch.

Then the Lord said, "Swing it and fight your way through, for nothing can stop you. Swing the torch and fight, Ray!"

I could see this lit torch, in the spirit, in front of me and it was swinging from side to side, as my Christian brother prayed, in English, and drove the car, as I prayed with all kinds of strange sounds coming out of my prayer language.

We listened to praise music as we both prayed, through this demonic occupied 20 km wide perimeter. The Lord placed the impression in my spirit that the area was blocked by Him, so the demonic reinforcements could not enter the war zone of Mississauga, and that I had to fight my way in.

The impression from the Lord was that He was protecting this area so the outside demonic reinforcements could not help the isolated demons inside the perimeter. The demons inside could only fight with what they had inside the perimeter, and that the territorial spirits inside were cut off and were left to there own resources.

We arrived at Mississauga about 30 minutes before the Vineyard Fellowship Sunday evening service started. I mentioned to my Christian brother that the enemy had taken me out of the war before I even got to Mississauga. For my lungs were sore and my voice was almost gone, from the warfare we had encountered an hour earlier, when we entered the protected perimeter. I was totally wasted.

We quickly washed up and proceeded to the Sunday church service. The service had already started so we took seats in the back of the church. I tried to stand and worship, but I was too exhausted, so I sat down and tried to pray for instructions, and almost fell off my seat asleep several times.

I kept telling myself, "Make yourself strong. I am here to intercede, not to sleep."

I took a deep breath, in my seated position, and the Lord gave me a Prophecy.

 

434. Matukio, Maono na Unabii aliopewa Raymond Aguilera tarehe 17 Aprili 1994, saa 5:13 asubuhi.

Wakati ndege yetu ilipokuwa inatua kwenye uwanja wa Detroit, Bwana alinipa maono. Bwana alinionyeshea kitu cha namna ya shimo lisilokuwa na mwisho amablo ni angavu kama kioo ambayo ilikuwa na maji yaliyokuwa yakiingia ndani mwake kutoka pande zote. Baadaye nikaona uchafu wa kila aina nyuma ya maji hayo.

Unabii
Bwana akasema, "imekwisha."

Maono

Sisi tulichukua gari la kukodisha na kuendelea na safari ya kwenda jijini Toronto. Na wakati tukiwa tunaendesha kwenye barabara namba 401, kitu kama kilometa 100 kusini mashariki ya Mississauga, Kanada, lugha yangu ya maombi ilianza bila ya kuitarajia au bila ya tahadhari yeyote. Kwahiyo sisi tulisimamisha gari na kuchukua kanda ya nyimbo za sifa kwenye buti ya gari na kuiweka kwenye kinasa sauti ya gari na hapo hapo vita vikaanza tena wakati tukiwa tunaelekea Mississauga. Sisi tulikuwa hatupo zaidi ya dakika tano kutoka pale tulipoingia kwenye barabara kuu, mara kitu fulani kikagonga koo langu ambalo lilinifanya ni kabwe, kwa maana nilishindwa kuhema, ndani ya sekunde chache tu hivi mapafu yangu yalijaa hewa na vita vikaendelea. Sauti ya lugha yangu hiyo ikaendelea kuwa kali zaidi na zaidi na kwa nguvu, ikitumia sauti ile ya mwanajeshi wa asilia wa kijapani aitwaye “samurai” ambayo mimi nimeisikia mara nyingi.

Wakati wa mapambano Bwana alinionyeshea mwenge (torch).

Kisha Bwana akasema, "Uizungushe na upiganie njia yako ya kupitia, kwa maana hakuna lolote litakalofanikiwa kuweza kukuzuia wewe. Zungusha mwenge huo na upingane, Ray!"

Nilikuwa nauona mwenge huo, katika ulimwengu wa kiroho, mbele yangu na ilikuwa inajizungusha kwenda upande huu na ule, wakati yule ndugu yangu katika Krsto akiwa anaomba, katika lugha ya Kiingereza, na huku akiendesha gari, na mimi nikiwa ninaomba katika lugha ya sauti za kila aina ambayo ilikuwa ngeni ikiwa inatokea kwenye sauti yangu ya maombi ya lugha.

Tukawa tunasikiliza nyimbo za sifa wakati sisi wote tukiwa tunaomba, na huku tukiwa tunaendesha kupitia kwenye eneo hilo lenye mzunguko wa kilometa 20 lilokuwa na mapepo. Bwana akaweka hisia ya kwamba amelifunga eneo hilo moyoni mwangu, ili mapepo ya kuongeza nguvu wasiingie kwenye eneo hilo la vita la Mississauga, na kuwa inanibidi ni piganie njia yangu ya kupitia eneo hilo.

Hisia nilizokuwa na pata kutoka kwa Bwana ilikuwa ni kwamba Yeye analinda eneo hilo ili mapepo kutoka nje ya eneo hilo wakutoa msaada wasipate kuingia kwa ajili ya kutoa msaada kwa mapepo wachache waliokuwa humo ndani ya eneo hilo. Mapepo waliopo ndani inabidi wapigane na kile walichonacho ndani ya mzunguko huo, na kuwa mapepo wanaolinda eneo hilo watakuwa wametengwa na walikuwa wamebakia kutumia jeshi na nguvu waliyonayo ya humo ndani.

Sisi tulifika Mississauga kitu kama dakika 30 kabla ya kuanza misa ya jioni ya Jumapili ya kwenye kanisa la “The Vineyard Fellowship”. Mimi nilimweleza yule rafiki yangu kuwa adui alikuwa amenitoa kwenye vita hata kabla hatujafika Mississauga. Kwa maana mapafu yangu yalikuwa yameanza kutoa malenge lenge na sauti yangu ni kama ilikuwa imekauka kutokana na vita vile tulivyokuwa tumekumbana nayo kama saa mmoja kabla ya wakati tulipoingia kwenye eneo hilo linalolindwa. Mimi nilikuwa nimechoka kabisa.

Sisi tukanawa haraka haraka na kisha tuka harakisha kwenda kwenye misa ya Jumapili. Misa ilikuwa imekwisha anza hivyo tukachukua nafsi ya kwenye vitu vya mwisho wa kanisa hilo. Mimi nikajaribu kusimama huku nikiabudu, lakini nilikuwa nimechoka sana, kwa hiyo nikaamua kukaa na kisha nikajaribu kuomba kwa ajili ya maelekezo, na mara nyingi nikakaribia kuanguka kutoka kwenye kiti kwa sababu ya usingizi.

Nilikuwa najiaambia kuwa, "Uwe imara. Mimi niko hapa ilikufanya maombi kwa ajili ya wenzangu na wala siyo kuja kulala."

Mimi nikavuta pumzi kwa nguvu, wakati nikiwa nimekaa na Bwana akanipa unabii.

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.