619. Dream given to Raymond Aguilera on 22 October 1994 at 6:30 AM.

A dream of an army ruling a city. It reminded me of how Germany occupied Europe during World War II. I found myself in a University sitting at a desk which would seat three people. It was a narrow room that looked like a passenger train with seats on each side. As I looked up, the door facing me opened and three soldiers walked in. They were walking from desk to desk and ordering everyone to take some kind of white tablet. It looked like an ant-acid tablet. The tablets were carried in a tin cup that looked like a tuna fish can. There were only ten to fifteen tablets in the tin cup and people had to place a tablet in their mouths then replaced the tablet into the tin cup. Everyone had to use the same tablets without question. It looked so gross as they went from desk to desk.

Then I found myself in a large lunch room with officers and army people eating turkey and other good food. For some reason I wasn't invisible anymore. Two soldiers were speaking to me, telling me what they had done during the day.

I thought to myself, "They think I am one of them."

I remember thinking, "Slip out of here before they find out you are not one of them."

Then I found myself outside on a street that was being repaired. I could see a circular auger ripping up an area that needed repair. And off to one side of the street I saw some non-military people standing. Some soldiers were soaking these people's clothes with tar. Then these people were made to roll on the prepared street. They were coating the street with the tar on their clothes for the asphalt laying. They were also using other soaked tar people as brooms, to coat the street.

Then I found myself back at the University where people weren't allowed to walk freely.

In the next image, I found myself on a street watching a crowd of people as soldiers rode up on horse back and started shooting them down. Then they rode off like they did nothing wrong. Everything in this city was regimented. The expressions on people's faces were like the people in the movie, Schlindler's List.

I could see people helping a pregnant woman and other people in need, but it was done discreetly. This was a very, very sad dream of how people can treat people. The pride and the arrogance was well written, all over these soldiers.

I remember wanting to leave the city because of all the violence. Two young women offered me a ride out of the city in their open car. The driver said that she needed gas, so we stopped at a gas station to see if we could get some gas.

I got out of the car to stretch my legs. I saw a small open building with three walls that looked like a small garage. Once inside the building, I noticed it was a place where people were tortured and killed. I turned to leave when a young boy appeared behind me. He started telling me that he was in charge of the small building. He acted very proud of his job and stated he had just executed his parents the day before. Trying not to appear shocked, I asked him how old he was. He said that he was sixteen.

Then a women came toward us and said she was his mother, and also acted so proud. But I remembered that the young man had just stated that he had killed his parents the day before. I couldn't understand why the women said one thing and the boy another, but the boy seemed to be telling the truth. This was one city a person wouldn't want to live in or want to be caught doing something wrong. (over)

 

619. Ndoto aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Oktoba 1994, saa 12:30 asubuhi.

Ndoto kuhusu mji fulani uliokuwa unatawaliwa kijeshi. Ulikuwa unanikumbusha kuhusu ni jinsi gani Wajerumani walivyoikalia Ulaya kijeshi wakati wa vita vikuu vya Pili. Nilijikuta kwenye Chuo Kikuu fulani; huku nikiwa nimekaa kwenye dawati iliyokuwa na uwezo wa kuketisha watu watatu. Chumba hicho kilikuwa chembamba kama chumba cha kwenye bogi la treni ya abiria ambayo ilikuwa na viti vilivyokuwa vinaangaliana. Wakati nilipokuwa na angalia, mara mlango uliokuwa ninatazamana nao ulifunguka na askari watatu wakaingia. Walikuwa wanaenda kutoka dawati hili hadi dawati lile wakiwa wanawamuru watu wachukue kitu kama kidonge fulani cheupe ya dawa. Ilikuwa inaonekana kama ile kidonge cha dawa ya kuzuia kiungulia. Vidonge hivyo vilikuwa vinachukuliwa kutoka kwenye mfuniko wa kopo unaofanana na kopo la samaki wa aina ya “tuna”. Humo ndani ya kopo hilo kulikuwa na tembe kumi hadi kumi na tano hivi na watu iliwabidi waziweke kwenye midomo yao kama kuimumunya na kisha kuirudisha kwenye mfuniko wa kopo hilo. Kila mtu alilazimika kutumia tembe hizo hizo bila kuuliza uliza maswali. Ilikuwa inatia kinyaa na udhia wakati wao walipokuwa wakizunguka kutoka dawati hili hadi lile.

Kisha nikajikuta nikiwa kwenye chumba kikubwa cha chakula cha mchana nikiwa pamoja na maofisa na wanajeshi wakiwa wanakula bata mzinga mkubwa pamoja na vyakula vingine vizuri. Kwa namna fulani ambayo mimi sielewi, mimi hapo nilikuwa ninaonekana kwao. Wanajeshi wawili walikuwa wananisemesha, kunieleza kazi walizo kuwa wanafanya mchana ule.

Mimi nikajiwazia kuwa, "Wanadhania kuwa mimi labda ni mwenzao siyo."

Mimi nakumbuka nikaanza kufikiria "Nijiondoe mahala pale kabla hawaja tambua kuwa mimi sikuwa mmoja wao."

Kisha nikajikuta nikiwa nje kwenye mtaa fulani ambao ulikuwa unafanyiwa matengenezo. Nilikuwa naona mtambo wa mfano wa kekei au ufagio wa mviringo wa kutafuna na kusaga barabara ya lami inayotaka kufanyiwa matengenezo. Na kwenye upande mwingine wa mtaa nilikuwa ninaona watu ambao siyo wanajeshi wakiwa wamesimama. Wanajeshi wengine walikuwa wanawamwagia lami watu hao, kwenye nguo zao. Na kisha watu hao wakatakiwa kujiviringisha kwenye eneo hilo lililo tayarishwa kupakwa lami kwenye mtaa huo. Walikwa wanapakaa lami mtaa huo; kwa lami iliyoko kwenye nguo zao.  Na walikuwa wanawatumia watu wengine waliojazwa lami lami mwili mzima kama mifagio ya kufagilia barabara zao, ili kuitayarisha kupakaliwa lami mtaa huo.

Kisha nikajikuta tena kwenye hicho Chuo Kikuu ambako watu walikwa hawaruhusiwi kutembea kwa uhuru.

Katika maono yaliyofuata nilijikuta katika mtaa fulani nikiwa ninawangalia kundi la watu wakati wanajeshi walipokuwa wanaingia kwa mafarasi na kuanza kuwafyatulia risasi. Kisha wakaondoka bila kujisikia kama wamefanya lolote kibaya. Kila kitu katika mji huo kilikuwa kinaendeshwa kijeshi na kwa mabavu. Nyuso za watu wa mji huo ilikuwa imetanda hofu kubwa kama ilivyo katika sinema ile ya “Schlindler's List”.

Nilikuwa naweza kuona watu wakimsaidia mama fulani mjamzito na watu wengine walio kuwa wanahitaji msaada, lakini ilikuwa inafanyika kwa siri sana. Hii ilikuwa ndoto ya majonzi makubwa ya jinsi watu wanavyo weza kuwafanyia wenzio mambo ya unyama mkubwa kiasi hicho. Majigambo, majivuno na kujikwenza yalikuwa yameandikwa wazi wazi juu ya nyuso za wanajeshi hao.

Nakumbuka nilitamani kuondoka kwenye mji huo kwa ajili ya machafuko yaliyoko humo. Wanawake wawili vijana walikubali kunipa lifti ya gari kutoka kwenye mji huo kwenye gari lao lililokuwa wazi kwa juu. Mwanamke yule aliyekuwa anaendesha gari hilo akatuambia anahitaji mafuta kwa hiyo tukasimama kwenye kituo cha mafuta ili kuona kama tunaweza kupata mafuta hapo.

Nilitoka kwenye gari hilo ili nikanyooshe miguu yangu. Nikaona jengo dogo lililokuwa wazi likiwa na kuta tatu tu ambazo inaonekana kama karakana ndogo. Mara nilipoingia kwenye jengo hilo, niliona dalili kuwa hicho kilikuwa ni chumba ambako watu walikuwa wanateswa na kuuawa. Wakati ninageuka ili nitoke humo mara nikamwona mvulana akajitokeza nyuma yangu. Akaanza kuniambia kuwa yeye ndiye mhusika wa jengo lile dogo. Alikuwa anaoneka mwenye kujivunia kazi yake hiyo na kunieleza kuwa aliwaua wazazi wake jana tu. Akijaribu kujifanya asionekana kama alifanya jambo mbaya. Mimi nikamwuliza alikuwa ana umri gani. Yeye akaniambia kuwa alikuwa ana umri wa miaka kumi na sita tu.

Kisha mwanamke fulani akatujia sisi na kusema kuwa huyo kijana ni mwanaye, na kuonekana akimwonea fahari kijana wake huyo. Lakini mimi nikakumbuka kuwa huyo kijana alikwisha sema kuwa aliwaua wazazi wake jana yake. Mimi sikuweza kuelewa ni kwanini mwanamke yule alisema hili na yule kijana akasema lile, lakini yule kijana alikuwa anaonekana kusema ukweli, kwa kweli mji ule ni mahala mmoja ambako mtu asingelipenda kuishi humo au kukamatwa akifanya kosa lolote humo. (Mwisho).

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.