620. Occurrence given to Raymond Aguilera on 22 October 1994 at 12:00 noon.

As I was talking to a Christian brother; he pointed out how strangely my dog was sniffing the air. Then I heard this voice say in the spirit, "Stick your fingers in-between the door and the door jam and slam the door shut. I told my Christian brother what I was hearing in the spirit and we just looked at each other.

About and hour or two later I got real sick. I started getting severe stomach cramps and indigestion problems. We had just started to work on my down stairs room, but I had to stop due to the pain. So my Christian brother went to the store and brought some anti-Acid medicine while I laid down. A few hours later I got up again. I got sick again so I laid down and started to pray in tongues.

Then the Lord said, "Get into the bathtub and fill it with hot water.

So I climbed into a hot bathtub of water and I found myself in spiritual warfare with my warfare tongue praying loudly.

Then the Lord said, "Fill the bathtub until it covers all of your chest so only your neck and head is exposed."

Then the warfare really got intense. The warfare tongue increased and was more focused. It was direct, pointed, fast and loud.

Then the Lord said, "Bless the water in the Name of the Father, the Son, and the Holy Spirit. Then it will become Holy."

So I did it, then I felt this heat come over my head and it wasn't from the hot water, just after the prayer language kick in again. It was very strange and satisfying at the same time. Then warfare got even crazier as my body started shaking the water started splashing all over the place. I tried to raise my hands into the air and the Lord said, "NO! Keep them under the water."

So I placed my arms back under the water and prayed and prayed in tongues.

I kept hearing this voice say, "Shut Reymundo up! Shut Reymundo up! Shut him up, shut him up!"

And my prayer language was just going crazy and my body and hands were going all over the place under the water. I kept wanting to raise my hands, but the Lord kept telling me, "Keep them under the water."

So I just kept them under the water and I prayed and prayed.

I kept telling the Lord, "Keep my body together, keep my body together!"

For my body felt like it was going to explode. I was praying so loud, so fast, so pointed I didn't believe my body could stay together.

So in my mind, I kept telling the Lord, "Keep me together, keep me together!!"

During this time, I prayed for the Christian brothers that were helping me in this prophetic ministry and their families. I prayed for my relatives and all the relatives of my friends that are in this ministry. Then the prayer language even got harder and more intense. I didn't believe my body would be able to stay in the war or battle because of the intensity. But somehow the Lord kept me together.

During this battle I kept seeing in the spirit nuclear explosions going off in Africa, South America, Europe, China, United States, and Canada. These nuclear explosions were going off all over the place and the prayer language kept getting crazier and crazier.

I could see myself giving Angels orders, to do this and to do that. But I didn't know what I was telling them. My flesh knew it was giving instructions, but it didn't know what the instruction were. For they were given in the spirit.

I remember thinking as I spoke to my spirit; as my prayer language was going crazy directing the Angels, "Do whatever the Holy Spirit says because I don't know what to tell you."

But my flesh did understand that the Holy Spirit was giving instructions to my spirit to instruct the Angels and that Angels were following the instructions.

I don't know if the Angels were using arrows or bullets of some kind. I could clearly see that when these demonic forces were hit with something that on impact they totally exploded with parts flying in every direction. These body parts or spirit parts or whatever you call them were flying all over the place during this warfare.

The Lord was really cleaning House. During this one part of the warfare I could see the Angels in front of me doing battle. As the Angels moved forward in battle, they left behind them demon graves with grave stones on top of these destroyed demons. I don't know how I could see this, but I was dancing on top of their graves moving at a safe distance behind the Lord's Angels. Like I said, I was viewing myself dancing and praising the Lord on top of their graves and seeing this from the air in the spirit all at the same time.

During this time, I kept thinking about how I got the tar beat out of me the week before. And now I was saying to myself, it's my turn or the Lord's turn! The war just went on and on. Then my prayer language just stopped just as fast as it started. I was so tired afterwards. I couldn't even get out of the bathtub. I was totally exhausted. I surely got the tar beat out of me last week, but it went the other way this time. Well, I'll see if I can get some rest. I guess that's all. (over)

620. Matukio aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 22 Oktoba 1994, saa 6:00 mchana.

Wakati nikiwa ninaongea na ndugu yangu fulani katika Mkiristo, yeye akaliambia jinsi ilivyo kuwa cha ajabu kwa namna mbwa wangu alivyokuwa akinusa nusa hewani. Kisha nikasikia sauti hii ikinisemesha katika ulimwengu wa kiroho, "Weka vidole vyako katikati ya mlango na fremu ya mlango na kisha ufunge mlango huo kwa nguvu.” Mimi nikamweleza yule rafiki yangu katika Kristo kile nilichokuwa ninakisikia katika ulimwengu wa kiroho na sisi tukawa tunaangalia kwa mshangao.

Baada ya saa mmoja au mbili hivi mimi niliugua sana kwa ghafla. Mimi nilianza kuugua tumbo la kusokota kutokana na kuvimbiwa vibaya sana. Sisi ndiyo kwanza tulikuwa tumeanza kufanya kazi kwenye chumba changu cha chini, lakini ilinibidi niache kazi hiyo; kutokana na maumivu makali ya tumbo. Kwa hiyo yule ndugu yangu katika Kristo ilibidi aende kwenye duka la dawa na kuninunulia dawa ili kutibu kule kuvimbiwa kwangu; na huku mimi nikiwa nimelala huku nikigaragara kwa ajili ya maumivu. Baada ya masaa machache baadaye, mimi niliamka tena. Nikaanza kuumwa tena kwahiyo ikanibidi nilale na kuanza kuomba kwa lugha.

Ndipo Bwana akasema, "Nenda bafuni na kisha ingia ndani ya sahani la bafu na baada ya hapo niijaze kwa maji moto.”

Kwa hiyo mimi nikaingia ndani ya sahani ya kuogea na kuijaza maji moto na kujikuta nikiwa kwenye vita vya kiroho na lugha yangu ya mapambano ikiomba kwa sauti kubwa.

Kisha Bwana akasema, "Jaza sahani hiyo ya bafu mpaka ifunike kifua chako chote hadi shingo, kichwa tu ndicho kijitokeze nje."

Ndipo hapo mapambano yakaanza kuwa makali sana. Lugha ya mapambano ikaongezeka kwa ukali na ilikuwa imelenga kabisa. Ilikuwa ni ya mmoja kwa mmoja, ya haraka naya nguvu na yenye sauti kubwa.

Kisha Bwana akasema, "Bariki maji katika Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu."

Kwa hiyo mimi nikafanya hivyo, ndipo nikaanza kusikia joto likianza kujitokeza juu ya kichwa changu na wala haikuwa inatoka kwenye maji yale ya moto, mara baada ya hayo lugha yangu ya mapambano ikaanza mara. Ilikuwa ni mambo ya ajabu lakini yalikuwa yanatikisa sana moyo wakati huo huo. Kisha lugha ya mapambano ikaanza kukazana sana na mwili wangu wote ukaanza kutikisikia kwa nguvu kiasi ambacho na yale maji yakaanza kutupwa tupwa kila mahali kwenye eneo hilo. Mimi nilijaribu kuinua mkono wangu hewani, Naye Bwana akaniambia, "HAPANA! Weka mikono yako chini ya maji."

Kwahiyo mimi nikarudisha mikono yangu chini ya maji na kuomba na kuomba katika lugha.

Mimi nikawa ninaendelea kusikia sauti iliyokuwa inasema, "Mnyamazisheni Reymundo! Mnyamazisheni Reymundo! Mnyamazisheni yeye, mnyamazisheni yeye!"

Na lugha yangu ya maombi ikawa inaendelea kwa nguvu zaidi na zaidi na mwili wangu na mikono yangu ilikuwa inaenda huku na huku ndani ya maji. Mimi nikawa ninazidi kutamani kuyanyanyua mikono yangu juu ya maji, lakini Bwana akawa anaendelea kuniambia, "Weka mikono yako chini ya maji."

Kwa hiyo mimi nikawa naendelea kuyaweka mikono yangu chini ya maji na kuomba na kuomba.

Nikawa ninaendelea kumwambia Bwana, "Weka mwili wangu pamoja, weka mwili wangu pamoja!"

Kwa maana mwili wangu ulikuwa unasikika kama ulitaka kulipuka. Mimi nilikuwa ninaomba kwa sauti kubwa sana, Na kwa haraka sana, tena kwa uhakika kiasi cha kudhania kuwa labda mwili wangu usingeliweza kukaa pamoja.

Kwa hiyo katika mawazo yangu nikawa ninaendelea kumwambia Bwana, "Niweke pamoja, niweke pamoja!!"

Wakati huo mimi nikawa ninawaombea ndugu zangu katika Kristo wanaosaidia katika huduma hii ya Unabii pamoja na familia zao. Nikaomba kwa ajili ya ndugu zangu wa familia yangu na jamaa za marafiki zangu wale walioko katika huduma hii. Kisha lugha ya maombi ikazidi kuwa kali na ya kasi kubwa zaidi. Mimi sikuamini kama mwili wangu ungeliweza kustahimili haya yote na kukaa pamoja katika mapambano haya au katika vita hivi kwa sababu ya uzito wa mapambano yenyewe. Lakini kwa njia nisiyoifahamu Bwana aliweka mwili wangu pamoja.

Wakati wa mapambano haya, mimi nilikuwa naendelea kuona milipuko ya kinuklia katika Afrika, Amerika ya Kusini, Ulaya, China, Amerika, na Kanada. Milipuko hii ya kinuklia ilikuwa inalipuka kila mahali na lugha yangu ya mapambano ikawa inaendelea kuwa kali zaidi na zaidi.

Mimi nilikuwa ninajiona nikiwa niwapa amri ya Malaika kutekeleza na kufanya hivi na vile. Lakini mimi sikuwa ninajua ni nini nilichokuwa ninawaambia. Mwili wangu ulikuwa unajua unatoa maagizo au maelekezo, lakini haikujua maelekezo yenyewe yalikuwa ni nini. Kwa maana yalikuwa yanatolewa katika ulimwengu wa kiroho.

Nakumbuka nikishikwa na mafikira wakati wakati nikiwa ninaisemesha roho yangu na wakati lugha yangu ya kuomba ikiwa imekazana sana, ikiwaelekeza Malaika, "Fanyani yote yale ambayo Roho Mtakatifu anayosema kwa sababu mimi sijui la kuwaambieni."

Lakini mwili wangu ulikuwa unajua kuwa Roho Mtakatifu alikuwa akitoa maagizo kwa kupitia kwenye roho yangu ili kuwaelekeza Malaika, nao walikuwa wanafuata maelekezo hao.

Mimi sielewi kama Malaika walikuwa wanatumia mishale au risasi ya aina fulani. Yote niliyokuwa ninaona kwa uwazi ni kuwa mara hayo majeshi ya mapepo wachafu wanapopigwa kwa kitu fulani ambacho kina wa gonga, wao wanasambaratika kabisa na vipande vyao vikiwa vinaruka kila upande. Vipande hivi vya miili au roho au sijui vinaitwaje vilikuwa vinaruka kila mahali wakati huo wa mapambano.

Bwana kwa kweli alikuwa anaonekana akisafisha Nyumba. Wakati fulani wa awamu mmojawapo ya mapamabno, nilikuwa ninaona Malaika mbele yangu, wakifanya mapambano. Wakati Malaika walipokuwa wanasonga mbele katika mapambano haya, waliacha nyuma yao makaburi ya mapepo yakiwa na mawe ya kutambulisha makaburi juu ya makaburi yao hao ya mapepo yaliyoangamizwa. Mimi sielewi ni kwa namna gani, lakini ninaweza kuona haya, nami nilikuwa ninaruka ruka na kucheza dansi juu ya makaburu yao hayo na huku nikiwa ninakaa nyuma kwenye eneo la usalama iliyo nyuma ya Malaika hao wa Bwana. Kama nilivyo kwisha sema mimi nilikuwa najiona nikicheza dansi na kumsifu Bwana juu ya makaburi hayo na nikiwa ninayaona hayo yote kutoka juu angani katika ulimwengu wa kiroho wakati huo huo.

Wakati huo, nilikuwa huko ninafikiria ilikuwaje wiki mbili tu zilizopita nilishindwa vibaya sana katika mapambano yale. Na sasa nilikuwa ninajisemeshea mwenyewe, ni zamu yangu au ni zamu ya Bwana! Mapambano hayo yaliendelea na kuendelea tu. Kisha lugha yangu ya maombi mara ikakoma kwa ghafla kwa haraka kama ilivyoanza. Mimi nikawa nimechoka sana baada ya hayo. Mimi nikawa nimeshindwa hata kutoka kutoka kwenye ile sahani ya kuogea. Mimi nilikuwa nimechoka sana sana. Mimi kwa kweli nilipigwa mpaka nikasambaratika wiki iliyo pita, lakini mambo yalikuwa tofauti safari hii. Naam ebu tuone kama nitaweza kupata mapumzika kidogo. Nadhani haya ni yote. (mwisho)

 

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.