652. Dream given to Raymond Aguilera 13 December 1994 at 1:14 AM

I had a dream of a garage that was attached to an enormous house and I was working for the owner and/or was in charge of this garage. I was not sure what was going on, but there were a bunch of men that looked like bikers that were leasing this garage from the owner of the house. The garage was full of mechanic's tools and auto parts. These men were working on Corvette cars. I could see this very pretty Corvette that belonged to the owner of the house parked outside in the driveway of the garage.

These men were stealing from this large house as they worked in the garage. I over heard these men say that they were going to steal the motor from the Corvette that belonged to the owner. So I told the owner's son what the men were planning to do. So the owner's son told them to move out of his father's garage. For he didn't want them working there anymore.

They said, they didn't want to go. So the owner's son got his servants (and I believe I was among them) and told them to pack up and go. So they finally decided to leave, but as they were leaving they kept trying to steal things. So the son had the servants count all of the parts to make sure they didn't take anything that didn't belong to them. These mechanics kept talking among themselves, of what they were going to steal. For they were very big and strong and all the son's servants were small. For some reason they didn't push them out of the way for they were afraid (somehow) of the law.

For some reason over the garage door opening a frosted plastic sheet fell where no one could see inside. The next thing I knew these men had all the tools and motors in this truck, with other things hanging from the side of this truck and they were driving away very slowly.

I called to them and said, "Stop! You mustn't take that motor for it belongs to the owner."

It was a bright red motor that belonged to a Corvette car that was parked in the driveway. They slowed down, but didn't stop, and tried to make excuses. They said that they didn't have time to remove it and that they would bring back later. But I knew they wouldn't. They were stealing it. I remember that I tried to tie a strap from one motor that was on the ground to the red motor on the truck hoping it would pull the motor off the truck, but I couldn't do it in time for there were all kinds of engine blocks and auto parts in the way. So they took off.

I said to myself, "I don't know what to do."

So the son called the police and the police stopped them down the long road leading from the house. They asked them what they were doing with all these stolen parts and I woke up (over)

 

652. Ndoto aliyopewa Raymond Aguilera tarehe 13 Desemba 1994, saa 7:14 usiku.

Mimi nilikuwa na ndoto kuhusu karakana fulani iliyounganishwa na jumba fulani kubwa sana nami nilikuwa ninafanyakazi kwa tajiri huyo na/au nilikuwa ndiye kiongozi wa karakana hiyo. Mimi nilikuwa sina uhakika na kile kinachoendelea humo, lakini kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanaonekana kama ni wasafirishaji walio kuwa wakikodisha karakana hiyo. Karakana hiyo ilikuwa inaonekana kujazwa na vifaa vya kutengenezea magari kama maspana na vipuli vya kila aina. Watu hao walikuwa wanafanyakazi ya matengenezo ya magari ya aina fulani iitwayo na Conveta. Mimi nikawa naona gari fulani nzuri sana aina ya Conveta ambayo ni mali ya tajiri wa nyumba hiyo ikiwa imeegeshwa kwenye njia ya kuingilia kwenye karakana hiyo.

Watu hawa walikuwa wanaiba kutoka jumba hilo la mwenye karakana, huku wakiwa wanafanya kazi. Mimi nikawasikia wakizungumza kuwa wao wangelienda kuiba injini ya gari hilo aina ya Corveta ambayo ni mali ya huyo tajiri mwenye karakana na nyumba. Kwa hiyo mimi nikamwambia mwanaye tajiri huyo yakuwa walikuwa wanafanya njama ya kuiba injini ya gari la baba yake. Kwa hiyo kijana huyo akawaambia waondoke kwenye karakana ya baba yake. Kwa maana yeye hakutaka waendelee kufanyakazi humo tena.

Wao wakasema, wao hawakupenda kuondoka. Kwa hiyo mwana wa yule mwenye nyumba na karakana akawachukua watumishi wake (na ninaamini mimi nilikuwa mmoja wao) na kuwaambia wafungashe na waondoke. Kwa hiyo mwishoni wao wakakubali kuondoka, lakini wakati wakiwa wanaondoka walikuwa wanajaribu kuiba vitu hapa na pale. Kwa hiyo mwana wa tajiri yule akawafanya watumishi wake wahesabu vipuli vyote kuhakikisha kuwa hawachukui lolote ambalo siyo mali yao. Wale mafundi wakawa wanaendelea kuongea wao kwa wao ya kuhusu wakaibe nini hapa na pale. Kwa maana wao walikuwa wakubwa sana na wenye nguvu zaidi kuliko wale watumishi wa mwana wa yule tajiri na watumishi wake walikuwa wadogo. Kwa sababu ambayo mimi sikuelewa wao hawakuwa sukuma watoke njiani kwa maana wao (mafundi) walikuwa wanaogopa (kwa namna fulani) mkono wa sheria.

Kwa sababu nisiyo ijua ghafla kitu kama pazia la plasti ambalo huwezi kuona ndani lilifunika mlango ambao ulikuwa umefunguliwa. Kitu kilicho fuata ambacho ninakijua watu hao walikuwa wamepakia spea zote na vifaa vyote vya karakana ile pamoja na mainjini kwenye lori fulani na vitu vingine vikiwa vinaning’inia pembeni mwa gari hilo na wakawa wanaondoka na lori hilo wakiendesha pole pole sana.

Mimi nikawaendea na kuwaambia, "Acheni! Msiibe injini hiyo kwa sababu ni mali ya tajiri wa karakana ile."

Ilikuwa ni injini iliyokuwa nyekundu na yenye kumeremeta ya gari ile ya aina ya Corveta iliyoegeshwa kwenye njia ile karibu na karakana, mali ya yule tajiri. Wao walipunguza mwendo wao, lakini hawakusimama, na kuanza kutoa visingizio. Wao wakasema hawakuwa na wakati wa kuiondosha, lakini wao wangeli rudisha baadaye. Lakini mimi nilijua kuwa wasinge rudisha. Walikuwa wameiiba. Mimi nakumbuka kuwa nilijaribu kufunga kamba kutoka kwenye injini iliyokuwa hapo chini na kuiunganisha na injini ile nyekundu kwenye lori kwa matarajio kuwa ingelivuta ile injini iliyokuwa kwenye lori, lakini mimi sikuweza kufanyakazi hiyo mapema kwa maana kulikuwa na bloku za injini kila mahali pale na spea nyingine nyingi njiani. Kwa hiyo wao wakaondoka.

Mimi nikajisemea, "Mimi sijui la kufanya."

Kwa hiyo yule mwana wa tajiri akaita polisi na polisi wakawasimamisha kwenye barabara ile ndefu itokayo kwenye nyumba hiyo. Wakawahoji kuhusu walikuwa wanataka kufanya nini na spea hizo zote walizoiba nami mara nikaamka (mwisho).

 


e-mail:Ray@prophecy.org
Kusaidia huduma hii Bonyeza hapa.  

au andika kwa: Raymond Aguilera, S.L.P.20517, El Sobrante, CA. 94820-0517, USA.

Kuagiza Vitabu vya Unabii bonyeza kwenye kitabu

Haki ya kunakili © 1989-2001, Raymond Aguilera, Prophecy.org (sm) Haki zote zimehifadhiw


Kurudi Kwenye Jalada la Kitabu cha Unabii.

Kurudi Kwenye Orodha ya Yaliyomo. (1-1000)

Kurudi kwenye Orodha ya Yaliyomo 2 (1000 + )

  Kwenda kwenye Unabii unaofuata.